Kumekuwa
na theology nyingi sana kuhusu kuanzisha mahusiano, ambazo nyingi ni
za uzoefu wa watu binafsi hasa wasio na MUNGU, au wale wanaofuata DINI
tu.
Nitajaribu kuzungumzia kwa kirefu zaidi kuanzisha mahusiano kwa
vijana waliookoka kutakuwa na contents zifuatazo
- Mahusiano kwa vijana wasiookoka na athari zake
- Mahusiano kwa vijana waliookoka
- Maandalizi kabla ya uchumba au ndoa kwa vijana wa kike na wakiume,
- Hatua za mwanzo kabla ya uchumba
- Kupata mchumba toka kwa BWANA
- Dhana ya upendo
- Utaratibu wa kanisa katika hatua za uchumba, n.k
Lakini Kwa ufupi nielezee kuhusu mahusiano yasiyo na MUNGU.
1. *MAHUSIANO KWA VIJANA WASIOOKOKA NA ATHARI ZAKE:*
Vijana
wengi ambao hawajaokoka huwa hawana hofu ya Mungu ndani yao,
hivyo wanakuwa na maamuzi yoyote kuhusu kufanya dhambi, ikiwa ni pamoja
na kufanya ngono pasipokupata hukumu ndani ya dhamiri zao, Sababu yake
kubwa BIBILIA inasema kwamba dhamiri zao zimekufa kwani wamesha kuwa
wafu japo watembea. Matakwa Yao wenyewe yasiyo na kujali kuwa hili ni
kosa mbele za Mungu au si kosa ndio wanayafanya.
*KUFUATA MATAKWA YAO NA ATHARI ZAKE:***
*Uharibifu na magonjwa:*
Kuna uharibifu mkubwa ambao hujitokeza katika mahusiano ambayo hufuatwa na vijana wasio na hofu ya Mungu.
- Kupata mimba katika umri mdogo na kukatishwa masomo (wasichana)
- Kupata magonjwa ambayo hutokana na zinaa, kama vile (Ukimwi),


*Kukosa mwelekeo sahihi:*
-
Pindi vijana wanapokatishwa masomo, hukosa mwelekeo sahihi wa
maisha yao. Na hata baadaye wanapokuwa hawana elimu, huishia kujiingiza
katika makundi mabaya.
- Kujiingiza katika (ukahaba) kwa kujiuza miili yao na hata kupata mahitaji yao (wasichana).
- Kujeruhiana baada ya kuchokana kimapenzi kwa kuachana bila taratibuKupata watoto wa mitaani
- Kuanzisha mahusiano mengine na msichana au mvulana mwingine hatakama hawajatarakiana. Na mengine mengi sana
-
Kujiingiza katika makundi mabaya ya uvutaji bangi na utumiaji wa
madawa ya kulevya na vitendo vya ujambazi na matokeo yake ni kifo.
1. *MAHUSIANO KWA VIJANA WALIOOKOKA*
*(Mungu ndiye Mhusika mkuu)*
Vijana
wengi waliookoka, huishi maisha matakatifu ambayo humpendeza Mungu.
Na pia hujiepusha kujiingiza katika vitendo vya kumchukiza Mungu Kama
walivyo watu wa mataifa. Hasa pindi ambacho tamaa katika miili yao
hazijaanza kuamshwa. Japo kuwa wengine wameokoka wakiwa katika umri
mkubwa na waliishi isipositahili lakini wakiokoka YESU huingia ndani yao
na kuzichukua zile kiu za dhambi zao.
*
[Waefeso 4:22-24, inasema, Mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu
wa zamani,unaoharibika kwa kuzifuata tama zenye kudanganya.(23)
Na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu. (24) Mkavae utu
mpya,ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.
* *Kuna mambo mengi ambayo kama vijana tuliookoka tunatakiwa kujiepusha
nayo, ili tusije tukaingia katika majaribu na kuangukia dhambini kingono.
i. *Simu za Mikononi*:
Simu
za mikononi, ni jambo moja wapo ambalo linaweza kuchangia mabinti
tukawa na uhusiano wa karibu sana na kijana wa kiume na matokeo yake
kuvuka mipaka na kumsahau Mungu, mfano, tunaweza kujikuta
tunatumiana message za kutaniana na baadaye ule utani ukaanza kuleta
hisia tofauti baina yetu na baadaye tukaunda kitu, na tukaamua kufanya
kweli.
* ii. **Matumizi ya mitandao ya internet.*
Hili
ni janga kuu na ni kubwa sana, maana vijana wengi
wamekuwa wakidanganyika kwa kuangalia picha ngono kwenye mitandao na
video za ngono kwenye simu na casseti. Hivyo hili linatupasa kujiepusha
Sana, ili lisitujengee akili dumavu(ukiangalia picha chafu hizo
utaishia kwenye kujichua, na kujichua kunaharibu akili kwa asilimia
90%, EPUKA). pia Matumizi mabaya ya Facebook, na technology nyingine
zinazokuwa kwa kasi kubwa kabisa kwa sasa.
iii. *Kwenda kuhudumu vijana wa jinsia tofauti mkiwa wawili: *
*
*Tunaweza tukawa na ukaribu sana kama kaka na dada, na baadaye
tukaanza kwenda kuhudumu/kushuhudia pamoja ,na itafikia hatua tutazoeana
na hata kutaka kuwa na muda wa kukaa pamoja na kujifunza neno na hata
kuomba pamoja, labda nyumbani kwa kijana wa kike au kijana wa kiume. Na
matokeo yake tukaanza kuwa na hisia tofauti na kuona kuwa tunapendana
na kuwa (tumeona maono) tutakuja kuoana, au binti akawa na hisia
tofauti na kuhisi kuwa kijana wa kiume anampenda wakati sivyo. Na
baadaye ikionekana kuwa yule kijana anachumbia mtu mwingine, yule binti
ataumia sana na matokeo yake kuamua kuacha wokovu.
 |
Mchungaji Daudi akiwa na Apostle Darmacy |
Na pia tunapoenda
kushuhudia inatakiwa kuwa watu watatu au zaidi ,akiwepo mmoja wa jinsia
tofauti na wawili wa jinsi moja ni nzuri zaidi.Au wote tukawa jinsia
moja.Hiyo inaleta ushuhuda mzuri kwa wale tutakao kuwa tunawashuhudia
neno la Mungu, hawatakuwa na maswali mengi kuhusiana na sisi.Pia
kukutana kwenye hotels/ hostel au mahali pa kificho kwa ajili ya
kujadili huduma au appointment huku ukijua mtakuwa wawili, au kusafiri
kikazi na mwanamke/mwanamme asiyeokoka au ameokoka na mkapanga HOTELI
MOJA, hapo ni hatari sana. Ni heri kwenda kama kikundi.
* iv. **Binti kujiachia kwa mvulana kupita kawaida:
*
*Binti aliyeokoka anatakiwa kutumia akili katika uhusiano wake na
vijana wa kiume. Sawa kuwa na kaka mpendwa siyo mbaya ila inatakiwa
ukaribu wetu usivuke mipaka [Mfano,utaona binti anamzoea sana kijana
(kaka) na kufikia hatua kumtembelea kijana katika chumba chake
anachokaa.Na hata kuanza kumsaidia kazi za ndani kama vile kudeki,kupika
na hata kufua kwa kigezo cha (mpendwa).Huko ndiko binti kujiachia kwa
mvulana.Kwa sababu unapoenda kwake na yeye anaishi peke yake unategemea
nini? Na yeye ni mwanadamu kama wanadamu wengine anahisia kama wanaume
wengine japo kuwa ameokoka, kufanya kwako hivyo hata kama ulikuwa
hauna nia mbaya kutomuingiza majaribuni kijana huyo. Na matokeo yake
yatakuwa mabaya na machukizo mbele za Mungu
(kuanguka
dhambini kingono, tena mtaanza na kukumbatiana, then kubusiana
baadae ulimini). Vyote hivyo havistahili kutajwa kwa watakatifu wa
Bwana.
* v. **Uhuru wa kuchangamana na kutoka pamoja kaka na dada mkiwa wawili (outing):*
Tukiwa vijana tuliookoka,tunatakiwa kuangalia mambo ambayo yanaweza
kutuangusha katika dhambi. Kitendo cha kutoka outing si kibaya
(kama wapendwa) ila inatakawa kuwa zaidi ya watatu.Utaona kaka na dada
wanatoka na kwenda, labda beach
na si ajabu anaenda kwa nia nzuri tu ya
kubadilishana mawazo na hata kupunga upepo ila
* ,shetani ni mjanja sana,
pindi wakiwa ufukweni wanaweza kuwaona watu wakiwa na (wapenzi) wao.
Labda wanashikana shikana na hata kula mate (romance). Na wao wakiwa
kama wanadamu wenye hisia kama wanadamu wengine lazima ile hali
wataiweka katika vichwa vyao. Na hata wakiwa wanaenda mara kwa mara na
kuendelea kuiona ile hali,itafikia hatua watashawishika na kufanya hivyo
kama wengine wafanyavyo, na matokeo yake ni kuangukia dhambini.
* vi. **Mahusiano ya kadi za Valentine kwa kaka na dada ni kinyume na mapenzi ya Mungu: *
* *Ni vijana wengi tuliookoka pindi ifikapo siku ya Valentine,tunajishughulisha kwa kununua kadi na maua na kupeana, kama kaka
na dada. Na bila kujua nini maana ya siku ya Valentine na ilitokana
na nini.Inatakiwa kabla ya kufanya kitu tuangalie kwanza mwanzo wake ni
nini? (Mf. Tunasherehekea Chrismas kwa sababu tunajua mwanzo wake ni
nini, tunapeana kadi na hata zawadi pia ikibidi) lakini sherehe ya
valentine inahusiana na Uzinzi, kama tukifuatilia mwanzo wake tutajua
hilo.Vijana tuliookoka tunatakiwa kufanya mambo ambayo ni mapenzi ya
Mungu si kuiga tu mambo ya dunia hii.Na matokeo yake kutumiana kadi na
maua (kaka na dada), inakuja kuunda kitu tofauti kabisa katika akili
zetu na mwisho wake ni kuangukia dhambini.
* vii. **Kujiepusha kuingia maeneo yasiyo husika:*
*
* Sisi kama vijana tuliookoka inatakiwa tuangalie sehemu
ambazo tunaingia, mf ,Utakuta kijana aliyeokoka anaingia Night clubs,
Casino .n.k. Na sehemu kama hizo mara nyingi uasi mkubwa hutendeka na
matokeo yake shetani anaweza kukushawishi na ukaangukia dhambini na
kufwatisha uasi huo.Kwa hiyo sisi kama vijana tuliookoka tunatakiwa
tuangalie sehemu za kuingia siyo kila sehemu ,sisi tunaingia.Na mwisho
wake tunaweza kumtenda Mungu dhambi.
* viii. **Kuzoea kuingia kwenye vyumba vya Wasichana au Wavulana:*
*
*Mazoea ya binti kuingia kwenye vyumba vya wavulana na kukaa kwenye
kitanda cha mdada, si jambo jema na hata mvulana kuingia kwenye chumba
cha binti si jambo jema na si heshima.Inatakiwa tuheshimiane sisi
kwa sisi .Na si kwamba siyo heshima tu, bali tunaweza kujikuta
tunaangukia dhambini kutokana na mazoea kama hayo.
* ix. **Kuwa na Boyfriend na Girlfriend, mara nyingi inapelekea vijana wengi dhambini:*
*
*Kwa habari ya kuwa na Girlfriend au Boyfriend, ni kweli wakati bado
hatujampokea Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yetu,wengi wetu
tulikuwa nao.Lakini inashangaza na kusikitisha na hata leo
katika Kanisa la Kristo vijana tuna kuwa na tabia kama ya mwanzo ambayo
tuliishazizika. Na matokeo makubwa ya kuwa na uhusiano huo, mwisho
wake ni kuangukia dhambini. Kwa hiyo sisi kama vijana tumtumikie
Mungu,wakati ukifika Bwana atafanya njia na atatupa waume na wake
kutoka kwake. Na watakuwa baraka
katika maisha yetu.
Katika mahusiano yetu sisi kama vijana tuliookoka inatupasa kutunza ushuhuda wa Bwana wetu Yesu Kristo.
 |
Mwandishi wa apostledarmacy.blogspot.com
|
Endelea kufuatilia http://apostledarmacy.blogspot.com/ kwa habari zaidi
Pia waweza ku share na watu wangine link hii
Bless u
Toa Maoni Hapa Chini