HUDUMA YA FISHERS OF MEN YAVUA MAMIA YA WANAFUNZI WA KIBAHA KWA YESU
Mavuno ya zaidi
ya wanafunzi 300 walimpa Yesu Kristo maisha.
 |
Mavuno tayari, wanafunzi wakimpa Yesu maisha yao. |
Huduma ya Fishers of Men ikiwashirikisha
waimbaji wa Glorious worship Team na mwimbaji wa muziki wa kufoka wa
injili Rungu la Yesu walivamia shule za sekondari wilayani Kibaha mkoa
wa Pwani kuwatangazia habari njema za Yesu na kurudi na mavuno ya zaidi
ya wanafunzi 300 walimpa Yesu Kristo maisha.
Huduma hiyo ilifanikisha tendo la kuwaleta wanafunzi pamoja kwa
kuwalipia nauli za kutoka mashuleni kwao hadi katika ukumbi wa elimu
Kibaha na pia waliandaa chakula cha mchana kwa wanafunzi wote ambapo
Mungu aliweza kujifunua kwa wanafunzi hao kumjua yeye na wengine wengi
kufunguliwa katika vifungo mbalimbali vya shetani. Baada ya huduma njema
wilayani Kibaha kwasasa huduma hiyo inajipanga kwenda mkoani Dodoma
kuwahubiria wanafunzi wa vyuo mkoani humo.
 |
Glorious Worship Team wakiongoza sofa na kuabudu. |
 |
Baadhi ya umati wa wanafunzi uliotoka mbele kumpa Yesu maisha yao. |
 |
Umati wa wanafunzi waliokubali mwito.
|
 |
Mwimbaji wa GWT akifanya huduma ya maombi kwa wanafunzi. |
 |
Hakika wanafunzi walifunguliwa. |
 |
Wanafunzi wakihudumiwa katika semina hiyo. |
 |
Mtumishi Sunbella Kyando mwenye fulana ya zambarau mmoja wa viongozi wa huduma hiyo akihudumia katika semina hiyo. | | |
 |
Apostle Darmacy |

Credit
Toa Maoni Hapa Chini