Wakiwa Mkoani Iringa wamepata nafasi ya kuzungumza na wanachuo 1,000
kutoka vyuo vikuu vya Iringa na Mkwawa kwenye semina iliyoelezea malengo
hayo ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu
duniani.
Kampeni hiyo imelenga kuwafanya vijana waelewe malengo 17 ya dunia
ambayo kwa sasa yana mwaka mmoja tangu yapitishwe na kuwatanabaisha
wajibu wao katika kufanikisha utekelezaji wake ndani ya mazingira ya
Tanzania.
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro
(kushoto) akisalimiana na mmoja wa wahadhiri wa chuo hicho alipowasili
katika ofisi za Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua
Madumulla akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP), Alvaro Rodriguez.
Semina katika vyuo hivyo ni sehemu ya
mpango madhubuti wa Umoja wa mataifa uliozinduliwa Arusha Mei mwaka huu
na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez wenye
lengo la kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu
malengo hayo ya dunia.
Ujumbe huo wa EU na UN pia ulipata
nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na EU ukiwamo wa
Boma la Kijerumani ambalo lilikarabatiwa kwa ruzuku ya EU kupitia
‘fahari yetu – Southern Highlands Culture Solutions’.
Boma hilo ni moja ya majengo ya zamani
katika mji wa Iringa na lilijengwa na Wajerumani mwaka 1900 kama
hospitali ya kijeshi. Baada ya vita ya Kwanza ya Dunia, jengo hilo
lilibadilishwa matumizi na watawala wapya, Uingereza, na kulifanya kuwa
jengo la utawala.
EU imesema inaona fahari kuwa mmoja wa
wawekezaji wakubwa katika sekta ya sanaa na urithi wa kitamaduni nchini
Tanzania, ikifadhili miradi 10 iliyo chini ya programu ya 10 ya EDF ya
kusaidia masuala ya kitamaduni.
Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akiwa kwenye
mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini
ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (upande wa kushoto katikati)
pamoja na Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce
Temu (kushoto) alipotembelewa ofisini kwake na ugeni huo. Kulia
ni Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever pamoja na Katibu Tawala
Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa, Henry Mditi.
Masuala yanayohusu urithi wa kitamaduni
ni muhimu katika kuchagiza ukuaji wa uchumi, ajira na huku ikifuma
mahusiano ya kijamii, na kutoa fursa ya kuboresha utalii endelevu
mkoani Iringa huku ikileta faida kwa wakazi wa eneo hilo.
Bw. Rodriguez, akizungumza katika
kampeni hiyo alisema kwamba ajenda 2030 ambayo ni ajenda ya maendeleo
endelevu inahitaji ushiriki wa kila mmoja.Aliwapongeza wanachuo hao na
wanazuoni kwa kujikita kutambua malengo hayo ya dunia.
Aidha aligusia umuhimu wa vijana
kushiriki katika masuala ya maendeleo kutokana na ukweli kuwa, kwa taifa
kama la Tanzania vijana ni asilimia 60 ya wananchi wote waliopo.Alisema
kwamba vijana wanajukumu kubwa la kushiriki katika maendeleo hayo kwa
lengo la kuipeleka nchi katika hatua nyingine ya maendeleo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwa
ameongozana na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa,
Henry Mditi kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano Chuo Kikuu cha Iringa.
Hata hivyo alisema kwamba ni wajibu wa kila mtu hasa vijana, kuhakikisha kwamba malengo hayo ya dunia yanafanikiwa .
Alisema Umoja wa Mataifa kwa kusaidiwa
na wadau wake muhimu kama Umoja wa Ulaya, utaendelea kusaidia Watanzania
kuwajibika katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika kuunga mkono
malengo hayo ya dunia.
Mmoja wa washiriki alipongeza Umoja na wa Mataifa kwa kuwafikia vijana wa vyuoni na kuwapa semina hiyo.
“Ninajisikia mtu mwenye
bahati kupata nafasi ya kujifunza maendeleo endelevu kutoka kwa Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini. Nikiwa kama kijana, naona
faraja kuona kwamba viongozi wetu wanafuata maelekezo yaliyofafanuliwa
kwenye malengo 17 ya maendeleo endelevu; naamini kama tukijitahidi
kuyafikia ifikapo 2030, basi Tanzania na duniani kwa ujumla itakuwa
eneo jema la kuishi. Na kwa kuwa sasa natambua kuhusu malengo hayo ya
dunia, ninaweza kutoa mchango wangu kusaidia kuyafikia -najisikia
kuwezeshwa sana.” amesema Mary, mmoja wa washiriki.
Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akisoma taarifa fupi
ya Chuo Kikuu cha Iringa mbele ya ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa na
Umoja wa Ulaya wakati semina kuhusu malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)
ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani kwa
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.
Mkuu wa
wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza kwenye semina ya malengo
ya dunia kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa ambapo aliwaasa wakawe
mabalozi wazuri wa malengo hayo kwenye jamii zao na wanafunzi wenzao wa
vyuo vingine.
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro
akitoa salamu za Umoja wa Ulaya kwa niaba ya Balozi wa Umoja huo, Bw.
Roeland Van De Geer wakati wa semina Malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) kwa wanachuo wa Iringa iliyowezeshwa na EU.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwapiga
msasa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa kuhusu Malengo ya Dunia katika
semina iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjini Iringa.
Mwanafunzi
wa mwaka wa tatu anayechukua Shahada ya Sayansi katika Uchumi na Fedha
wa Chuo Kikuu cha Iringa, Sarafina Sayi akiuliza swali kwa mkufunzi wa
malengo ya dunia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez (hayupo pichani) wakati wa semina hiyo.
Mwanafunzi
wa Shahada ya Sayansi katika Uchumi na Fedha wa Chuo Kikuu cha Iringa,
Geoffrey Kadori akiuliza swali kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard
Kasesela wakati wa semina ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo
ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani kwa wanafunzi wa
Chuo hicho.
Mkuu wa
wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akijibu swali wakati wa kipindi cha
maswali na majibu kwenye semina kuhusu malengo ya maendeleo endelevu
(SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.
Pichani juu
na chini ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa kutoka vitivo tofauti
chuoni hapo waliohudhuria semina ya malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)
ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani kwa
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya
(EU).
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla makabrasha na
majarida yenye ripoti na taarifa mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ripoti na makabrasha
mbalimbali ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kuhitimisha semina kuhusu
SGDs kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.
Mkuu wa
wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatu kulia) katika picha ya
pamoja na ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya pamoja na
Balozi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs Champion), Sabinus Paul
(kushoto) nje ya ukumbi kulikofanyika semina kuhusu SDGs kwa wanachuo wa
Iringa.
Picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa semina hiyo huku wakiwa na mabango ya SDGs.
Muonekano
wa nje wa jengo la Makumbusho ya Mkoa na Kituo cha Utamaduni -Iringa
Boma ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).
Kibao cha Makumbusho ya Mkoa wa Iringa kinachoratibiwa na Mradi wa Fahari yetu kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Iringa
Meneja wa
Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever akielezea dhumuni la mradi Fahari Yetu
unaolenga kuendeleza utamaduni nyanda za juu kusini kwa Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto)
aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni
Afisa Miradi, Anna Muro (mwenye suti) ambao ndio wafadhili wa jengo
hilo la Makumbusho ya Mkoa wa Iringa. Wengine katika picha ni wahadhiri
na maprofesa kutoka Chuo Kikuu cha Iringa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akisaini
kitabu cha wangeni ndani ya Makumbusho ya mkoa wa Iringa.
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro
akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Makumbusho ya mkoa wa
Iringa.
Meneja wa
Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever akitoa maelezo picha mbalimbali
zinazoelezea historia ya mkoa wa Iringa wakati wa utawala wa Chifu
Mkwawa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini
ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro walipotembelea makumbusho ya mkoa
wa Iringa
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akisoma
historia mbalimbali za enzi za utawala wa kichifu ndani ya Makumbusho ya
Mkoa wa Iringa.
Mwongoza
wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Jacob Shenyagwa (mwenye
miwani) akitoa maelezo ya picha mbalimbali kwa ugeni huo wa UN na EU
uliotembelea makumbusho hiyo iliyojengwa chini ya ufadhili wa Umoja wa
Ulaya (EU).
Mwongoza
wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Deonis Mgumba akitoa maelezo
ya vifaa mbalimbali vilivyokuwa vikitumika enzi za utawala wa kichifu
kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez
(kushoto) na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa,
Henry Mditi (katikati) walipotembelea makumbusho hayo mjini Iringa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro
wakitwanga mahindi kienyeji katika moja ya kinu kilichokuwa kinatumika
enzi hizo za utawala wa kichifu kilichopo katika makumbusho hayo.
Mwongoza
wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Matatizo Kastamu akitoa
maelezo ya picha mbalimbali zenye kumbukumbu za utawala wa kichifu na
historia ya mji wa Iringa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya
(EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro.
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro
(kushoto), Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu
na Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever wakipitia vipeperushi
vyenye maelezo ya kina ya Mradi wa Fahari Yetu unaoendesha Makumbusho na
Kituo cha Utamaduni mkoa wa Iringa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro
katika picha ya pamoja kwenye sanamu maalum za mavazi ya kipindi cha
utawala wa Chifu Mkwawa walipotembelea Makumbusho ya mkoa wa Iringa.
credit to