Musa
alipoomba, Bahari ya Shamu iligawanyika.
Eliya alipoomba, moto ulishuka
kutoka mbinguni. Danieli alipoomba, malaika aliyafumba makanwa ya simba
wale wenye njaa kali. Biblia inatueleza visa vingi vya kusisimua vya
maombi yaliyojibiwa. Tena inapendekeza kwetu maombi kama njia ya kupata
ule uweza kwetu maombi kama njia ya kupata ule uweza mkuu wa Mungu.
Yesu anaahidi hivi:
"Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu,
nami nitalifanya" - (Yohana 14:14).
Lakini
maombi mengine bado yanaonekana kana kwamba hayasikilizwi. Kwa nini?
Hapa chini zipo kanuni saba zitakazokusaidia wewe kuomba kwa ufanisi
zaidi:
(1)
Uwe karibu sana na Kristo.
"NINYI MKIKAA NDANI YANGU, na maneno yangu
yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtapewa." - Yohana
15:7.
Tunapoupa
kipaumbele uhusiano wetu na Mungu na kuwa karibu naye, tutakuwa tunasikiliza
na kutazamia kupata majibu kwa maombi yetu ambayo, vinginevyo, tusingeyatambua.
(2)
Endelea Kumtumaini Mungu.
"MKIAMINI, mtapokea yote myaombayo katika
sala zenu" - (Mathayo 21:22).
 |
Pastor Thobias Tambikeni Na Mama Mchungaji |
Kuamini
au kuwa na imani, maana yake ni kwamba tunamtazamia Baba yetu aliye
mbinguni kwamba kweli atatupa hayo mahitaji yetu. Kama wewe una wasiwasi
kwamba huna imani, basi, kumbuka kwamba Mwokozi alitenda mwujiza kwa
mtu yule aliyemsihi sana akiwa amekata tamaa, aliyesema:"
"Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu!"
- (Marko 9:24).
Wewe
kazana tu kuitumia imani ULIYO nayo; usiwe na waiswasi juu ya imani
ile usiyo nayo.
(3)
Jisalimishe kimya kimya chini ya mapenzi ya Mungu.
"Huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya
kuwa, tukiomba kitu cho chote SAWA SAWA NA MAPENZI YAKE, anatusikia"
- (1 Yohana 5:14).
Kumbuka
kwamba Mungu anataka kutufundisha sisi, pamoja na kutupa sisi vitu,
kwa njia ya maombi. Kwa hiyo, wakati mwingine anatuelekeza upande mwingine.
Maombi ni njia ya kutusogeza sisi zaidi na zaidi karibu na mapenzi ya
Mungu. Hisia zetu zinatakiwa ziwe kali kutambua majibu ya Mungu na kujifunza
kitu kutokana nayo. Kuyafuatilia kwa karibu maombi yetu fulani fulani
ya pekee pamoja na kile kinachotokea kuhusiana nayo ni msaada mkubwa
kwetu.
Roho
Mtakatifu atakusaidia kulenga shabaha yenyewe: "Roho anawaombea
watakatifu kulingana na mapenzi ya Mungu" (Warumi 8:27. Kumbuka
kwamba mapenzi yetu yangeweza kulandana siku zote na mapenzi ya Mungu
endapo sisi tungeweza kuona kama yeye anavyoona.
(4)
Mngojee Mungu kwa Saburi.
"NALIMNGOJA BWANA KWA SABURI, akaniinamia
akakisikia kilio changu" - (Zaburi 40:1).
Jambo
kubwa hapo ni kukaza mawazo yako yote kwa Mungu, kukaza mawazo yako
yote juu ya suluhisho lake. Wala usithubutu kumwomba Mungu akusaidie
kwa dakika moja, na halafu kujaribu kuzizamisha shida zako kwa kujifurahisha
katika anasa dakika inayofuata. Umngoje Bwana kwa saburi; tunahitaji
kuwa na nidhamu hiyo vibaya sana.
(5)
Usiing'ang'anie Dhambi iwayo yote.
("Kama ningalinuia maovu moyoni, Mwenyezi-Mungu
hangalinisikiliza")- Zaburi 66:18.
Dhambi
ijulikanayo hukata mara moja uweza wa Mungu katika maisha yetu; inatutenga
mbali na Mungu (Isaya 59:1-2). Huwezi kuishika na kuing'ang'ania dhambi
kwa mkono mmoja na kunyosha mkono mwingine kupokea msaada wa Mungu.
Ungamo la dhambi litokalo moyoni hasa pamoja na toba ya kweli ndilo
suluhisho la tatizo hilo.
Kama
sisi hatutaki kumruhusu Mungu kutuweka huru mbali na mawazo, maneno
na matendo yetu mabaya, basi, maombi yetu hayawezi kutuletea jibu lo
lote.
"Hata
mwaomba, wala hampati, kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa
zenu" - (Yakobo 4:3).
Mungu
hatajibu "ndiyo" kwa maombi ya uchoyo. Acha wazi masikio yako
yapate kuisikia sheria ya Mungu [Amri Kumi], yaani, mapenzi yake, naye
ataacha masikio yake wazi kuzisikia dua zako.
"Yeye
aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria [Amri Kumi], hata sala yake ni
chukizo" - (Mithali 28:9).
(6) Tambua Kwamba Unamhitaji Mungu.
Mungu huwajibu wale wanaoomba kuwako kwake na uweza wake katika maisha
yao.
"Heri
wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa." - Mathayo
5:6.
(7)
Kuendelea Kuomba Tu.
Yesu alitoa kielelezo cha kuwapo kwa haja ya kuendelea tu kutoa dua
zetu kwa kusimulia kisa kile cha mjane aliyekuwa anaendelea tu kuomba
na kuendelea kuja kwa hakimu akiwa na ombi lake lile, lile. Mwishowe
yule hakimu alisema, huku akiwa ameudhika vibaya sana, "Kwa kuwa
mjane huyu ananiudhi, nitahakikisha kwamba nampatia haki yake."
Kisha Yesu alitoa hitimisho lake hili: "Je! Mungu hatawapatia haki
wateule wake wanaomlilia mchana na usiku? Je! atazidi kuahirisha kuwapatia
haki yao?" (Luka 18:5-7).
Zungumza
na Mungu juu ya mahitaji yako yote, matumaini yako yote, na ndoto zako
zote. Omba mibaraka ya pekee, omba msaada unapokuwa na shida. Endelea
kutafuta, tena endelea tu kusikiliza, mpaka ujifunze kitu fulani kutokana
na jibu lake Mungu.
6.
Malaika Wanayahudumia Mahitaji Ya Waombao
Mtunga
Zaburi alishangilia kwamba kwa njia ya huduma ya malaika wa Bwana maombi
yake yalijibiwa:
"Nalimtafuta BWANA akanijibu; akaniponya
na hofu zangu zote... malaika wa BWANA hufanya kituo kuwazunguka wale
wamchao na kuwaokoa" (Zaburi 34:4-7).
Tunapoomba,
Mungu anawatuma malaika zake kujibu maombi yetu (Waebrania 1:14). Kila
Mkristo anaye malaika wake mlinzi anayetembea pamoja naye:
"Angalieni msimdharau mmojawapo wa wadogo
hawa. Kwa maana nawaambia ya kwamba MALAIKA WAO mbinguni siku zote huutazama
uso wa Baba yangu aliye mbinguni." - Mathayo 18:10.
Kwa
sababu ya maombi yetu tunayotoa:
"Bwana yu karibu. Msiwe na wasiwasi na
jambo lo lote, lakini katika kila jambo kwa maombi na dua zetu pamoja
na kushukuru, wekeni mambo yenu myatakayo mbele zake Mungu. Ndipo amani
ya Mungu, ipitayo ufahamu wote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu
katika Kristo Yesu." - Wafilipi 4:5-7.
7.
Mtindo Wa Maisha Ya Kikristo
Biblia
inaeleza wazi juu ya mtindo wa maisha ya Kikristo. Kulingana na Waefeso
4: 22-24, Mkristo anatakiwa ku"vua" mtindo wake wa maisha
ya zamani uliotokana na "tamaa zenye kudanganya", na ku"vaa"
mtindo mpya wa maisha ambao ume"umbwa kwa mfano wa Mungu."
Katika maandiko hayo na mwongozo tuligundua kwamba wakati ule wa kuzaliwa
upya sisi tuna"umbwa upya" kuwa watu tofauti ndani ya Kristo.
Mwongozo
huu na miongozo sita inayofuata hutangaza upya mtindo wa maisha ya Mkristo;
huifunua siri ya maisha ya Kikristo yenye furaha. Itakusaidia wewe kujenga
uhusiano wenye nguvu zaidi na Kristo, ambao matokeo yake yatakuwa mtindo
wa maisha ya Kikristo ulio tofauti. Kwa hiyo kaza macho yako kwa Yesu
leo hii, nawe unaweza kuwa na sehemu katika sherehe ile ya mwisho ya
ushindi wakati amani yake Kristo itakapotawala bila kupingwa.
Toa Maoni Hapa Chini