Ni moja ya Mafundisho Ya Mwl. Christopher Mwakasege
SABABU NYINGI AMBAZO MUNGU HAJIBU MAOMBI
ZIPO NYINGI LAKINI NAKUONYESHA AMBAZO NI ADIMU
|
Mwl. Christopher
Mwakasege |
1.
KUTAKA KUJIBIWA
MAOMBI YAKO NJE YA NJOZI AU NJE YA MAONO YA MUNGU
Habakuki 2: 1 – 3 … Bwana akanijibu, akasema iandike
njozi hii ukaifanye kuwa wazi sana katika …
- Wakati Habakuki anaomba ondoa uovu/ udhalimu/
haki imepotoka, Mungu amenyamaza, halafu anaenda kuomba kwa nini Mungu
hakujibu malalamiko yake ndipo Mungu akajibu!
- Mungu hakujibu kutatua malalamiko yake ila Mungu
alijibu malalamiko yake (Vs. 2 - 3)
Lile neno njozi kwa kiingereza limeandikwa vision na
kwa Kiswahili lingefaa kuwa maono.
- Mungu alikuwa anamwambia Habakuki badilisha aina
ya uombaji wako,usiombe kwa kuangalia mazingira yanavyoonekana ila omba
kwa kuangalia njozi
NJOZI za aina 3:
a). Njozi yake mwenyewe
b). Njozi ya eneo ambalo analiombea
c). Njozi ya maeneo ambayo habakuki alikuwa ana mazoea
ya kukaa au kupita
Habakuki alikuwa anaelewa Mungu alikuwa na maana gani
maana hakuna alipomwambia aina gani ya njozi aliandike!
Ndani ya hiyo mistari miwili yapo mambo 7 ambayo
sitayataja hapa ila nitayataja kesho, leo acha nieleze kidogo juu ya
njozi/maono / vision. Maana kila mtu hapa atatoa tafsiri yake
MAANA YA NJOZI/ MAONO/ VISION
NJOZI/ MAONO/ VISION NI KUSUDI LA MUNGU LINALOFUNULIWA
NDANI YA MTU KWA NJIA YA MFUMO WA PICHA, ni kusudi la Mungu linalowekwa ndani
yako linapofunuliwa linakuwa maono/ vision.
Na linapofunuliwa linakupa kuona angalau vitu 3 au
kimoja wapo au vyote vitatu kwa pamoja:
1. Kukupa sababu ya kuumbwa kwa kitu/ kuwepo kwa
kitu,
Sababu ya kuwepo kampuni/ nchi / ndoa, cho chote kile na unapopewa
sababu na ikifunuliwa ndani yako ile sababu inakuwa vision.
Bangi ni mbaya kwa sababu hatujui makusudi ya Mungu
kuiumba. Hivyo serikali imepewa na Mungu kuweka sheria ya kuhakikisha kuwa
bangi haitumiki vibaya mpaka pale tutakapojua matumizi mazuri ya bangi.
Ajali nyingi za mabasi ni kwa sababu ya utengenezaji
wa mabasi, mabasi yana chases yake na magari ya kubeba mizigo yana chases.
Unakuta mtu ananunua kichwa cha lorry na anachonga basi, ukilitazama kwa nje
unaona linapendeza na linapokimbizwa na kukata kona gari linamshinda dereva kwa
sababu halikuundiwa kukata kona likiwa na watu lakini likiwa na mizigo halafu
tunasema ni shetani.
2. Kukupa picha ya mwishoni wa jambo ukiwa mwanzoni,
maono yanakupa mwisho wa jambo ukiwa mwanzoni mwake. Na unapoona mwisho wake
unapata ndani yako msukumo, na mtu asiyeona mwisho wa jambo anaweza kukatishwa
tamaa maana hajaona mwisho wake lakini yule aliyeona mwisho wake hauwezi
kumkatisha tamaa hata iweje!
Kabla nyumba haijawa nyuma inakuwa nyumba ndani ya
mtu. Mchoraji anaweza kuweka kwenye computer na anaonyesha kilichondani yake na
hata ukimwambia kuwa hii nyumba haiwezi kujingwa hawezi kukuelewa kwa sababu
hameiona
3. Kusudi la Mungu linakupa ‘motive’ (kujua)
Wakati wa kesi za mauaji mahakamani wanachunguza
sababu za kuua, i.e wakati hukumu inatolewa wanaangalia sababu ya kuuna na
inapokuja kuwa aliua pasipo kukusudia adhabu yake ni tofauti. Kusudi la Mungu
kukupa maoni ni kukupa kujua sababu ya kuwepo
WATU WENGI SANA WANACHANGANYA KATI YA WITO NA MAONO
Waefeso 4: 11 – 16 … mitume/ manabii/ waalimu/
wachungaji … KWA KUSUDI LAKE
Unamuuliza mtu wito wake anaeleza maono yake!
- Kuitwa kuwa nabii, mtume, mwalimu hilo sio KUSUDI
ni WITO
- 2Timotheo 1: 8 – 9 … akatuita kwa mwito mtakatifu
… KWA KADRI YA MAKUSUDI YAKE YEYE.
- USIPOJUA KUSUDI LAKE HUTAJUA MAONO YAKO
- Mungu aliponiita kuwa mwalimu anakusudi la
kuniita kuwa mwalimu.
- Unapoombea uinjilisti/ uchungani unaombea wito
lakini hujaombea MAONO/ KUSUDI LA MUNGU
- Mungu hawezi kukupa nje ya maono/ kusudi la
kukuitia, ukiwa unaomba mkumbushe Mungu ndani ya maono/kusudi alilokuitia
na mengine yote atakutimizia. Fedha hazijawa connected na maono! Mungu
anakupa pesa kama una maono ya ile pesa/ huduma.
- Mungu hawezi kumlipa mtu kwa kazi ya hasara
- Wachungaji wanapata hali ngumu kifedha kwa sababu
wanadhani wito ni maono na wanataka Mungu awape pesa kwa ajili ya
wito wakati Mungu anataka atoe pesa kwa ajili ya MAONO
Matendo 13: 36 … akiisha kutumikia SHAURI/KUSUDI
LA BWANA…
Si kusudi la Israel/ kusudi la baba yake/ si kusudi la
serikali ila KUSUDI LA MUNGU i.e alijua kusudi la Mungu.
- Kampuni inaweza kuwepo na ukatumikia wito
ukasahau kutumikia kusudi la Mungu
Kutoka 25: 1 – 9 … wamjengee HEMA ambalo Mungu
atakaa ndani!
- Kazi ya hema sio kukaliwa na watu ila Mungu
- 2Samweli 7: 1 – 5 hekalu sio nyumba ya ibada ila NYUMBA YA MUNGU;
Kwa sababu Mungu yupo ndani ndio maana ibada inafanyika – kama Mungu
hayupo ndani ibada inafanyika ya nini?
- Ukiacha kufuata kusudi la Mungu usithubutu
kuulizia ulinzi wa kusudi la Mungu
- Mtu aliye ndani ya kusudi na aliye nje ya kusudi
wanapata vita vilivyosawa lakini ulinzi unatofautiana
|
Mwandishi wa blog Darmacy |
Toa Maoni Hapa Chini