Kituo cha Kwa Neema Fm Radio ndani ya shangwe za maadhimisho ya Miaka minne tangu kuanzishwa kwake
Kituo cha Radio cha Kwa Neema FM Radio
cha jijini Mwanza jumapili hii kimefanya sherehe za maadhimisho ya miaka
minne tangu kituo hicho kilipoanzishwa na kuanza kwenda hewani
kikirusha matangazo yake katika mikoa ya Kanda ya ziwa matangazo ambayo
yamefanyika msaada kwa watu wengi kutokana na mafundisho ya Neno la
Mungu ambayo yamekua yakitolewa na kituo hicho.
|
Mwanamuziki Flora Mbasha akienda sawa na mashabiki |
Maadhimisho ya kituo hicho cha Radio
yamefanyika ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kupambwa na
uimbaji toka kwa wanamuziki wa nyimbo za injili nchini Tanzania ikiwa ni
pamoja na Flora Mbasha na Emannuel Mbasha,Bahati Bukuku ,na Upendo
Nkonne.
|
Emannuel Mbasha akiwaimbisha umati wa watu uwanjani hapo |
|
sehemu ya wadau wa Radio hiyo wakifatilia mambo uwanjani hapo CCM Kirumba |
|
timu ya Watangazaji wa Kwa Neema FM Radio |
|
Flora Mbasha,Bahati Bukuku wakiwa na wadau mbalimbali |
|
Bishop Nzwalla wa kanisa la Hossa Christian Center jijini Mwanza akilishwa keki taratiiiiiiibu |
|
watangazaji wa kituo hicho wakijitambulisha kwa watu mbalmbali waliokua wamehudhuria kwenye sherehe za maadhimisho hayo |
|
Bi Evelyne Buchanagandi kongozi mmojawapo wa kituo hicho akielezea jambo |
|
Pastor Zakayo Nzogere wa kanisa la Mwanza International Community Church nae akapata fursa ya kulishwa Keki | |
credit to ;http://maishaushindi.blogspot.com/2014/03/kituo-cha-kwa-neema-fm-radio-ndani-ya.html#more
Picha kwa niaba yaMjap inc
Toa Maoni Hapa Chini