Na Apostle Darmacy
IDADI ya wajawazito nchini wanaojifungua mapacha walioungana au wenye
ulemavu inazidi kupanda ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita, Pili Hija
(24), mkazi wa Jang’ombe, Zanzibar alijifungua watoto walioungana,
kinachosikitisha zaidi mmoja alikuwa ni kiwiliwili.
Pili alijifungua mapacha hao saa 1:00 asubuhi ya Agosti 18, 2013,
nyumbani kwake na baadaye kupelekwa kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja,
Zanzibar baada ya watoto kuonekana si wa kawaida.
Kufuatia
matukio kama hayo, Ijumaa Wikienda lilichimba kwa undani ili kubaini
nini husababisha wanawake kubeba ujauzito wenye matokeo ya mapacha…
Na Mwandishi Wetu
IDADI ya wajawazito nchini wanaojifungua mapacha walioungana au wenye
ulemavu inazidi kupanda ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita, Pili Hija
(24), mkazi wa Jang’ombe, Zanzibar alijifungua watoto walioungana,
kinachosikitisha zaidi mmoja alikuwa ni kiwiliwili.
Pili
alijifungua mapacha hao saa 1:00 asubuhi ya Agosti 18, 2013, nyumbani
kwake na baadaye kupelekwa kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar
baada ya watoto kuonekana si wa kawaida.
Kufuatia matukio kama hayo,
Ijumaa Wikienda lilichimba kwa undani ili kubaini nini husababisha
wanawake kubeba ujauzito wenye matokeo ya mapacha walioungana au mtoto
mmoja kulemaa kiungo chochote cha mwili.
Mtaalam mmoja aliyesomea
mambo ya afya ya uzazi ambaye aliomba hifadhi ya jina, ndiye aliyefunua
siri hii nzito ambayo wanawake wengi nchini hawaijui isipokuwa kwa
kusoma habari hii leo.
Mtaalam huyo alivitaja vidonge maarufu kwa
matibabu ya tumbo la kuendesha viitwavyo Flagyl au Metronidazole kuwa
ndivyo vinavyosababisha matatizo hayo.
Alisema vidonge hivyo ni
hatari mno kwa afya ya mama mjamzito, hasa kwa mtoto aliye tumboni
ambaye anatarajwa kukua na kutoka akiwa amekamilika.
“Wanawake wajawazito, hasa wakiwa wa miezi mitatu ya mwazo, hawatakiwi kabisa kutumia vidonge hivi aina ya Flagyl.
“Hivi vidonge ndivyo husababisha tatizo hili la watoto mapacha kuzaliwa wameungana, kitaalam tunaita Siamese Twins.
“Unajua kwa kawaida mimba huanza kuwa binadamu kamili miezi mitatu tu
ya mwanzo, kitaalam tunaita First Trimester ambapo kila kitu
kinachopaswa kuwa kiungo cha mwilini hufanyika.
“Baada ya hapo mpaka mwezi wa tisa ni kukua kwa viungo hivyo.
“Katika kipindi hiki cha miezi mitatu ya mwanzo kuelekea miezi mingine
hadi tisa, mwanamke akitumia Flagyl kwa sababu viungo vinakuwa, ni
rahisi kwa watoto kuungana au kuzaliwa wakiwa na ulemavu wowote,”
alisema mtaalam huyo.
Mtaalam huyo alisema vidonge hivyo ambavyo
hupatikana kirahisi kwenye maduka ya madawa (famasi) hutumiwa zaidi kwa
matatizo ya tumbo, hasa la kuendesha.
“Kwa nchi za wenzetu
(zilizoendelea), ili mtu auziwe vidonge ambavyo vinaweza kuleta madhara
lazima awe na karatasi ya maelekezo ya matumizi kutoka kwa daktari.
“Hakuna daktari wa kweli hata mmoja atakayekubali kumpa Flagyl mwanamke mjamzito, kwa sababu anajua madhara yake,” alisema.
Kuhusu Pili Hija, mapacha wake walifanyiwa upasuaji Agosti 29, 2013
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Kitengo cha Tiba ya Mifupa (Moi)
chini ya daktari wa upasuaji wa watoto, Dk. Zaituni Bokhary.
Mtoto
aliyebaki ni yule aliyezaliwa akiwa na kichwa, ilibidi kumuondoa asiye
na kichwa kwa sababu asingeweza kuwa binadamu kamili.
Dokta Bokhary
alisema hii ni mara ya kwanza kwa jambo hilo kutokea katika miaka ya
hivi karibuni. Mara ya mwisho lilitokea mwaka 1984
Toa Maoni Hapa Chini