|
APOSTLE DARMACY |
“kanuni za kibiblia za usimamizi
wa fedha zitakazo linda na kustawisha uchumi wako”
UTANGULIZI:
Kuna mafundisho mengi kuhusu jinsi ya kufanya
biashara,kufanya ujasiriamali,kufanya miradi ,Kujiari n.k yote yaki lenga
katika kuzalisha na kupata fedha au kukuza uchumi.lakini kuna
mafundisho kidogo kuhusu upande wa pili ambao ni wa muhimu sana katika uchumi,jinsi ya kusimamia fedha.matatizo makubwa ni namna ya kusimamia fedha
kuliko jinsi ya kuzalisha fedha.
wengi tuna pata fedha tatizo ni jinsi ya
kuzisimamia,somo hili litazungumzia eneo
hili la pili la “ jinsi ya kutumia
kanuni za kibiblia za usimamizi wa fedha ili kuulinda na kustawisha uchumi
wetu.”
KANUNI KUMI ZA KIBIBLIA USIMAMIZI MZURI WA FEDHA:
Biblia inatoa mwongozo mzuri wa usimamizi wa fedha ambao
tukiufanyia kazi tuta punguza kwa asilimia kubwa matatizo mengi ya kifedha
tuliyo nayo.Matatizo mengi ya kifedha tuliyo nayo yanachangiwa sana kwa namna moja
au nyingine na usimimamizi mbaya wa fedha zetu,wengi wetu tatizo letu kubwa zaidi ni usimamizi wa fedha kuliko
kuzalisha na kupata fedha.
usimamizi mzuri wa fedha utalinda uchumi wako
na kuukuza uzalishaji wako,kipato chako.Hata kama unazalisha sana fedha lakini
kama una usimamzi mbaya wa fedha uchumi
wako utayumba tu.Matatizo mengi ya kifedha tunakimbilia kuombewa na
kukemea,lakini hayo yote bila kujifunza
usimamizi mzuri wa fedha utakuwa hujatatua tatizo katika mzizi.hata ukiombewa kupata mpenyo wa kifedha
matatizo ya kifedha yatarudi baada ya muda mfupi kwa kushindwa kuzitendea kazi
kanuni za fedha.
1. MUNGU NDIYE MMILIKI WA FEDHA ZETU
Fedha ni Mali ya Bwana,sisi tu wasimamizi
tu au mawakili,hivyo tunawajibika na vile tunatumia kila fedha tuliyoaminiwa na
Mungu.( Mathayo 25:1-30 ; Zaburi 24:1,)
2. TAMBUA FEDHA NI SUALA LA KIROHO.
Kwa mtu wa Mungu fedha ni suala la
kiroho,fedha ina athiri na inagusa maisha yako ya kiroho pia.vile unavyo
shughulika na fedha kuna sema zaidi juu ya hali yako ya moyo kuliko ushuhuda
wako.vile unavyoshughulika na fedha zako ni kiashirio cha ukomavu wako kiriho.LUKA 16:10-11
Fedha inaweza kuwa mungu wako,fedha ina
uwezo zaidi kutuvuta taratibu na kwa ujanja kutoka kwa Mungu kuliko kitu
kingine chochote.MATH 6:24,Ina nguvu
ya kuwa Bwana wetu.
Katika mifano
38 ya Yesu,16 inahusu
fedha,katika agano jipya fedha imezungumzwa zaidi kuliko habari za mbinguni na
kuzimu vikiunganishwa pamoja.mara tano
zaidi imezungumzwa kuhusu fedha kuliko maombi,kuna mistari zaidi ya 1500 inayohusu maombi na imani,wakati
kuna zaidi ya mistari 2000 inayohusu
fedha na mali.Aslimia 15% ya
Biblia ni kuhusu fedha.
3. TUNZA KUMBUKUMBU ZOTE ZA FEDHA
Kutunza kumbukumbu ni hatua ya kwanza
kukusaidia katika kuandaa bajeti yako ambayo utaishi nayo.tafuta daftari ndogo
na anza kuweka kumbukumbu za wapi fedha zako zinakwenda,ni kazi ngumu lakini
itakusaidi kwa mipango ya muda mrefu ya kifedha.kiasi gani unatumia kwa mwezi
kwa usafiri?simu?chakula?matibabu?chakula n.k ni lazima ujue wapi fedha yako
inatoka na wapi fedha yako ina kwenda. Nini nina mililki,nini nina dai,nini
nina daiwa,natuamiaje(MITHALI 27:23-24, 23:23,)
4. FANYA TATHIMINI YA MARA KWA MARA YA FEDHA ZAKO:
ni muhimu kufanya tathimini kwa uaminifu
kuhusu uchumi wako,mapato yako,madeni,vitega uchumi vyako n.k. hii itakusadia
kufanya marekebisho unayoyahitaji na
kukusaidia kuishi kwa mpango,kama huwezi kutathimini hutaweza kupanga,ukishindwa
kupanga,tayari umeshindwa kusimamia fedha yako.(MITHALI 21:5 LUKA 14:28)
5. JIWEKEE MFUMO WA KUPANGA BAJETI NA KUUFUATA:
Bajeti kirahisi nikuandika katika karatasi nini unategemea kupata kama
mapato na njisi gani unategemea kutumia.panga matumizi yako.Ni mpango wa jinsi
gani utatumia rasilimali fedha ambazo
unatarajia kupata ,bajeti inapaswa ijumuishi vyanzo vya mapato pia mpango wa matumizi wa mapato mf.mpango wa
chakula,kodi,zaka,utoaji,akiba n.k(Mithali
21:5, Mithali 21:20)
6. JIWEKEE UTARATIBU WA KUWEKA AKIBA
Weka Akiba, kwaajili ya dharura,akiba
kwaajili malengo maalumu, (Mithali
21:20a ;13:11)
Mithali
6. Tenga kiasi cha kuweka akiba anza na kiasi kidogo kwanza.
7. JIFUNZE KUTOA KWA UKARIMU-
(Mithali
11:24-25).kanuni ya uchumi wa Kimungu ni tofauti,kadiri unavyotoa na
sivyo
unavyo jilimbikizia ndiyo uchumi wako unastawi.Kumtolea Mungu,kutoa
kwaajili ya
kuwabariki wengine,kutoa kwaajili ya wahitaji(Mithali 28:27 Mithali
11:25.Mithali 19:17,Mithali 3:9-10),Kutoa kunafungua Baraka za Mungu
katika Maisha
yako.
8. TUMIA FEDHA YAKO KWA HEKIMA NA RIDHIKA NA
ULICHO NACHO:
Zingatia
vipaumbele na umuhimu,Epuka matumizi ya anasa,manunuzi ya bila
mpangilio,manunuzi ya papo kwa papo,usifanye matumizi yaliyo nje,yanayozidi
kipato chako au uwezo wako wa kifedha.Jifunze kuridhika na kuuepuka tamaa.usifuje
fedha kwa matumizi ya ovyo.jifunze kuridhika(Mithali 21:20 ;Waebrania 13:5,Mhubiri 6:9)
9. TUNZA VITU NA MALI AMBAVYO UMEVIGHARIMIA
FEDHA.
Vitu,mali ni fedha,usipovitunza utatoa
fedha tena kununua. Tunza visiharibike ovyo,vitumike kwa uangalifu ili kuokoa
gharama ya matengenezo au kununua upya.
10. EPUKA MADENI.
biblia haijakataza moja kwa moja kuhusu
kukopa,ila kwa uwiano wa maandiko Haiti moyo madeni,bali inakatisha tamaa
kukopa.inazungumza zaidi madhara ya kukopa.Unapokuwa katika deni unakuwa katika
kifungo,Madeni yana haribu uhusiano.usitumie fedha zaidi ya ile unayozalisha
utaishia kwenye madeni.weka akiba kidogo kidogo badala ya kukopa.
MITHALI
22:26-27,ZABURI 37:21,MITHALI 22:7
HITIMISHO:
Pengine umekuwa unapitia katika kipindi
kigumu cha kifedha,uchumi wako umeyumba,kabla ya kuhitaji fedha zaidi unahitaji
kuzifanyia kazi kanuni hizi za usimamizi wa fedha.Mungu anakusubiri ujifunze na
kuzingita kanuni hizi za fedha ili akufungulie mlango mkubwa zaidi wa
kifedha,ni jukumu lako kutii kanuni hizi na hali yako ibadilike au ubaki katika
hali uliyo nayo.Mungu akubaliki unapochukua uamuzi wa kusimamia fedha zako kama
wakili mwaminifu.MUNGU akubariki sana . By pastor Mtitu.
Toa Maoni Hapa Chini