Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA KIBALOZI
Popote pale ulipo balozi wa usalama barabarani una wajibu mzito wa kutekeleza majukumu yako na kwa ukamilifu. Majukumu hayo ni pamoja na wewe mwenyewe kuwa mfano wa utii wa sheria bila shuruti. Ukikosea unalipa lakini pia unajitahidi sana kutofanya makosa yanayoepukika. Hata hivyo zipo njia mbali mbali za namna unavyoweza kutekeleza majukumu yako.
1. KUONGEA NA ABIRIA UWPAO NDANI YA BASI
Ikiwa unasafiri na basi husika unaweza kuamua kuongea na abiria kwa kuwahimiza kufunga mikanda na kuhakikisha usalama wao muda wote wanapokuwa safarini ikiwamo kuzingatia usafi na kuchukua tahadhari muhimu, hata ile ya kutokupokea kitu hovyo kutoka kwa mtu asiyemfahamu. Hii inaweza kusaidia hata wahudumu wa basi kujua ndani ya basi kuna mtu anayejitambua hivyo dereva akawa makini wakati wote. Usisubiri hadi dereva aanze kuharibu ndio uanze kuongea.
2. UNAWEZA KUTOA TAARIFA YA SIRI TU
Kulingana na mazingira uliyopo mfano kwenye chombo cha usafiri. unaweza kuamua kutoa taarifa ya siri bila wewe kujulikana. Mfano ukapiga picha ya hali ya basi ilivyo mf.kukosa mikanda, au tiketi kutojazwa inavyotakiwa au hata kuzidishiwa nauli kisha ukatuma picha hizo na ujumbe unaoelezea hali hiyo kwenda nambari 0682 887722. Uzuri wa kutuma ujumbe moja kwa moja kwenda namba hii ni kwamba TCC watakapopeleka taarifa kwa askari walipo ground namba itakayosomeka ni ya kwao kama originators. Usisahau kusema mnakotokea, mlipo na mnapoelekea. Tunawaasa mabalozi pia kutumia njia hii kutokana na mazingira mengine ya utoaji taarifa kuwa hatarishi, na ndio maana njia hii pia inakubalika.
3. KWA KURIPOTI KWENYE GROUPS ZA RSA AU FACEBOOK
Unaweza kuripoti moja kwa moja kupitia groups za rsa zilizopo whatsapp, na telegram. Taarifa utakayoitoa kwenye group itasomwa nchi nzima kwa wakati huo huo na ufuatiliaji kufanyika kiurahisi. Angalizo ni kwamba ukituma taarifa facebook inaweza kuchelewa kufanyiwa kazi.
4. KWA KUTUMA KWA ADMIN
Unaweza kuripoti kwa kutuma ujumbe moja kwa moja inbox kwa admin ambapo admin husika atareport kwenye mamlaka na kukupa mrejesho baadae. admin anaweza pia kupost kwenye group.
MADHARA YA KUTORIPOTI
Madhara ya kutoripoti au kutekeleza wajibu wako, usishangae gari inapata ajali na wewe umo ndani au hata wewe mwenyewe balozi unalipa nauli kubwa kuliko ile inayoruhusiwa. Au wakati mwingine hata gari linawatelekeza njiani na mnakosa msaada kwa jambo ambalo lingeweza kushughulikiwa mapema. Hapo ndilo unakuja ule msemo usemao "NINGEJUA HUJA BAADAYE".
Balozi pia uwe na tabia ya kureport uwapo safarini ili mabalozi wenzio wajue unatoka wapi unakwenda wapi ili hata ukitokea kuna dharula waweze kukupa msaada haraka. kwani network ya mabalozi ni kubwa nchi nzima. Usisafiri kibubububu isipokuwa tu pale kunapokuwa na sababu za msingi za kufanya hivyo.
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.