Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
✨FASDO TANZANIA✨
SIKU 3 ZA KUJIPANGA
#JIJUE #JIJUE_CAMPAIGN #JIPANGE
Siku 1
Kadri tunavyozidi kukua, ndio majukumu na vitu vya kufanya vinaongezeka.
Kila siku inapoanza, mwanadamu anakuwa ana vitu vingi anavyotakiwa kuvifanya.
Ili afanikiwe katika maisha, anahitaji kujua vipi ni vya muhimu na vya kuanza navyo, vipi vya kusubiri kufanywa baadaye na vipi vya kuwaachia wengine wafanye.
Hii inaleta kitu kinachoitwa mpango au kupanga. #jipange
Kwanini tupange?
1. Muda hautoshi kukamilisha kila kitu unachotakiwa kukifanya kama usipougawanya vizuri.
2. Rasilimali hazitoshi kukamilisha kila kitu kwa wakati wake hivyo zinatakiwa zielekezwe kwa vitu muhimu.
3. Kupanga ni kuuona mwisho wa jambo kabla haujalianza. Ni kuona kitu, shughuli au jambo fulani likiwa limekamilika kabla hujaanza kulifanya.
4. Kuna mambo ya muhimu lakini sio ya haraka na ya haraka na sio ya muhimu na yasiyo ya haraka wala muhimu. Kupanga kutakufanya uyajue yapi ni yapi.
5. Maisha yanafuata kanuni ya mayai kwenye kikapu.
Unatakiwa kuchagua, aidha kuweka mayai yote kwenye kapu moja lakini unahakikisha macho yako, akili yako, mikono yako na hisia zako zote zinaangalia kikapu na kukichukua kwa umakini. Au la, basi uyapunguze kwenye vikapu tofauti tofauti na uwape watu tofauti tofauti, wewe ubaki na kimoja au viwili. Hii ni kanuni inayoamua nani anafikia mafanikio na kwa kiasi gani.
Zoezi (Chukua peni na karatasi uandike)
1. Je, una malengo unayotaka kuyatimiza? Yataje kwa kuyagawanya katika vipengele.
Mf. Kiuchumi - Nataka nipate milioni 1 kwa mwezi.
Kifamilia - Nataka niongeze muda wa kukaa na mke wangu. N.k
2. Gawanya kila lengo katika muda mfupi mfupi. Halafu weka rasilimali itakayokusaidia kufanikisha lengo hilo.
Mf. Milioni 1 kwa mwezi - Kila wiki Laki 2.5 (Biashara)
3. Je, katika hayo malengo yako, yatachukua muda gani kukamilika?
Mf. Nataka nianze kusoma diploma February - Hili lengo litachukua miaka miwili kulikamilisha.
Nataka kuanza kujenga nyumba December - Hili litachukua miezi 6 n.k
4. Je, katika malengo uliyonayo, kuna ambalo ulikuwa nalo mwaka jana? Kwanini halikukamilika?
5. Fikiria na waza kana kwamba hakuna kikwazo chochote katika kufikia unachotaka. Ungetamani uwe na maisha ya aina gani?
Andika bila kuogopa kila linalokuja akilini.
#JITAMBUE #JIJUE #JIJUE_CAMPAIGN
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.