Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE
MAHALI: VIWANJA VYA MPIRA MAJENGO MOSHI.
TAR 19-2-2017
DAY !
SOMO: UTATUZI WA MATATIZO YATOKANAYO NAHALI YA KIROHO YA ARDHI..
Lengo la somo hili ni kupata ufumbuzi wa matatizo yatokanayo na hali ya kirohoya ardhi nakujua namnaya kuyatatua
2 NYAKATI 7; 14-15
Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuomba nitaskia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi zao na kuiponya nchi yao.. 15; sasa macho yangu yatafumbuka na maskio yangu yataskiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.
Neno kuu "NCHI'
Tunaona katika tafsiri ya Biblia za kiingereza neno nchi limetafsiriwa kama ardhi yenye mipaka halali ya umiliki.
Katika Biblia kuna tofauti kati ya nchi na Taifa. Neno hili halijatumika kama Taifa.
Taifa halihusiani na ardhi na ukumbuke pia kuwa Taifa linaweza kuwa ndani ya ardhi ya Taifa jingine kama vile taifa la Israel lilivyokuwa ndan iya ardhi ya Taifa la Misri'.
Taifa linahusisha watu wa aina flani walioamua kujitawala kwa namna moja.
Ndani ya Taifa pia utapata kabila; koo na familia
Hapa ndipo unapogundua kuwahaya yote hayahusiani na ardhi.
Kwa mfano ni kwamba kuna maombi ambayo hayajibiwi mpaka watu washughulike na matatizo yaliyoko katika ardhi husika iwapo ardhi hiyo ina shida..
MATATIZO YATOKANAYO NA ARDHI..
1> Tabia mbaya zinazopata msaada kutoka kwenye hali ya kiroho ya ardhi.
>Ikiwa kuna jambo ambalo Mungu atahitaji ushiriki wako uwe na uhakika kuwa atakutafta kwa namna na gharama yoyote ile.
Joshua 2;1
Matahyo1;1-17
Joshua 6;25
Hapa tunaona ya kuwa kutoka Ibrahim mpaka Yesu yapata vizazi 42
>Uwe na hakika kuwa Mungu alijua vizazi hivi vyote pamoja na jaribu ambalo shetani alitaka kuliinua kupitiaukahaba wa Rahabu.
shetani alitaka kumfanya Rahabu hata kushindwa kujifikiria kuingizwa katika kusudi la Mungu juu yake
> Mungu huangalia mwisho tangu mwanzo.
>Aliona mwisho wa Rahabu asiye kahaba "Mtumishi wake" na hakukuwepo na namna ambayo wana wa Israel wanaweza kulifuta tena jina lake katika historia zao na uzao wao kwa sababu Mungu alikuwa na kusudi naye.
>Gharama ambazo Mungu hutumia kukufatilia ili uweze kurudi kwake hukuonyesha thamani halisi ya kitu alichokuitia kwake kwanihatokubali upotee hata kidogo.
>Kilichomfanya Mungu kwenda Yeriko ni Rahabu
>Alitafta mtu mmoja tu pamoja na kuuangamiza mji mzima
>Mungu yuko tayari hata kuangamiza taifa zima ili ampate hapo mtu mmoja anayemhitaji kwa ajili ya kusudi lake
>Kama alikuwa tayari kumfata Rahabu aliyekuwa kahaba pamoja na shetani kuleta jaribu la ukahaba inashindikanaje kwako?
>Kama Rahabu alifatwa basi tambua ya kwamba haijalishi umekufa kiasi gani atakufata tu kwa Roho wa ufufuo.
.Haijalishi una dhambi kubwa kiasi gani''
2> Mungu alishughulikana ardhi ya Yeriko ili kumfungua Rahabu kutoka kwenye ukahaba..
Joshua 6;1-5
>Je? Kwa nini kwa nini Mungu alishughulika na ardhi ya Yeriko badala ya kushughulika na tabia "ukahaba" wa Rahabu?
>Baada ya Rahabu kuachilia imani yake na kuitoa nyumba yake kama sadaka hatukuona tena akifanya ukahaba.
>Familia yake pamoja na mali zake zote zilifunguliwa
> Hapa tunaona kuwa tabia ya mtoto inaweza ikazima mafanikio ya familia nzima
>Rahabu alipokwama familia yake pia ilikwama sababu Rahabu alikuwa lango la familia yake
> Kuna tabia shetani hukuletea ili kukukwamisha usiweze kufikia kiwango flani cha maisha ambayo Mungu amekupangia'
VITU GANI VILIVYOMFANYA RAHABU KUFUNGULIWA?
1>Unyenyekevu wa Joshua kukubali kuwa kuna vitu vya kiroho vilivyopo katika ardhi ambavyo hakuvijua;
Joshua 5;13-15
Yule malaika alimwonyesha Joshua kuwa kuna kitu katika ardhi ndio maana alimwambia vua viatu vyako.
>Wakati mwingine ni mtihani mkubwa sana kwa Mtumishi/ viongozi wa kifamilia/ viongozi wa serikali/ na wakubwa wa namna yoyote ile kukubali au kunyenyekea kuwa kuna vitu asivyovijua| .
>Pamoja na kwamba Joshua alikuwa kiongozi alionesha unyenyekevu wa hali ya juu wa kutii na kufahamu kuwa kuna mambo hakuyafahamu.
2>Imani ya wana wa Israel juu ya kutii kuuzunguka ule mji
Ebrania 11;30"imani"
>Kwa imani kuta za Yeriko zilianguka
>Kuomba kwakutembea pasipo kuwa na imani haiwezi kukusaidia chochote hata ufanye nini..
>Ilikuwa kazi ngumu sana kwa wale wazee kukubali kuuzunguka ule mji kila siku kama wasingekuwana imani.
3>Wapelelezi kutumia ishara yaagano na Mungu ili kumhakikishia Rahabu ukombozi
Joshua 2;12;17-18
"funga kamba hii" hii kamba ilikuwa yao wakampa
>Naye alionesha kwadai wale wapelelezi alama ya uaminifu
*Kamba** ilisimama badala ya kifungo
*Nyekundu* ilisimama badala ya damu
>Hii inaonesha ya kwamba wale wapelelezi walikuwa katika kifungo na Mungu wao na walipompa kamba walikuwa wanamaanisha kwamba naye"Rahabu" aliingizwa katika agano na Mungu na kuanzia hapo basi mtu yeyote angemtazama basi angetambua moja kwa moja kuwa yeye ni wa Mungu yupi..
>Ile kamba ilimuingiza Rahabu moja kwa moja katika agano na Mungu wa wana wa Israel.
4> IMANI YA RAHABU ILIYOKUWA INAJISEMEA NDANI YAKE AMBAYO ILIMJENGEA IMANI NDANI YAKE.
>Hakutaka ukahaba uamue hatma ya maisha yake
Luka 22;20
>Ile kamba ilirudisha heshima kwa yule dada kama ambavyo damu ya Yesu inavyotuletea heshima tulipodharaulika."Damu ya agano"
Kwa leo tunaishia hapo tukutane tena kesho Mungu awabariki sana.....
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.