UMOJA
wa Mataifa nchini Tanzania unaendelea na uelimishaji wa wananchi kuhusu
malengo ya Dunia yaliyoelezwa katika Maendeleo Endelevu (SDGs), malengo
ambayo sasa yana takribani mwaka mmoja.
Septemba 2015, viongozi 193 kutoka nchi mbalimbali duniani walikubaliana kuhusu malengo endelevu 17 kuelekea mwaka 2030.
Malengo
hayo ambayo yanatakiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 14 ijayo
yanaleta kwa pamoja shughuli za kijamii, kiuchumi na kimazingira ili
kuwa na maendeleo endelevu.
Mashirika
ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yakifanya kazi chini ya mwavuli
mmoja yanasaidia serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba
inafanikiwa katika kuyaingiza malengo yote 17 katika mpango wake wa
maendeleo wa mwaka 2025 kupitia mpango wake wa kuisaidia Tanzania (UNDAP
ll) ulioanza mwaka huu hadi mwaka 2021
Ili
kuweza kufikisha malengo hayo kila mahali , Umoja wa Mataifa kwa
kushirikiana na Chuo kikuu iringa wametoa elimu kwa wanafunzi wa chuo ili wawe wakufunzi kwa
wenzao.
Mafunzo
hayo yamelenga kuwafanya vijana kuelewa na kuongeza ufahamu kuhusiana
na malengo hayo ya dunia, hivyo kuwasaidia wenzao na wananchi wengine
kutambua wajibu wao katika utekelezaji wake.
|
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro
Rodriguez. katika Semina ya Uelewa wa Malengo Endelevu (picha; Damas A) |
|
Baadhi ya washiriki chuo kikuu cha Iringa katika Semina ya Uelewa wa Malengo Endelevu wa uliohudhuria mafunzo ya siku
moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yaliyoandaliwa na Ofisi ya
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na kufanyika katika
ukumbi wa chuo kikuu Iringa mkoani.(picha; Damas A) |
|
Pichani mwenye Komputa mpakato ni Ofisa
wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Didi Nafisa mwenye suti ya Blue ni Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu
Pamoja na David Mtegile wakisikiliza kwa umakini
Malengo ya Dunia (Global Goals) katika mafunzo ya
Malengo ya Dunia (Global Goals) yaliyofanyika mkoani Iringa.
( picha; Damas A.) |
|
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. akimkaribisha Mgeni rasmi wa Semina ya Uelewa wa Malengo Endelevu Ndugu |
|
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Richard Kasesela katika Semina ya Uelewa wa Malengo Endelevu (picha; David Mtegile) |
Mafunzo
hayo mkoani Iringa ni mwendelezo wa mafunzo yaliyozinduliwa mkoani
Arusha na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro
Rodriguez.
Hadi
sasa Umoja wa Mataifa umewezesha vijana wengi kutambua malengo hayo na
kutumika kufunza wengine.
|
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akiwasalimia wanafunzi wa chuo cha Karibu ujifunze |
Aidha Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela, wahadhiri na wanafunzi walipewa mafunzo
hayo kuhusiana na malengo hayo ya maendeleo
endelevu.
|
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Richard Kasesela katika Semina ya Uelewa wa Malengo Endelevu | | | | | | | | | | | |
|
Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi, Hoyce Temu
|
|
Sabinus Paul SDG Champoion alisema ''Niliamini, naamini na nitaendelea kuamini kwamba maisha bila unyanyasaji wa kijinsia yanawezekana''.
akihojiwa na vyombo vya habari katika Semina ya Uelewa wa Malengo Endelevu mkoani Iringa |
|
Damas Anthony Mwandishi wa Apostle Blogspot. Ni
muhimu sana kwa vijana kuelewa Malengo ya Dunia. Huu ni wakati wao. Kwa
kuyaelewa malengo haya inarahisisha utekelezaji wake. Nimefurahi kuona
muamko wa vijana waliojitekeza hapa leo na natumaini watawafikishia
wengine ujumbe huu.” ( picha; David Mtegile) |
Toa Maoni Hapa Chini