Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
Tanzia
Ndugu Wanaudasa,
Ninasikitika kuwataarifu habari za msiba wa Dr. Richard Mgaya wa Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta kilichotokea usiku wa kuamkia jana. Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara (Dr. Honest Kimaro) kifo cha Dr Mgaya kimesababishwa na ajali ya gari.
Siku ya jana kulisambaa picha kwenye mitandao ya kijamii za gari lilipopata ajali eneo la Mbezi Afrikana baada ya kugongana na lori na kuwaka moto. Mashuhuda walishuhudia gari likiwaka moto na hivyo dereva aliungua moto na kuteketea na hakuweza kutambulika. Hivyo watu wakasambaza ujumbe kwa kutaja plate number za gari lililoungua ili kutafuta utambulisho wa dereva.
Kwa masikitiko makubwa, imejulikana kwamba dereva wa gari hilo alikua ni Dr. Richard Mgaya. Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta na jamii ya CoICT kwa ujumla imeshtushwa sana na msiba huu.
Dr. Mgaya alijiunga na idara miaka kama minne hivi iliyopita akitokoea masomoni Marekani na alikua ni mtaalamu kijana wa Artificial Intelligence ambayo ni moja ya specialities za computer science zenye wataalamu wachache sana wa kiwango cha PhD hapa nchini mwetu (kama wapo zaidi ya yeye). Taarifa za kwamba aliyeungua kwenye gari hili alikua ni Dr. Mgaya zimeifikia familia yake leo mchana.
Mungu mwenyewe awe faraja kwa ndugu, jamaa, wafanyakazi wenzake na familia nzima ya UDSM.