Na Apostle Darmacy
Angalia baadhi ya picha kutoka kanisa la E.A.G.T Temeke jijini Dar es
salaam ambako ndiko ulipo msiba wa aliyekuwa askofu mkuu wa kanisa hilo
la Evangelistic Assemblies of God, marehemu Dkt. Moses Kulola
aliyefariki dunia jana asubuhi jijini Dar es salaam.
|
Mchungaji Florian Katunzi wa City Centre ambaye anahusika na taratibu za msiba, akizungumza na wenzake msibani hapo. |
|
Watu wakibadilishana mawazo. |
|
Kina mama nao wapo msibani hapo kumsindikiza askofu Kulola. |
|
Waombolezaji wakipata chakula msibani hapo. |
|
Askofu Bruno Mwakibolwa mwenye shati ya kitenge akiwa na mwenzake katika kikao. |
|
Kikao cha baadhi ya watumishi wa E.A.G.T jimbo la Temeke. |
|
Mwimbaji wa
nyimbo za injili nchini Flora Mbasha ambaye pia ni mjukuu wa marehemu
Kulola akirejea msibani hapo usiku akitokea hospitalini ambako alikuwa
amepelekwa baada ya kuzimia msibani hapo. |
|
Emanuel Mbasha kushoto akizungumza na wafiwa wengine msibani hapo. |
|
Mjane wa askofu Kulola akimuuliza mjukuu wake Flora anaendeleaje baada ya mwimbaji huyo kuingia ndani. |
Toa Maoni Hapa Chini