TAARIFA ZA KAMPENI YA ABIRIA PAZA SAUTI
PAZA SAUTI NI NINI?
Abiria PAZA SAUTI
ni kampeni maalumu inayoendeshwa na taasisi ya mabalozi wa
Usalama barabarani, yaani Road Safety Ambassadors (RSA) Tanzania
kwaajili ya kukuza uelewa na kuwahimiza watanzania kutambua haki na
wajibu wao wawapo safarini kama abiria.
KWANINI KAMPENI INALENGA ABIRIA?
Kampeni ya PAZA
SAUTI inawalenga abiria hasa wa mabasi ya mikoani kwa kuwa kwanza wao
ndio wanachukua idadi kubwa ya watumiaji wa barabara hasa kipindi hiki
cha kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya. Katika kituo cha mabasi
UBUNGO pekee kuna mabasi Zaidi ya 200 yanayoondoka kwa siku moja, huku
basi moja likiwa na takribani abiria 60, hivyo kufanya idadi ya abiria
Zaidi ya 12,000 wanaosafiri kila siku. Hawa ni abiria wengi sana
ukilinganisha na abiria 15 au 30 wanaoweza kuwa katika daladala au
kwenye chombo kingine cha usafiri.
Sababu nyingine ni kwamba kwakuwa abiria hawa wanasafiri wengi kwa mara
moja kwenye basi, hivyo hata ikitokea ajali madhara yake yanakuwa
makubwa sana kulinganisha na chombo cha usafiri chenye watu chini ya 30.
Aidha abiria hawa wanasafiri na mabasi ya masafa marefu ambapo
kitaalamu kadiri urefu wa safari unavyoongezeka ndivyo vihatarishi
(risks) au visababishi vya ajali vinavyoweza kuongezeka
Tatu, abiria wengi wanaosafiri na mabasi ya mikoani hawana uelewa wa
kutosha kuhusu usalama barabarani, hasa wajibu wao kama abiria. Wengi
wetu tukiwa kama abiria maisha yetu yote tunakuwa tumeyakabidhi kwa
dereva na kondakta wake. Hawa ndio wanaamua mwendo gani basi litembee,
wapi wasimame, wapi wasisimame, nk. Abiria wa basi anakuwa kama mateka
asiye na haki yoyote akiwa kwenye basi, wala hana wajibu wowote. Yeye
akishalipa nauli tu, basi wajibu wake umekwisha, na wakati mwingine hana
thamani tena.
Kwa sababu hii basi ndio sababu baadhi ya abiria hushabikia mwendokasi,
au kuwa maadui wa wale abiria ambao ama wamekuwa wakimwonya dereva au
kutoa tahadhari fulani. Abiria wengi hata pale wanaposimamishwa na
askari na kuulizwa kuhusu mwendo wa dereva, huamua kuficha ukweli na
kumwambia askari kuwa dereva alikuwa anakwenda mwendo sahihi tu. Hata
hivyo ni abiria hawa hawa ambao, inapotokea ajali tumeshuhudia wakiwa
mstari wa mbele katika kusema kuwa mwendo wa dereva ulikuwa mbaya, na
uendeshaji wake ulikuwa wa hovyo. Lakini wakati huu wanaongea haya
tayari wako hospitali, wameshakatika vingo na wengine ni marehemu.
Nne, abiria wengi pia hawatambui haki zao za msingi kama vile kuwa na
tiketi, na faida za kuwa na tiketi. Hawatambui haki zao mathalani pale
gari inapoharibika njiani au anapopewa usafiri tofauti na ule aliolipia,
na wakati mwingine hata basi linapochelewa kuondoka kituoni.
Aidha pamoja na baadhi ya abiria kujua haki zao, wengine wamekuwa
wakishindwa kudai haki hizo kutokana na kutojua wapi kwa kupeleka
malalamiko au kutoa taarifa. Hivyo basi kujikuta wakishindwa kutimiza
wajibu wao. Baadhi ya abiria wameogopa kutetea haki zao au kutimiza
wajibu wao kwa kuona aibu, au kuogopa abiria wenzao wasije wakaanza
kuwasimanga nchi nzima
Kwa ufupi hii ndio sababu, kampeni hii imeanzishwa ili kumjengea abiria
uwezo wa kutambua haki na wajibu wake na kuweza kutekeleza kwa vitendo
wajibu huo.
RTO Iringa akiwa na wana ROAD SAFETY AMBASSODOR (Mabalozi wa Usalama Barabarani)
mara baada ya kusimika bango la ABIRIA PAZA SAUTI Stendi ya Mabasi Ipogoro mkoani Iringa.
Copy the BEST Traders and Make Money :
http://bit.ly/fxzulu
RTO Iringa akiwa na wana ROAD SAFETY AMBASSODOR (Mabalozi wa Usalama Barabarani)
mara baada ya kusimika bango la ABIRIA PAZA SAUTI Stendi ya Mabasi Ipogoro mkoani Iringa.
Copy the BEST Traders and Make Money :
http://bit.ly/fxzulu
RTO Iringa akiwa na wana ROAD SAFETY AMBASSODOR (Mabalozi wa Usalama Barabarani)
mara baada ya kusimika bango la ABIRIA PAZA SAUTI Stendi ya Mabasi Ipogoro mkoani Iringa.
Copy the BEST Traders and Make Money :
http://bit.ly/fxzulu
|
RTO WA Iringa akiwa pamoja na Mabalozi wa usalama Barabarani |
RTO Iringa akiwa na wana ROAD SAFETY AMBASSODOR (Mabalozi wa Usalama Barabarani)
mara baada ya kusimika bango la ABIRIA PAZA SAUTI Stendi ya Mabasi Ipogoro mkoani Iringa.
Copy the BEST Traders and Make Money :
http://bit.ly/fxzulu
|
Mabalozi wa usalama barabarani wa Iringa |
|
Ramdhani Msangi | | | | | |
|
|