Uwezo wa kukuongoza katika njia
sahihi.
 |
|
“Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu” Zaburi 119:105 ,
neno linatuonyesha tunapoelekea, linatuongoza kutenda kwa usahihi kama vile
nchi bila katiba inapotea, ndivyo mtu anayemwamini Yesu kutokuwa na neno la
Mungu moyoni mwake! lazima atapotea! Mungu akamwambia Joshua “kitabu hiki cha
torati kisitoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na
usiku…ndipo utakapoifanikisha njia yako…” Joshua 1:8. Ni kwa kufuata Neno la
Mungu ndipo mtu anaweza ifanikisha njia yake!
Uwezo wa kutufanya hai.
“maana mtu hatoishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha
Mungu” Mathayo 4:4, neno limejaa uwezo wa kutufanya hai, kama vile mwili bila
chakula unakufa ndipo mtu aliye na Yesu bila neno lake lazima atakufa kiroho.
Neno la Mungu linatupatia nguvu ya kuishi bila neno la Mungu maisha yetu ya
kiroho yamo hatarini, Petro akamwambia Yesu “basi twende kwa nani wewe unayo
maneno ya uzima” maneno ni uzima!
Uwezo wa ushindi dhidi ya shetani.
“tweni upanga wa roho ambao ni neno la Mungu” Waefeso 6:17b ,. Mkristo asiye na
neno la Mungu ni sawa na mwanajeshi asiye na silaha alafu yuko vitani, neno la
Mungu ni salaha kuu dhidi ya shetani “je, neno langu si kama moto, asema Bwana,
na kama upanga ukatao kuwili?” neno la Mungu ni ushindi mkamilifu dhidi ya
shetani! Tukijua kulitumia ni ushindi mkamilifu!
Uwezo wa kupokea kutoka kwa BWANA.
“…….na maneno yangu yakikaa ndani yenu , ombeni lolote mtalipata” Yohana 15:17.
Neno likijaa ndani yetu tutajua jinsi ya kuomwomba Mungu sawa sawa. Ni muhimu
kuishi kwa kusoma neno la mungu ili tuombe sawa na mapenzi yake .
Uwezo wa kuumba.
 |
|
“kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa NENO LA MUNGU….” Waebrania
11:3. “maana yeye alisema ikawa,NA YEYE ALIAMURU IKASIMAMA” Zaburi 33:9 neno
lina nguvu ya kuumba inategemea unaamuru nini na kwa uweza gani! Hivyo hata
ukipita katika ugonjwa unaweza ukasimama mwenyewe ukaamuru kwa uweza wa kuumba
na ugonjwa ukaondoka. Yesu alikuwa anatumia maneno kama haya kuponya watu
“nataka takasika” uwe mzima” “mtoke mtu huyu” haya ni maneno ya kuumba kama
Mungu alivyo tamka “iwe nuru ikawa n.k.” mwanzo 1:1-..
Ni Mungu mwenyewe.
“hapo mwanzo kulikuwa na neno , naye neno alikuwako kwa Mungu naye neno alikuwa
Mungu” Yohana 1:1 ,. Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe, kwasababu huwezi
kumtofautisha mtu na neno lake , Mungu ni neno na ndio maana sisi tukilishika
neno lake tunakuwa washiriki wa tabia ya kiungu “…tupate kuwa washiriki wa
tabia ya kiMungu…” 2Petro 1:4,. The Amplified Bible says that “ sharer
(per-takers) of divine nature” na kwa namna hiyo tunaitwa miungu “mimi nimesema
ndinyi miungu,na wana waa aliye juu wote pia..” Zaburi 82:6. Kumbe tunapata
uwezo wa kuumba kwasababu na sisi ni mi ungu kwa kulishika neno lake!
Tunapataje uwezo wa Neno la Mungu!
“hapo mwanzo kulikuwa na neno, naye neno alikuwako kwa Mungu naye neno alikuwa
Mungu, . Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa yeye; wala
pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa
uzima , nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo yang’aa gizani wala giza
halikuiweza!” Yohana 1:1-5 ,.
Mambo ya kujifunza kutoka kwenye hilo andiko!
1.) Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe hivyo si la kulifanyia mzaha, kamwe huwezi
kumtenganisha mtu na neno lake , ndiyo maana hata Mafalisayo walimtega Yesu
kwenye maneno yake ili wamkamate “wakamviziavizia …ili wamnase kwenye maneno
yake, wapate kumtia kwenye enzi ya mamlaka ya liwali” Luka 20:20. Neno la Mungu
ni Mungu mwenyewe.
2.) Tunajifunza jinsi ya kulitumia neno la Mungu , biblia inasema “ ndani yake
ndimo ulimokuwa uzima” ni muhimu kujua kusikia neno tu haitoshi bali kujua
kilichoko ndani ya neno hilo, Neno la Mungu lina uzima ndani yake ambao huwezi
kuupata kwa kusikia peke yake! Ni kweli kusikia neno la Mungu kunaleta
imani(warumi 10:17) lakini imani inatakiwa kuwekwa kimatendo hapo inamaanisha
udhihirisho wa neno ulilolipokea na hapa ndipo wakristo wengi wanashindwa kujua
na kubaki kumlaumu MUNGU!
3.) Tunaweza kuupokea ule uzima ulio katika neno , kwa kutafakari neno, kivipi
basi? Tuchukue mfano wa tundo kama chungwa huwezi kula pamoja na maganda yake
ni lazima kumenya maganda kwanza ndipo ule , sasa chungwa ni kama neno la Mungu
na maganda ni tafsiri za kibinadamu, Kutafakari neno ni kumruhusu Roho
mtakatifu akufundishe kama tulivyoona hapo juu kuwa NENO NI MUNGU, na hakuna
anayejua mafumbo ya Mungu isipokuwa Roho mtakatifu, (1wakorintho2:10-11) hivyo
Roho hutufunulia kwa kutafakari neno la Mungu Daud akasema “na sheri huitafakari
mchana na usiku”
4.) Je wajua kuto kutafakari neno la Mungu ni kumzimisha Roho wa Bwana?
Biblia inasema “ tusimzimishe Roho wa Bwana” 1Thesalonike 5:19 ,. Kuto
kutafakari neno la Mungu ni kumzimisha Roho wa Bwana, kwa sababu haumruhusu
yeye kukufundisha na huku biblia inasema “Roho atatufundisha kuyashika yote”
sasa ni Muhimu kutafakari neno la Mungu kwa kufanya hivyo tunaruhusu uwezo wa
Neno la Mungu kutenda kazi katika maisha yetu!
5.) Sasa kwa kutafakari ndipo unapo ingiza uzima kwenye maisha yako, kwenye
kazi yako , mafanikio yako (Joshua 1:8) n.k. iyo ndiyo Nuru inayo ng’aa gizani
hata giza na wakuu wake hawataiweza kabisa! Jifunze kujiwekea Ratiba ya kusoma
neno la Mungu kila siku na kutafakari(meditation) unahusianisha na maisha na
kumwomba Roho mtakatifu akufundishe
 |
| Blogger |
Toa Maoni Hapa Chini