Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
USIMLAUMU MUNGU KWENYE NDOA YAKO
Mungu ametupa nafasi siku ya jumatano ya tarehe 09/12/2015, ni nafasi ya kuja kupata maarifa kwa ajili ya ndoa zetu. Najua changamoto iliyopo sasa hivi makanisani ni kwamba watu wanataka vitu rahisi, na watu wameaminishwa kwamba maombezi ni kila kitu, kwa hiyo hawataki maarifa wanataka maombezi, wanataka kuwekewa mikono, na siku hizi wanawekewa na miguu.
Watapiga simu kwa watumishi wakitaka waombewe ndoa zao zikae sawa, na watumishi waongo wanawaibia, wanawaambia watoe sadaka za kumgusa Mungu ili aponye ndoa zao (WIZI HUU!!) na mambo yanazidi kuwa mabaya….sio kwa sababu hakuna maombi, bali ni kwa sababu HATUNA MAARIFA.
Na maarifa yanapokuja watu hawataki kujifunza, wanadhani wanaelewa kila kitu so long as they are Christians, wanaenda makanisani, they think they know everything, lakini hatujui kila kitu ndugu zangu, tunahitaji kujifunza kila leo. Na wengine wanaweza wasije wakisema ni mbali, lakini wanaweza kufuata mambo ya dunia hii kwa gharama yoyote na kokote, lakini sio mambo ya Mungu, huku ni kuvamiwa kiroho!
Mungu alishatuambia kwa kinywa cha Nabii Hosea “WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWA KUKOSA MAARIFA” (HOSEA 4:6) na alirudia kwa kinywa cha Mtume Paulo kwamba “WANA JUHUDI NYINGI KWA AJILI YA MUNGU, LAKINI SI KATIKA MAARIFA” (WARUMI 10:2).
Mwanandoa, semina hii ya jumatano sio semina ya kawaida, sio semina ambazo pengine umezoea kwenda, hii ni zaidi ya semina, ni tiba, ni dawa na kinga kwako na kwa vizazi vinge.
KUMETOKEA NINI? MBONA WENGI WANALIA KWENYE NDOA?
Hawa ni wale ambao enzi za urafiki/uchumba waliitana majina matamu, waliishi kwa furaha ungedhani wako paradise, leo hii wanaitana majina ya wanyama na wadudu, wanaishi kwa kuvumiliana au kuwindana humo ndani. Kila mmoja ni shubiri kwa mwingine.
KUMETOKEA NINI? Nilisema hivi, kuna mambo baadhi ya Mapadri na Wachungaji hawatakaa wakwambie, wanasaikolojia hawatakaa wakwambie, lakini ndiko kulikoficha ukweli kuhusu ndoa zenye migogoro, na ni ukweli huo utakaowarejesha pamoja wapenzi hawa kama wataukubali.
Sikiliza! Kama wewe ni mwanandoa, au umeachana na mume/mke wako, au uko kwenye maandalizi ya kufunga ndoa, nataka nikushauri kitu, kwamba usikose semina hii tarehe 09/12/2015. Ni kuanzia saa 6:00 mchana pale SAMSARA RESTAURANT – STENDI YA MAKUMBUSHO.
KIINGILIO? Wengi wameuliza hili, sipendi kuita kiingilio, lakini kwa ajili ya mazoea, neno la Mungu halina malipo. Kutokana na mahali tutakapokuwapo, masomo yatakayogawiwa kwa washiriki, vinywaji na chakula cha mchana kila mmoja atalazimika kutoa shilingi 12,000/=
Kama utashiriki jisajili sasa, kwa maelekezo zaidi tumia namba 0672 663 482.
MCH. OVERCOMER DANIEL
MLIMA WA MAKIMBILIO
DAR ES SALAAM – TANZANIAMCH. OVERCOMER DANIEL
MLIMA WA MAKIMBILIO
DAR ES SALAAM – TANZANIA
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.