Na Apostle Darmacy
MASOMO YA UFALME WA MUNGUHATUA YA KWANZA
KUUINGIA UFALME WA MUNGU
Leo hii tungemwuliza Mungu ni jambo gani lililo muhimu sana
katika moyo wake analohusika na kufuatilia kwa karibu zaidi hapa duniani
angesemaje?
Tunaweza kuwa na majibu mengine lakini naamini UFALME WA MUNGU ndio
agenda ya kwanza kabisa katika moyo wa Mungu.
Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya
akihubiri Habari Njema ya Mungu. akisema Wakati umetimia, na UFALME WA
MUNGU umekaribia tubuni na kuiamini Injili.
Marko 1 :14
Hayo ndiyo mahubiri ya kwanza Bwana Yesu aliyofanya;
akatambulisha kuwa huduma yake duniani inatambulisha ujio wa UFALME wa
Mungu duniani. Kwa Nikodemu akasema ili kuuona UFALME wa Mungu lazima
kuzaliwa mara ya pili.
“ mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.” Yohana 3:5
Hapa tena Bwana Yesu anasema kuna KUUONA lakini kusudi la Mungu ni
KUINGIA. Sharti la kuingia ni KUZALIWA KWA MAJI na KWA ROHO.
Hapa tena si maji ya mtoni, tunajua biblia inajifafanua yenyewe na kamwe
haijipingi. Kuhusu kuzaliwa mara ya pili sehemu zingine anasema hivi:-
“Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo bali
kwa ile isiyoharibika: kwa neno la Mungu lenye uzima lidumulo hata
milele.” 1 Petro 1:23
Je kuna uhusiano gani kati ya Neno na Maji? Linganisha na
Efeso 5:25
“ Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda
kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase kwa maji katika
neno…" Hivyo katika kuzaliwa mara ya pili Neno la Mungu huleta
uzima wa milele ndani ya roho ya mtu anayeliamini na hapo roho ya mtu
uhuishwa na kuzaliwa upya kwa uwezo wa Roho Mtakatifu!
“lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu na upendo wake kwa
wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki
tuliyotenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa
pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu". Tito 3:4-5
Watu wanaposikia Habari Njema ikihubiriwa wakaiamini ile Injili nguvu
ya Mungu katika neno lake huuleta ufalme wa Mungu katika moyo wa mtu.
Na hapo UFALME wa Mungu hupanuka kwa kuwa na kituo hapa duniani ambako
matakwa ya mfalme yanatekelezwa. Ndani ya moyo wa mwamini.
‘ …ufalme wa, Mungu hauji kwa kuuchunguza; wala hawatasema, Tazama,
upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, UFALME wa Mungu umo ndani yenu".
Luka 17:20-21.
Hii ni serikali ya Mungu, mamlaka na nguvu ya Mungu katika moyo wa
mwanadamu. Hapo Mungu anatekeleza malengo yake kupitia mtu aliyekubali
kumtii apitishe mawazo yake kwake; nguvu za Mungu zinatimiza matakwa ya
Mungu kupitia duniani. Duniani anayeonekana ni mwanadamu lakini
kinachofanyika ni cha Mungu. Mtu anakuwa ni station ya siri inayofanya
mambo ya UFALME wa Mungu ndani ya falme za dunia hii. Ukipenda kuwa
sehemu ya mpango huu wa ajabu lazima kutubu na kuiamini Injili.
Ikiwa hii ni shauku ya moyo wako basi Sali sala hii ukimaanisha toka moyoni mwako.
Mpendwa Bwana Yesu nakushukuru kuwa umeleta ufalme wa Mungu
hapa duniani. Nakubali kuwa nimeishi nje ya matakwa ya Mungu na hivyo
kumhuzunisha Mungu. Naomba unisamehe dhambi zangu zote. Naufungua moyo
wangu nikikuribisha ndani ya maisha yangu. Kuanzia leo naomba unitawale.
Nitakutii na kukufata siku zote zilizobaki za maisha yangu. Ahsante kwa
kuniokoa katika jina la Yesu ninaomba Amen.
Toa Maoni Hapa Chini