Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
Mzozo Burundi wasababisha wahisani kusitisha misaada ya bajeti
Baada ya ziara nchini Burundi kujionea hali ya kibinadamu, Mkuu wa operesheni kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa kibinadamu, OCHA, John Ging, amesema mzozo wa kisiasa umesabisha nchini humo umesababisha wahisani kusitisha msaada wa kibajeti na hivyo kuzorotesha hali ya kibinadamu na kiuchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani, Bwana Ging amesema bajeti ya Burundi inategemea zaidi ya asilimia 51 kutoka kwa wahisani kwa hiyo kusitishwa kwa misaada kumeongeza shida juu ya shida.
(Sauti ya Ging)
“Wahisani wakuu wanaosaidia bajeti kama vile upatikanaji wa huduma muhimu za umma wamesitisha misaada hiyo. Kwa hiyo basi huduma hizo sasa hivi hazina fedha, mathalani dawa muhimu, malipo ya mishahara na kadhalika.”
Bwana Ging amesema kwa sasa yaonekana hakuna mwenye jibu kwenye mzozo wa Burundi na hilo ndio tatizo kwa hiyo..
(Sauti ya Ging)
“Tunatoa wito kwa wale wenye wajibu wa kisiasa kuongeza juhudi zao maradufu! Kila mmoja anapaswa ajikite na wajibu wake, mimi najikita suala la kibinadamu lakini nina wajibu wa kupaza sauti na kusema kuwa hali ya kibinadamu inazorota, na suluhu iko wapi? Si ya kibinadamu! Sisi hatuna jibu bali ni suluhu ya kisiasa!”
Kwa mujibu wa Ging, hali ya kibinadamu inashuka kwa kasi na amenukuu ripoti ya maendeleo ya kibinamu inayoiweka Burundi nafasi ya 194 kati ya nchi 197.
(Pichani:Raia wa Burundi wakifungasha virago kwenda kambini: UNHCR/Video capture)