KUMTUMIKIA MUNGU KATIKA UJANA | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Tuesday, December 15, 2015

KUMTUMIKIA MUNGU KATIKA UJANA

“NINATAKA nifanikiwe maishani.” Ndivyo alivyosema msichana mmoja. Inaelekea wewe pia unataka kufanikiwa. Lakini unawezaje kufanikiwa maishani? Huenda vyombo vya habari, marika wako, hata labda walimu wako, wakasema kwamba mtu mwenye mafanikio ni yule ambaye amechuma pesa nyingi na ana kazi nzuri.
Hata hivyo, Biblia huwaonya vijana kwamba kutafuta mali ni “kujilisha upepo” tu. ( ) Sababu moja ni kwamba, ni vijana wachache tu wanaofanikiwa kuwa matajiri na mashuhuri. Mara nyingi, wale wanaofanikiwa huvunjika moyo sana. Kijana mmoja Mwingereza aliyepata kazi nzuri alisema kwamba kufanikiwa kupata mali ni kazi bure. ‘Unapofikiria matokeo yake unakatishwa tamaa.’ Naam, nyakati nyingine huenda kazi ikamwezesha mtu kupata mali na umashuhuri. Lakini haiwezi kutosheleza ‘uhitaji wako wa kiroho.’ ( ) Isitoshe, huonya kwamba “ulimwengu unapitilia mbali.” Hata ukifanikiwa katika ulimwengu huu, mafanikio hayo hayatadumu.
Hivyo, huwasihi vijana hivi: “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako.” Naam, kumtumikia Yehova Mungu ndiyo njia bora ya kutumia maisha yako. Lakini kwanza, ni lazima ustahili kumtumikia Mungu. Unawezaje kustahili? Na kumtumikia Mungu huhusisha nini?

Kwanza kabisa, unapaswa kukuza tamaa ya kumtumikia Mungu—na tamaa hiyo haitokei tu bila jitihada yoyote, hata kama wazazi wako ni Wakristo. Ni lazima wewe mwenyewe uwe na uhusiano pamoja na Yehova. Msichana mmoja asema hivi: “Kusali humsaidia mtu kuwa na uhusiano pamoja na Yehova.”—
.
Andiko la linaonyesha hatua nyingine unayopaswa kuchukua. Linasema hivi: ‘Jithibitishieni wenyewe mapenzi ya Mungu yaliyo mema na yenye kukubalika na makamilifu.’ Je, umewahi kutilia shaka mambo fulani ambayo umefundishwa? Basi tii shauri la Biblia, na ‘ujithibitishie mwenyewe’ kwamba mambo hayo ni ya kweli! Fanya utafiti. Soma Biblia na vichapo vyenye habari za Biblia. Hata hivyo, kujifunza juu ya Mungu si jambo la kutumia akili tu. Tumia wakati kutafakari yale unayosoma ili yaingie kabisa moyoni. Ukifanya hivyo, upendo wako kwa Mungu utazidi.— .
Kisha, jaribu kuwaeleza wengine yale unayojifunza, labda wanafunzi wenzako shuleni. Hatua inayofuata ni kuhubiri nyumba hadi nyumba. Mara kwa mara unapohubiri, unaweza kukutana na mwanafunzi mwenzako, na huenda jambo hilo likakubabaisha. Lakini Biblia inatusihi ‘tusiaibikie habari njema.’ ( ) Unapeleka ujumbe unaowapa watu uhai na tumaini! Basi, ya nini uaibike?
Iwapo wazazi wako ni Wakristo, huenda tayari umehubiri nao. Lakini je, unaweza kufanya mengi zaidi badala ya kunyamaza kimya mlangoni au kugawa tu magazeti na trakti? Je, wewe mwenyewe unaweza kumhubiria mwenye nyumba, ukimfundisha kupitia Biblia? Iwapo huwezi, basi waombe wazazi wako au mtu mwingine mkomavu katika kutaniko akusaidie. Weka mradi wa kustahili kuwa mhubiri asiyebatizwa wa habari njema!
Muda si muda, utachochewa kujiweka wakfu, yaani kuweka nadhiri ya kumtumikia Mungu toka wakati huo na kuendelea. ( ) Hata hivyo, kujiweka wakfu si siri. Mungu anataka kila mtu afanye “tangazo la hadharani kwa ajili ya wokovu.” ( ) Wakati wa ubatizo, kwanza mtu hutangaza imani yake kwa maneno. Kisha, anabatizwa katika maji. ( ) Ni kweli kwamba ubatizo ni hatua nzito. Lakini usisite kubatizwa ukifikiri kuwa hutafaulu. Ukimtegemea Mungu akupe nguvu, atakupa “nguvu ipitayo iliyo ya kawaida” ili usimame imara.—
.
Unapobatizwa, unakuwa Shahidi wa Yehova. ( ) Jambo hilo lapasa kuathiri sana jinsi utakavyotumia maisha yako. Kujiweka wakfu hutia ndani ‘kujikana mwenyewe.’ ( ) Huenda ukatupilia mbali miradi yako na mambo mengine uliyotamani kutimiza na ‘kutafuta kwanza ufalme wa Mungu.’ (
) Kujiweka wakfu na kubatizwa huandaa njia nyingi za kufanya hivyo. Ebu tuchunguze baadhi ya njia hizo.
Njia za Kumtumikia Mungu Wakati Wote
● Upainia ni njia moja. Mhubiri aliye painia ni Mkristo aliyebatizwa mwenye mfano mzuri. Yeye hupanga kutumia angalau saa 70 kila mwezi ili kuhubiri habari njema. Ukitumia muda mwingi zaidi shambani, utaweza kuboresha ustadi wako wa kuhubiri na kufundisha. Mapainia wengi wamepata shangwe kwa kuwasaidia wanafunzi wao wa Biblia wawe Mashahidi waliobatizwa. Hakuna kazi nyingine yoyote inayoweza kufurahisha na kuridhisha zaidi ya hiyo.
Mapainia wengi hufanya kazi ya muda ili wajiruzuku. Wengi wao hupangia kimbele jambo hilo kwa kujifunza ufundi fulani shuleni au kufundishwa na wazazi wao. Huenda wewe na wazazi wako mkaona kwamba itafaa upate masomo fulani ya ziada baada ya kumaliza shule ya sekondari. Ikiwa ndivyo, hakikisha kwamba mradi wako si kupata pesa nyingi, bali ni kutegemeza huduma yako na labda kuwa mhudumu wa wakati wote.
Hata hivyo, badala ya kutanguliza kazi yake ya kujiruzuku, painia hutanguliza huduma yake ya kuwasaidia wengine wapate uhai. Mbona usiweke mradi wa kuwa painia? Mara nyingi, upainia hutokeza mapendeleo mengine. Kwa mfano, baadhi ya mapainia huhamia maeneo yenye uhitaji mkubwa wa wahubiri wa Ufalme. Wengine hujifunza lugha ya kigeni na hutumikia katika kutaniko la lugha ya kigeni nchini kwao au hata katika nchi nyingine. Naam, kufanya upainia huleta uradhi maishani!
● Utumishi wa mishonari ni njia nyingine. Tangu mwaka wa 1943, Shule ya Biblia ya Gileadi ya Watchtower imewawezesha mapainia wanaostahili kupata masomo bora yanayowazoeza kwa ajili ya utumishi wa mishonari. Wahitimu hupewa mgawo wa kuwa wahubiri wa wakati wote katika nchi za kigeni. Katika baadhi ya nchi hizo, hali za maisha ni ngumu, kwa hivyo ni muhimu mishonari kuwa na afya nzuri na nguvu. Hata hivyo, mishonari huishi maisha yenye kusisimua na yenye kuridhisha.
● Shule ya Mazoezi ya Kihuduma
ilianzishwa ili kuwazoeza wazee na watumishi wa huduma waseja wanaostahili. Masomo hayo ya majuma manane huhusisha mambo mengi kama vile majukumu ya wazee na watumishi wa huduma, kusimamia mambo, na kusema mbele ya watu. Wengine hupewa mgawo kutumikia katika nchi zao. Wengine hupewa mgawo kutumikia katika nchi nyingine.
● Utumishi wa Betheli huhusisha kujitolea kutumikia katika mojawapo ya ofisi za tawi za Mashahidi wa Yehova. Washiriki wengine wa familia ya Betheli huhusika moja kwa moja katika utayarishaji wa vichapo vya Biblia. Wengine hupewa migawo inayotegemeza kazi hiyo, kama vile udumishaji wa majengo na vifaa au kutunza familia ya Betheli. Migawo yote ni mapendeleo matakatifu ya kumtumikia Yehova. Zaidi ya hayo, wale wanaotumikia katika Betheli wanajua kwamba lolote wanalofanya, huwafaidi ndugu zao wengi ulimwenguni pote.
Nyakati nyingine ndugu walio na ustadi maalum huitwa ili watumikie Betheli. Hata hivyo, wengi huzoezwa wanapowasili. Wanabetheli hawatumikii ili wapate mali bali wanatosheka na chakula, makao, na rudishio dogo la gharama kwa ajili ya mahitaji yao. Kijana mmoja anayetumikia katika Betheli anasema hivi kuhusu utumishi wake: “Unafurahisha sana! Ratiba ya kila siku si rahisi, lakini nimepata baraka nyingi kwa kutumikia hapa.”
● Utumishi wa kimataifa humwezesha mtu kushiriki katika ujenzi wa ofisi za tawi na Majumba ya Ufalme. Watumishi wa kimataifa husafiri kwenda nchi nyingine ili kusaidia kufanya kazi hizo za ujenzi. Huo ni utumishi mtakatifu, sawa na kazi ya wale watu waliojenga hekalu la Solomoni. ( ) Watumishi wa kimataifa hutunzwa kama Wanabetheli. Ndugu na dada hao wana pendeleo lililoje la kumsifu Yehova kwa njia hiyo!
Mtumikie Yehova kwa Nafsi Yote
Kumtumikia Yehova ndiyo njia bora ya kutumia maisha yako. Mbona usifikirie kuweka mradi wa kumtumikia Mungu wakati wote? Zungumza na wazazi wako, wazee wa kwenu, na mwangalizi wenu wa mzunguko kuhusu utumishi wa wakati wote. Iwapo unataka kwenda Betheli, Gileadi, au kwenye Shule ya Mazoezi ya Kihuduma, hudhuria mikutano inayozihusu inayofanywa kwenye makusanyiko ya mzunguko na ya wilaya.
Naam, si wote wanaoweza kustahili au kutumikia wakati wote. Nyakati nyingine matatizo ya afya, hali za kiuchumi, na majukumu ya familia huwazuia watu wasifanye mengi sana. Hata hivyo, Wakristo wote waliojiweka wakfu wanapaswa kutii amri hii ya Biblia: “Lazima umpende Yehova Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa akili yako yote.” (
) Yehova anataka ufanye yote uwezayo kulingana na hali zako. Hivyo basi, hata hali yako iweje, jambo kuu maishani mwako na liwe kumtumikia Yehova. Weka miradi ya kiroho unayoweza kufikia. Naam, “mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako”—nawe utabarikiwa daima!
Mhubiri 4:4
Mathayo 5:3
1 Yohana 2:17
Mhubiri 12:1
Zaburi 62:8; Yakobo

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.