Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
KAMATI ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Barabarani, imetoa namba za simu kwa abiria wakati wakizindua kampeni yao ya ‘Abiria Paza Sauti’. Kampeni hiyo inayolenga kupunguza ajali wakati wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, ilizinduliwa juzi katika stendi ndogo ya mabasi yaendayo mikoa ya Ipogolo, mjini Iringa.
Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani, Ramadhani Msangi alizitaja namba hizo kuwa ni 0658376053 ya Trafiki Iringa na 0758807734 ya Sumatra Iringa. Alizitaja namba nyingine kuwa ni 0682887722 ya Trafiki Makao Makuu Dar es Salaam na 0800110019/20 ya Sumatra Makao Makuu Dar es Salaam.
Msangi alisema kwa kupitia namba hizo, abiria wanatakiwa kupaza sauti zao kama kaulimbiu ya kampeni yenyewe inavyotaka kwa kuwaripoti madereva wanaokwenda mwendo kasi, wanaopita magari mengine kwa hatari, walevi na wanaokiuka sheria nyingine zote za barabarani.
“Kampeni hii inawataka pia abiria wakatae kulanguliwa tiketi, kusafiri na dereva mmoja safari ndefu na kupanda gari lisilo na mikanda kwa kutoa taarifa kupitia namba hizo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa mara moja,” alisema.
Akizindua kampeni hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Asas alisema; “tunashirikiana na mabalozi wa usalama barabarani kuhakikisha kwamba abiria wanafanya safari zao kuanzia maeneo mbalimbali ya mkoa wa Iringa wanashiriki kuzuia ajali za barabarani.”
Asas aliipongeza kampeni hiyo akisema imekuja katika kipindi mwafaka cha mwezi Desemba ambacho rekodi zake zinaonesha ndicho kipindi kinachokuwa na ajali nyingi za barabarani.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Leopord Fungu alisema; “pamoja na kwamba kampeni hii inalenga kipindi hiki cha Desemba, hapa Iringa tunataka iwe ya kudumu.”
Mabalozi Wa usalama barabarani Leo katika stendi juu ya Mkoa wa Iringa
Credit to .
Frank Leonard-
Clever Anton-Rsa
Salma Mfaume- Rsa
Hadija Kimaro- Rsa
Damas Anthony-Rsa ( photographer)