Kwa
kutambua umuhimu wa kuwezeshana kiuchumi na kijamii kama sehemu ya utamaduni
mzuri wa Kitanzania, na ukweli kwamba mila, desturi na tabia za mababu zetu ni
kufanya kazi pamoja na kushirikiana
wakati wa shida na wakati wa furaha. Na kwa kuwa tumekuwa na kulelewa katika
mila na desturi hizo, na kwa kuzingatia ukweli wa ugumu wa maisha ambapo si
rahisi mtu kuwa na akiba ya kutosha kukabiliana na dharula mbalimbali.
Tumeamua
kwa kauli moja kuanzisha umoja wa ……………………………
na tunakubaliana kuwa kanuni zifuatazo zifuatwe na kuheshimiwa katika kuendesha
umoja huu.
KATIBA YA UMOJA
Umoja huu utajulikana kwa jina la umoja…………………………………………..
Umoja huu umeanzishwa rasmi tarehe……………, na mwanzo wa
mwaka wa umoja utakuwa ni…………………. ya kila mwaka na makao makuu ya Umoja yatakuwa katika mkoa wa
Dar es salaam.
Kwa madhumuni ya Katiba hii:
(i)
“Umoja” maana yake ni……………………………. ikiwa ni kielelezo kuwa
umoja huu unaundwa na wanachama wakazi wa Dar es salaam.
(ii)
“Mwanachama” ni Mtanzania yeyote aliesoma au
anaeishi wilaya ya Mbinga mbaye amejiunga na umoja kwa kulipia ada ya kujiunga
na ambaye anaendelea kulipia ada ya uanachama ya kila mwezi ipasavyo.
(iii)
Ikitokea kutoelewana kuhusu
tafsiri ya kifungu fulani cha Katiba hii, pamoja na ufafanuzi wa Kamati kuu,
uamuzi wa mwisho utatolewa na wanachama kwa kupiga kura.
(i)
Kuwawezesha wanachama
kufahamiana kwa karibu kabisa na kudumisha ushirikiano katika shida na raha
kama ndugu.
(ii)
Kufanya shughuli za kiuchumi
zitakazolenga kukuza, kuboresha au kuimalisha hali za maisha ya wanachama pale
itakapowezekana, kama vile kununua hisa, kufungua biashara, kutoa mikopo kwa
wanachama.
(i)
Wanachama wa umoja huu ni wakazi wa mkoa wa Dar es
salaam.
(ii)
Bila kuathiri kifungu
chochote katika ibara ya 5(1) mwanachama anatakiwa asiwe na umri chini ya miaka
ishirini (20).
(iii)
Awe na akili timamu na tabia
njema.
(iv)
Awe na uwezo wa kuisoma na
kuielewa na kuitekeleza katiba hii
(v)
Akubali na kulipa kiingilio
pamoja na ada ya uwanachama kila mwezi.
(i) Kuhudhulia vikao vyote vya
chama vitavyofanyika mwishoni au mwanzoni mwa mwezi
(ii) Kutoa
huduma mbalimbali inayotakiwa kwa wenzake wakati wa shida na raha (hasa wakati
wa misiba)
(ii)
Kutoa taarifa ya tukio la
shida au raha kwa viongozi pale linapotokea.
iv) Kulipa kiasi cha mkopo alichochukua kwa wakati
pamoja na riba.
5.3 Masharti na Miiko ya Uanachama:
(i)
Kuitii katiba hii na
kuheshimu maamuzi ya umoja huu.
(ii)
Kuwa mkweli na muadilifu
katika kutoa taarifa yeyote ile inayohusu umoja huu.
(iii)
Kuwa huru na wazi kutoa
mawazo, maoni na dukuduku mbele ya kikao na ni mwiko kueneza majungu mitaani au
popote pale.
(iv)
Kuhudhuria vikao na mikutano
ya umoja kwa kuzingatia muda uliokubaliwa.
(v)
Mwanachama atakuwa na jukumu
na wajibu wa kutoa taarifa kwa uongozi pale atakapopatwa na udhuru
utakaosababisha ashindwe kuhudhuria kikao au mkutano.
(vi)
Mwanachama hai wa umoja huu
ni yule anayelipa michango yake ya kila mwezi kwa kuzingatia muda uliokubaliwa.
(vii)
Kila mwanachama anatakiwa
ajaze fomu maalum ya uanachama itakayotolewa na uongozi.
(viii)
Ni mwiko kwa mwanachama
kusema au kutoa taarifa za uongo.
(ix)
Endapo mwanachama kwa kupitia
taarifa ya uongo ambayo imemsaidia kujipatia kipato katika kikundi kinyume na
utaratibu atashtakiwa Mahakamani.
(x)
Ni mwiko kwa mwanachama
kutohudhuria katika kikao/mkutano bila taarifa.
(xi)
Ni mwiko kwa mwanachama
kuchelewa katika kikao/mkutano bila taarifa.
(xii)
Mwanachama atakayekuwa
safarini nje ya Dar es salaam kwa muda mrefu hali inayoweza kusababisha
asihudhurie vikao vya umoja huu anapaswa kutoa taarifa kwa uongozi wa umoja.
(xiii)
Mwanachama wa umoja huu
endapo atajiengua au kijitoa atarudishiwa 50% tu ya michango yake.
(xiv)
Mwanachama atakayeshindwa kutoa michango yake
ya kila mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo bila kutoa taarifa ya
maandishi ya kuridhisha atatakiwa kulipa deni lake hilo pamoja na faini ya 10%
ya kiasi anachodaiwa. Hali kadhalika kwa yule atakayeshindwa kulipa michango
yake kwa miezi minne mfululizo atatakiwa kulipa faini ya 15% ya kiasi
anachodaiwa. Mwanachama atakayeshindwa kulipa michango yake kwa kipindi cha
miezi mitano mfululizo atatakiwa kulipa faini ya 20% ya kiasi anachodaiwa.
(xv)
Mwanachama ambaye hatatoa
michango yake kwa kipindi cha miezi sita mfululizo bila kutoa taarifa ya
maandishi yenye sababu za msingi atakuwa amejitoa mwenyewe katika umoja,
kutokana na hilo hatarejeshewa michango yake ambayo alilipa hapo awali. Bila
kuathiri kifungu chochote cha katiba hii, mwanachama ambaye atatoa taarifa yake
kwa maandishi kuhusu nia yake ya kuendelea kulipia michango yake ya kila mwezi
baada ya kushindwa kulipa kwa miezi sita mfululizo kama ilivyoelezwa hapo juu,
atapaswa kulipa michango yake yote anayodaiwa pamoja na faini ya 25% ya deni
hilo, hata hivyo mwanachama huyo atatakiwa kuandika maelezo kwa uongozi wa
umoja akieleza nia yake ya kujirekebisha, kuheshimu na kutekeleza maamuzi ya
umoja.
a) Mwanachama yeyote anao uhuru wa kujitoa katika umoja kwa kuandika barua
kwa uongozi akielezea uamuzi wake wa kujitoa.
b) Mwanachama yeyote atakayeshindwa kutoa michango yake kwa kipindi cha
miezi sita mfululizo atahesabiwa amejitoa katika umoja.
c) Mkutano mkuu utakuwa na uwezo wa kumfukuza mwanachama yeyote pale tu
atakapothibitika kuwa kwa maksudi amevunja masharti ya katiba ya umoja huu.
Hata hivyo hatua hii itachukuliwa baada ya mhusika kushindwa kujirekebisha
baada ya uongozi kumpa onyo kali kwa maandishi
Wanachama wote ni sawa ndani ya umoja kwa msingi wa
kupata msaada kwa kiasi kilicho sawa pasipo ubaguzi wa aina yoyote.
(i)
Muundo wa umoja utakuwa Mkutano Mkuu ikiwa ndicho
chombo cha juu kabisa, ikifuatiwa na Kamati Kuu na mwisho wanachama.
(ii)
Kutakuwa na Mwenyekiti wa umoja ambaye
atachaguliwa na wanachama kutoka miongoni mwa wanachama. Mwenyekiti ndiye
atakayekuwa kiongozi wa umoja kwa maana ya kuongoza mikutano yote ya umoja na
ndiye Msemaji Mkuu wa umoja.
(iii)
Kutakuwa na Makamu Mwenyekiti wa umoja ambaye
atachaguliwa na wanachama kutoka miongoni mwa wanachama. Makamu Mwenyekiti
ndiye atakayefanya shughuli zote za uenyekiti pale ambapo Mwenyekiti hayupo.
(iv)
Kutakuwa na Katibu wa umoja ambaye atachaguliwa na
wanachama kutoka miongoni mwa wanachama. Katibu wa umoja ndiye atakayekuwa
Mtendaji Mkuu wa shughuli zote za umoja kwa maana ya kutayarisha na kutoa taarifa
katika mikutano yote ya umoja juu ya kazi zifanywazo na umoja huu. Pia
atawajibika kuandaa na kuitisha mikutano yote ya umoja kama watakavyoshauriana
na Mwenyekiti. Aidha, Atatayarisha na kutunza kumbukumbu za kazi zote na
mikutano yote ya umoja huu.
(v)
Kutakuwa na Mweka Hazina wa umoja ambaye
atachaguliwa na wanachama kutoka miongoni mwa wanachama. Mweka Hazina
atawajibika kila mara na mapema
iwezekanavyo kuwasilisha Benki katika Akaunti ya umoja michango yote
itakayokusanywa. Pia Mweka Hazina atawajibika kuandaa gharama za uendeshaji na
kutoa taarifa ya Mapato na Matumizi katika kila kikao cha kawaida cha Kamati
Kuu. Aidha, Mweka Hazina atatakiwa kutunza vizuri kumbukumbu zote zinazohusiana
na mapato na matumizi ya umoja, zikiwemo risiti za kuweka na kutoa fedha Benki
na kuzionesha kwa mwanachama/wanachama pale itakapohitajika.
(vi)
Kutakuwa na Muamasishaji wa umoja, ambaye
atachaguliwa na wanachama kutoka miongoni mwa wanachama. Muamasishaji huyo
ndiye atakayefanya shughuli zote za kuhamasisha watu katika kutoa michango,
kushiriki shughuli za kijamii, kiuchumi na uhudhuriaji wa vikao/mikutano .
(vii)
Viongozi wote waliotajwa hapo juu watakaa
Madarakani kwa kipindi cha ………... Baada ya kipindi hicho kuisha kutafanyika
uchaguzi wa viongozi ambapo kiongozi anayeondoka madarakani anaweza kugombea
tena. Iwapo itatokea kwamba Kiongozi yeyote ameshindwa kufanya kazi zake
ipasavyo, mwanachama yeyote anaweza kutoa hoja ya kuvuliwa madaraka kiongozi
huyo, hoja ambayo ataiwasilisha katika Mkutano wa kila mwezi. Kama hoja hiyo
itaungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe waliohudhuria, kiongozi
aliyetuhumiwa atakuwa amevuliwa madaraka na itabidi uchaguzi mdogo wa kumchagua
kiongozi mwingine ufanyike.
(viii)
Endapo itatokea kwamba kiongozi yeyote aliyetajwa
katika kifungu cha 7(i) hadi 7(vi) cha Katiba hii ameondoka madarakani kwa
namna yoyote ile kabla ya kuisha kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi tangu
uchaguzi mkuu ufanyike, kutafanyika uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi iliyoachwa
wazi.
(i)
Kiingilio cha kujiunga na
Umoja ni Tshs.50,000/=.
(ii)
Kila mwanachama atatakiwa
kutoa ada ya kila mwezi ambayo ni Tshs. 20,000/=.
Kiwango cha ada ya kila mwezi kinaweza kubadilika kulingana na wakati na kwa
idhini ya wanachama.
(iii)
Mtu atakayetaka kujiunga na
umoja huu baada ya umoja kuanzishwa atatakiwa kutoa kiingilio kiasi cha Tshs.……….= pamoja na kiasi cha nusu ya
jumla ya michango ya ada ya kila mwezi kuanzia mwanzo wa michango ilipoanza
wakati umoja unaanzishwa hadi sasa.
(iv)
Aidha, umoja unaweza kupokea
mchango wa ziada kutoka kwa mwanachama au mtu yeyote au chombo kingine chochote
kinachoendesha shughuli zake kihalali kwa madhumuni ya kuimarisha umoja.
(v)
Kifo cha mwanachama chama kitachangia……………….
(vi)
Kifo cha mwenza/mume/mke halali
kisheria chama kitachangia Tshs………….
(i)
Michango yote ya kiingilio cha kujiunga na umoja
na ada ya kila mwezi itakuwa inakusanywa katika kila mkutano/kikao cha kila
mwezi cha umoja.
(ii)
Kila mwanachama ana wajibu wa kuwasilisha mchango
wake wa kila mwezi kwa Mweka Hazina.
(iii)
Iwapo mchango wa kila mwezi utafuatiliwa na Mweka
Hazina kwa mwanachama nje ya mahali ambapo umoja utakubaliana ndipo mahali pa
kuendeshea mikutano au shughuli za umoja (ofisi ya Umoja) atatakiwa kufidia gharama za nauli
alizotumia mkusanyaji kufuatilia mchango huo, huu ni wajibu wa mweka hazina
kufuatilia michango.
(i)
Kutakuwa na Akaunti ya Umoja katika Benki ambayo
wanachama wataichagua, ambapo fedha zote za umoja zitahifadhiwa. Akaunti ya
umoja huu itaitwa ………………………………...
(ii)
Katika kufungua Akaunti ya Umoja katika Benki,
kutakuwa na watu wanne (4) kutia sahihi. Watu hao ni Mwenyekiti wa umoja,
Katibu wa umoja, Mweka Hazina wa Umoja pamoja na mwanachama mmoja aliyeteuliwa
na mkutano mkuu.
(i)
Baada ya Kamati Kuu kuidhinisha utoaji wa fedha
Benki watu wasiopungua watatu kati
ya wanne waliotajwa katika kifungu cha 9.3(ii) cha Katiba hii ndio watakaotoa
(“draw”) fedha zilizoidhinishwa.
(i)
Kutakuwa na Kamati Kuu ambayo ndiyo itakayokuwa
chombo kikuu cha kuratibu na kutekeleza shughuli za umoja. Kamati Kuu itapanga na kusimamia matumizi ya fedha
za umoja.
(ii)
Kamati Kuu itakuwa na wajumbe
sita (6) ambao ni Mwenyekiti, Katibu, Mweka Hazina na Wajumbe watatu (3)
watakaochaguliwa na wanachama kutoka miongoni mwa wanachama.
(iii)
Muda wa Kamati Kuu kuwepo
madarakani ni miaka……………………
(iv)
Aidha Kamati Kuu inaweza
kuunda kamati ndogondogo kwa lengo la kuisaidia kazi Kamati Kuu.
Kutakuwa na mikutano/vikao vifuatavyo:-
(i)
Kikao hiki kitajadili shughuli na mambo mbalimbali
ya Umoja ikiwa ni pamoja na wanachama kupewa taarifa ya mapato na matumizi na
madeni wanayodaiwa wanachama.
(i)
Mkutano Mkuu utakuwa ndicho kikao cha juu na ndicho
chombo chenye maamuzi ya mwisho kuhusu umoja wa ……………………….. na utafanyika mara mbili kwa mwaka na notisi ya mkutano
huo itatolewa siku kumi na nne (14) kabla ya tarehe ya mkutano.
(ii)
Akidi ya Mkutano Mkuu itakuwa
si chini ya nusu (1/2) ya wanachama wote.
a) Kutathmini mafanikio na matatizo ya shughuli za umoja kwa mwaka.
b) Kupokea taarifa ya fedha kwa mwaka, kuweka malengo na mikakati ya
shughuli mbalimbali kwa mwaka unaofuata.
c) Kuchagua viongozi wa umoja iwapo muda wa viongozi kukaa madarakani
umekwisha.
d) Kuthibitisha au kabatilisha maamuzi yoyote kutoka katika kikao chochote
cha chini kwa mujibu wa Katiba hii.
e) Katika kutafakari ni nini kifanyike ili kuboresha umoja, kama hali ya
umoja itaruhusu wanachama wanaweza kujipongeza.
(i)
Mkutano huu utaitishwa endapo kutakuwa na jambo
lolote linalohitaji maamuzi ya haraka.
(ii)
Akidi ya Mkutano wa Dharula
itakuwa ni nusu (1/2) ya wanachama wote.
Kamati Kuu au Mwanachama yeyote anaweza kutoa mapendekezo
ya mabadiliko ya kifungu/vifungu fulani vya Katiba hii. Mapendekezo hayo
yatajadiliwa na Kamati Kuu na kupelekwa katika Mkutano Mkuu kwa ajili ya
maamuzi. Mapendekezo hayo yanaweza kupitishwa iwapo yatapata theluthi mbili (2/3)
ya kura za wajumbe.
Umoja huu unaweza kukoma kwa sababu zifuatazo:-
(i)
Kukosa kabisa wanachama kwa
sababu zozote zile;
(ii)
Robo tatu (3/4)
ya wanachama wakiamua Umoja uvunjwe kwa kutoa notisi ya siku 14. Iwapo hili
likitokea, Mkutano Mkuu utatoa tamko kuhusu mali na madeni
yatakavyoshughulikiwa.
Kama hali ya mtaji wa umoja itaruhusu, umoja huu unaweza kuanzisha
shughuli yeyote ile halali kwa kuzingatia idhini ya wanachama wasiopungua robo
tatu (¾) ya wanachama wote, kwa lengo la kuongeza kipato cha umoja. Aidha
Kamati Kuu ndicho chombo kitakachowajibika katika kuandaa kanuni na utaratibu
wa usimamiaji wa shughuli hiyo itakayopendekezwa.
IMEPITISHWA na Mkutano Mkuu wa umoja wa ………………………
hapa Dar es Salaam leo
tarehe …………
mwezi …………………….. 2015.
……………………………………
…………………………………….
Mwenyekiti
Katibu