Licha ya kuongoza mazishi hayo, Rais Kikwete pia
alitoa ushuhuda kwamba licha ya kuwa muumini wa dini ya Kiislamu, Askofu
Kulola wakati wa uhai wake mara kadhaa alikwenda Ikulu kumfanyia
maombi.
Rais Kikwete katika salamu zake za rambirambi,
alisema amekwenda kushiriki msiba huo kuungana na waombolezaji kutokana
na kumfahamu Askofu Kulola ambaye alikuwa mtu wa watu.
“Tuzidi kuwaombea kwa Mungu, familia katika
kipindi hiki kigumu, kwa jinsi nilivyomfahamu marehemu alikuwa mpenda
watu, hakujali kabila wala hali zao, alijali utu na heshima hii ndiyo
sababu na mimi alikuwa rafiki yangu,” alieleza Rais Kikwete.
Alibainisha kwamba licha ya kuwa Muislamu mara
kadhaa Askofu huyo alifika kumwombea Ikulu na katika maombezi yake
alisisitiza kuwa alikuwa akiwaombea Watanzania na nchi nzima kwa ujumla,
hivyo aliwahimiza walio hai kumuenzi Askofu kwa vitendo.
hali ya simanzi na majonzi ilitawala
katika mazishi hayo ambapo pia Rais Kikwete alimuelezea Dr.Moses Kulola
kama mtu aliyefahamiana nae mda mrefu na mtu ambaye aliwahi pia kwenda
ikulu na kumuombea na pia kuiombea nchi ya Tanzania idumu katika Amani
na mshikamano
aidha Rais Kikwete alimuelezea Dr.Moses
Kulola kama mtu ambaye alikua mkweli mpenda watu watu na mtu ambaye
hakua na ubaguzi wa kabila,dini rangi wala dhehebu na ndio maana hata
leo hii watu wa madhehebu yote wamehudhuria hata katika mazishi yake.
"Mimi sio msukuma wala mimi sio
mkristu lakini kikubwa kilichonifanya nifike katika mazishi ya ndugu
yetu na mpendwa wetu huyu askofu mkuu Dr.Moses Kulola ni vile maisha
yake aliyoishi hapa duniani ambayo ni mahubiri tosha
aliisimamia kweli bila kuogopa wala
kutetereka ,,,,,penye baya alisema hili ni baya na penye zuri alisema
hili ni zuri....kama asingekua mtu wa namna hiyo wala asingekua rafiki
yangu...
kuna kipindi alishakuja yeye pamoja
na mama mpaka kwangu ikulu akanambia nimekuja nataka nikuombee wewe
binafsi na pia niiombee nchi ya Tanzania kupitia wewe Raisi wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania ufanikiwe na upate kuongoza vema usiogope Mungu
yupo pamoja nawe.
kwa namna mtu huyu maisha yake
alivyoishi binafsi nimehuzunishwa sana baada ya kusikia kifo chake kwani
taifa limepoteza mtu wa muhimu sana mtu aliyekua kila kukicha akiiombea
tanzania iwe na amani na mshkamano na ndio maana leo hii wote tupo hapa
bila kujali vyama vyetu wanasiasa dini zetu wala kabila zetu....kikubwa
tumuenzi kwa kutenda yale aliyotufundisha.
alisema Rais Jakaya Kikwete
Kwa upande wake, Makamu Askofu Mkuu wa EAGT
Asumwisye Mwaisabila, akizungumzia msiba huo kuwa marehemu Kulola
alikuwa mchungaji wa aina yake na hivyo kuwataka wanaotaka kufanana naye
kuomba kwa Mungu awajalie hekima.
“Alikuwa askofu wa ajabu sana, hata kama ungeweza
kumtandikia mkeka ili alale, angelala. Jambo hili ni tofauti sana na
maaskofu wa kileo ambao ukiwatendea hivyo watanung’unika na kukusema
kila siku,” alieleza na kusisitiza wanapaswa kumuenzi kwa vitendo.
Katika Ibada ya maziko ya Askofu Kulola
iliyoongozwa na Makamu Askofu Mkuu, Asumwisye Mwaisabila, mbali na Rais
Kikwete pia Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Dk Willibroad Slaa, aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo, Wabunge William Ngeleja (Sengerema),
Ezekiel Wenje (Nyamagana), Highness Kiwia (Ilemela) pamoja na Mchungaji
Peter Msigwa, ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini.
Florah Mbasha na wajukuu wenzake wakiimba kwa huzuni.
| Mchungaji Abiudi Misholi akiimba wimbo aliotunga takriban nusu saa mara baada ya kupata taarifa za msiba wa Askofu Kulola. |
| Nyota imezimika, anaimba mchungaji Abiudi Misholi |
Wakati huohuo Rais Kikwete jana alisafiri kwenda Kampala, Uganda, kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.