UNAWEZA KUDHIBITI U.T.I MWENYEWE
U.T.I
ni ugonjwa sugu unaosumbua sana watu wengi hivi sasa, wakubwa kwa
wadogo. U.T.I (Urinary tract Infection) ni ugonjwa unaoathiri njia ya
mkojo na huweza kusababisha maumivu makali na unapojiimarisha mwilini
kwa muda mrefu huathiri figo pia. Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na mtu
kusikia haja ya kukojoa kila wakati na kusisimka wakati wa kujisaidia,
kusikia maumivu, kutoa mkojo mchafu na hata kutoa haja ndogo
iliyochanganyika na damu.
Wataalamu wetu wa masuala ya tiba
wanatueleza kuwa tatizo hili hujitokeza pale mlango wa njia ya haja
ndogo inaposhambuliwa na bakteria ambao husambaa na wasipotibiwa mapema
huenea hadi kwenye figo na athari zake ni mbaya.
UNAWEZA KUDHIBITI U.T.I KWA TIBA MBADALA
Kwa
kawaida kila ungonjwa una tiba mbadala, siyo lazima kwenda hospitali.
Unaweza kuudhibiti au kuponya ugonjwa huu kwa kunywa maji mengi pamoja
na juisi itokanayo na matunda halisi, iwapo utawahi kabla tatizo
halijawa sugu.
Kwa maana nyingine, unaweza kujikinga na ugonjwa
huu kwa kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Ukinywa maji
ya kutosha yatakufanya uende haja ndogo kila mara na kwa njia hiyo wale
bakteria watakuwa wakitoka na hatimaye kuisha kabisa. Aidha, njia
nyingine ya kuudhibitibi ugonjwa huu ni kunywa maji mengi husaidia
kuwaondoa mapema bakteria wote.
Katika hali ya kawaida, ugonjwa wa UTI hutoweka ndani ya
siku tatu mara baada ya kuanza kutumia tiba asili ya kunywa maji mengi
na juisi ya matunda halisi, iwapo ugonjwa utaendelea kuwepo baada ya
siku hizo, hiyo itakuwa na maana ugonjwa wako umeshakomaa na hivyo
hauwezi kutibika kwa tiba hii ya nyumbani.
Katika hali kama hii,
utakuwa huna njia nyingine isipokuwa kwenda hospitalini na kuonana na
daktari ambaye atakufanyia uchunguzi na kukupatia dozi sahihi ambayo
utatakiwa kuizingatia bila kukosa. Uamuzi huu ni muhimu hasa kama
unasikia maumivu makali ambayo yanaweza kuwa yanasababishwa na
kuathirika kwa figo. Kwa kawaida tiba ya kidaktari kwa ugonjwa huu
huhusisha matumizi ya dawa kali za ‘antibiotics’, ambazo watu wengi
wanazikimbia kutokana na athari zake za baadae (side effects). Lakini
ni muhimu kufuata ushauri wa dokta na kumaliza dozi ili kuepuka
uwezekano wa kurejea kwa ugonjwa, tena kwa kasi kubwa.
KUZUIA
Ili
kujiepusha na ugonjwa huu, suala la usafi na kuwa na tabia ya kunywa
maji ya kutosha ni jambo muhimu sana. Hakikisha unajisafisha vizuri mara
baada ya kwenda haja na kubadilisha mara kwa mara nguo yako ya ndani,
hasa kwa akina mama.
Vile vile usikae na haja ndogo kwa muda
mrefu, nenda kajisaidie mara nyingi kadri unavyosikia kufanya hivyo.
Kitu cha mwisho cha kuzingatia kwa mgonjwa wa UTI ni kupunguza unywaji
wa pombe na vinywaji vingine vyenye sukari, kwa sababu sukari ni chakula
cha bakteria hivyo kwa kuendelea kunywa kinywaji chenye sukari
kutaifanya hali kuendelea kuwa mbaya. Ugonjwa huu ni rahisi kuepuka kwa
mtu anayependa kunywa maji ya kutosha na kunywa juisi halisi kila siku
KUDHIBITI U.T.I
Katika
kuudhibiti ugonjwa huu, pendelea kula vyakula ama vinywaji vyenye
kiwango kikubwa cha vitamini C ambayo utakipata kwenye matunda ya aina
mbalimbali yakiwemo machungwa, mboga za majani n.k. Jiepushe na ulaji wa
vyakula vya ‘kupaki’ kama vile ‘chizi’, chokoleti na bidhaa nyingine
zilizotengenezwa kutokana na maziwa. Pia jiepushe na ulaji wa vyakula
vyenye viungo vingi kama pilau, epuka vyinywaji vyenye ‘caffeine’,
kilevi na sigara na mwisho achana na vinywaji kama soda na vinavyofanana
na soda.
Toa Maoni Hapa Chini