Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
Kwa sababu ni fani yangu, nimeonelea leo niwashirikishe umuhimu wa mazoezi ya viungo kwa mwili wa binadamu. Naandika haya kwa makusudi kamili nikijua kwamba wengi hasa wa jamii ya waaminio wa ki-Tanzania huona ni kama kupoa kiroho kwa mpendwa kushiriki katika mazoezi ya viungo, kucheza mpira, riadha, kuogelea, na michezo mingineyo inayohusisha mjongeo wa viungo vya mwili (body movements). Biblia inaeleza katika kitabu cha
1Timotheo 4:8 "... Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote..." Huo mstari unaweka bayana kwamba mazoezi yanafaa japo ni kwa kiwango fulani-HAUKATAZI mazoezi ya mwili.Kwa kuonesha kwamba mazoezi ni muhimu na hata wakati fulani kushiriki kwenye mashindano ya michezo, Paul anasisitiza kwa kutolea mfano 1 Wakorintho 9:24-27 "... Je! Hamjui ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja?..." Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote ........" Paul anajiringanisha kama mwanariadha mahali hapo." Anaonesha pia kwamba katika michezo zipo sheria zake na kanuni za kufuata ili kuweza kufikia lengo
(2 Timothy 2:5) . Kana kwamba haitoshi, Paul anaonesha pia hata michezo ya kukabiliana ana kwa ana (combat sports) kwamba nae yupo katika kupiga ngumi na si kama apigaye hewa (2 Timothy 4:7) .
Kwa vielelezo hivyo ni dhahiri kabisa hakuna dhambi ndani yake kwa mtu wa Mungu kushiriki kwenye michezo au mazoezi ya mwili cha msingi ni kuwa na dhamiri na nia njema ya kwa nini unafanya hivyo. Ni agizo la Mungu kwamba hekalu lake litunzwe hii sio kiroho tu hata katika utu wa nje ni muhimu pia (1 Corinthians 6:19-20) .
Efeso 5:29 - yazungumzia juu ya matunzo ya mwili, pia Biblia inakataza ulafi naam hata inafikia hatua ya kusema ujitie kisu kooni kama wewe ni mlafi
Mithali 23:2 , kuwa makini hapa!!! Kwa ujumla twaweza sema biblia inakazia juu ya suala la mtu kuitunza afya ya mwili wake.
Kwa mtazamo huo hapo juu, nikirejea kwenye umuhimu wa michezo au mazoezi ya mwili, ziko faida lukuki ndani yake. Tafiti nyingi zimefanyika na karibu zote zinaonesha mtazamo chanya juu ya umuhimu wa michezo na mazoezi kwa mwili wa mwanadamu. Michezo au mazoezi ya mwili yana faida zifuatazo:
1. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na magonja ya moyo na kifo kutokana na magonja hayo.
2. Hupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la damu
3. Hupunguza mafuta yaliyo hatari kwa mwili wako katika damu (blood cholesterol and triglycerides) na kuachilia yale yaliyo salama tu (HDL - or good cholesterol).
4. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na mgandamizo mkubwa wa damu (HBP) na kushusha kwa wale walio nao tayari (hypertension)
5. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa kisukari (Diabetes mellitus type 2DM)
6. Inapunguza uwezekano wa kupata kansa ya utumbo mpana
7. Husaidia katika kufikia na kutunza kiwango cha uzito maridhawa wa mwili.
8. Hupunguza hisia za mtindio wa mawazo na tashwishwi
9. Huimarisha hali njema ya kisaikolojia na kupunguza hisia za msongo
10. Hujenga na kuimarisha mifupa, viungo na misuli za mwili
11. Hupunguza na ama kuondoa tatizo la unene (Obesity)
12. Kwa wazee huwafanya kuwa imara na uwezo wa kudhibiti miili yao kutokana na kuanguka au kuchoka kwa haraka.
Kwa faida hizo na nyingine nyingi ambazo sijazitaja upo uwezekano kabisa wa mtu wa Mungu kuongeza siku zako za kuishi hapa duniani ambayo kwa hakika ni ahadi ya Mungu, na hakuwa mjinga anaposema "...siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na bwana Mungu wako..." (Kutoka 20:12). Wengi wetu kwa kutokushiriki katika mazoezi japo kidogo tumeiharibu miili yetu na kuwa na vitambi visivyokuwa na sababu na miili ambayo ni goigoi ambayo hata imekua kizingiti kwa kazi ya Mungu. Ni kweli yapo magonjwa lakini si yote ni shetani, mengine ni uzembe wetu tu wenyewe (Hosea 4:6).
Kanisa ambalo kimsingi ni eneo la kuwajenga watu kiimani na kuwasogeza kwa Mungu limesahau na kuiweka nyuma habari ya mafundisho ya mazoezi ya miili kwa washirika wake. Eneo hili likitumika vema, laweza hata kuwa ni eneo la injili ya kuwaleta watu kwa Yesu! Fikiria umeanzisha timu ya mpira iko daraja la kwanza, na slogan au moto wenu unakuwa Yesu Ni Mwokozi kila muingiapo uwanjani, unafikiri ni watu wangapi watakuwa wamefikiwa na ujumbe huu kwa msimu mmoja tu wa ligi? au kanisa likiwa na ukumbi wa kufanyia mazoezi Gymn au likianzisha aerobic fitness centre ni watu wangapi watakuwa wakihudumiwa hapo kwa mazoezi hayo na pia kuipata injili kwani hazitapigwa nyimbo za duniani bali ni nyimbo za kumtukuza Yesu na hata ikibidi kabla na baada ya mazoezi mwaweza weka utaratibu wa kuwa na maombi. Yote haya ni katika kuujenga mwili na ufalme wa Mungu! Yatosha kwa leo!!!!!
Mbarikiwe na Yesu!
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.