Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
✨FASDO TANZANIA✨
SIKU TATU ZA KUJIJUA 2016
#JIJUE
SIKU 1
A. MIMI ni NANI?
Kuna tofauti kati ya jinsi watu wanavyokufahamu na jinsi halisi ulivyo.
Kuna namna watu wanavyokuita na kuna namna jinsi ulivyo.
Kuna namna watu wanavyokufikiria na jinsi vile ulivyo.
Ili uyafikie mafanikio, ni lazima ufahamu WEWE ni nani ili uendelee kuwa hivyo au ubadilike.
Mtu halisi ni yule ambaye unakuwa pale unapokuwa peke yako.
Matendo halisi ni yale unayotenda pale ambapo hakuna anayekuona wala hakuna atakayegundua kuhusu ulilofanya.
Huyu ndio wewe halisi.
#jijue
Zoezi (Chukua peni na karatasi uandike na kujibu haya maswali)
1. Je, uko tofauti na watu wanavyokufahamu?
2. Je, unayapenda matendo unayotenda ukiwa peke yako unayojua wengine hawatayafahamu?
3. Je, ni kitu gani unatamani kukibadili?
4. Umewahi kujaribu kubadili ukashindwa? Kwanini?
5. Je, unataka/unatamani uwe vipi?
#Jijue
B. Nimezaliwa nifanye nini?
Katika maisha ya mwanadamu, kila mmoja amezaliwa ili aje afanye jambo fulani kwa ufanisi wote na kuweza kufikia mafanikio makubwa na ya kweli katika jambo hilo.
Kitu cha kusikitisha, ni watu wachache wanaofanikiwa kufahamu ni nini kimewaleta duniani.
Chanzo kikuu cha utajiri wako ni kufahamu nini umekuja kufanya duniani.
Zoezi (Chukua peni na karatasi na ujibu)
1. Je, kitu gani unapendelea sana kukifanya?
2. Je, ukifanya nini, kinakufanya usahau kabisa hata kula?
3. Ulipokuwa mdogo, kutoka moyoni mwako, ulitamani kufanya nini hasa?
4. Watu wanasema unaweza sana kufanya kitu gani?
5. Unahisi umekuja duniani kufanya kitu gani?
#jijue
Photo credit Francis Mtey na Anna Ben Paul
Model: Anna Ben Victus Paul
Fanya haya mazoezi na endelea kutufuata ili uweze kujijua na kujitambua.
#JIJUE #FASDO_GOALS_2016