Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
Uzinduzi wa Boma la Makumbusho ya Mkoa na Kituo cha Utamaduni
Ofisin ya mkuu wa mkoa wa Iringa Pamoja na Chuo kikuu cha Iringa siku ya tarehe 25/06/2016 kutakuwa na uzinduzi wa Boma la Kihistoria
Kutakuwa na matukio mbalimbali yatakayoambatana na ufunguzi ikiwemo maonesho ya kitamaduni na sherehe rasmi za ufunguzi. Tunawakaribisha wakazi na watanzania wote kuja kusheherekea utamaduni na historia ya nyanda za juu kusini.
Pamoja na maonesho mbalimbali ya kuvutia ikiwemo Historia ya Iringa, Uganga na tiba asili, Hazina na asili ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa, pia kuna jambo la ziada la kujifunza kwa kila mtu.
Tafadhali jiunge nasi na kuona matokeo ya miaka kadhaa ya kazi ya kujitolea ya kulifufua Boma la iringa na kulifanya kuwa alama ya kipekee kusini mwa Tanzania.
Hili ndilo jengo la makumbusho ambalo linaziduliwa leo.
Mgeni Rasmi ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga.
MKUU wa Chuo Kikuu cha Iringa (IUCo), Profesa Joshua Madumulla amesema Nyumba ya Makumbusho ya Mkoa wa iringa itafanya kazi kubwa ya kukusanya na kutunza vitu mbalimbali vya kale.
MKUU wa Chuo Kikuu cha Iringa (IUCo), Profesa Joshua Madumulla
Vitu hivyo vya kisayansi, sanaa na historia vitatoa fursa kwa jamii ya ndani na nje ya nchi kujionea hazina ya urithi uliopo mkoani Iringa. Lina vitu mbali mbali vya zamani vya kihistoria vikiwemo
Mifupa ya Binadamu wa zamani
Vyungu
Pasi ya chuma
Historia fupi ya mke wa Mkwawa
“Uwekezaji katika urithi wa utamaduni hauna budi kupokelewa kama sehemu muhimu ya program itakayosaidia kukuza uchumi wa jamii husika na taifa kwa ujumla,”alisema.
Ukarabati wa nyumba hiyo iliyojengwa takribani miaka 116 iliyopita na utawala wa mjerumani aliyeitumia kama boma lake kuu, umefanywa kupitia mradi wa Kuendeleza Utamaduni Nyanda za Juu Kusini (Fahari Yetu) unaofadhiliwa na umoja wa nchi za Ulaya (EU) kwa zaidi ya Sh Milioni 230.
Jan Küver Meneja wa fahari yetu
Project Manager at fahari yetu - Southern Highlands Culture Solutions
“Fursa ya kulibadili jengo hilo la boma la kihistoria kuwa jumba la makumbusho ni msingi imara wa kukataa hatari ya kuyumbishwa na mabadiliko yasiyoleta tija katika kukuza na kuendeleza tamaduni zetu na utalii wa kiutamaduni nchini,” alisema.
Meneja msaidizi wa mradi huo unaokishirikisha chuo hicho kikuu, Jimson Sanga alisema uzinduzi wa nyumba hiyo utafanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga.
Meneja msaidizi wa mradi huo unaokishirikisha chuo hicho kikuu, Jimson Sanga
Sanga alisema katika hafla hiyo itakayowashirikisha mawaziri wengine na viongozi mbalimbali wa serikali, siasa, mila, utamaduni na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi, utakwenda sambamba na maonesho ya rasilimali za utamaduni na historia ya mkoa wa Iringa.
Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa kibali kwa Chuo Kikuu cha Iringa kulikarabati na kulihuisha jengo lililojengwa na wakoloni wa kijerumani miaka 114 iliyopita maarufu kama Iringa Boma na kuwa jumba la makumbusho.
Jengo hilo ambalo litafanyiwa ukarabati na mradi wa kuendeleza na kukuza utamaduni wa asili kanda ya Nyanda za Juu Kusini unaoitwa Fahari yetu unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Iringa kwa ufadhili wa Jumuiya ya nchi za Ulaya kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita limekuwa likitumika kwa shughuli mbalimbali za Serikali ikiwemo ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa.
Jengo hilo lililojengwa kwa usanifu wa hali juu kwa kutumia mawe, tofali zilizochomwa na tope au udongo na wakoloni wa kijerumani yapata miaka 114 iliyopita limekuwa Makao Makuu ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Iringa kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Kutokana na kuwa na historia ya kuvutia, Serikali kupitia idara ya mambo kale imekuwa na mchakato wa kuligeuza kuwa jumba la makumbusho ambapo baada ya ofisi mpya ya Mkuu wa wilaya ya Iringa iliyogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.8 kukamilika.
Kwa mujibu wa Naibu Mkuu Chuo Kikuu cha Iringa Utawala Dokta Hosea Mpogole, chuo kikuu hicho kupitia mradi wake wa Fahari Yetu wamepata kibali cha kukarabati jengo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu amesema lengo ni kulibadili jengo hilo na kulifanya kuwa jumba la makumbusho kwa kukusanya na kuweka ama kutunza kumbukumbu, kufanya maonesho mbalimbali ya urithi wa utamaduni wa Mkoa huo kwa ajili ya kukuza utalii na kuleta maendeleo endelevu
Jumuiya ya Nchi za Ulaya wametoa zaidi ya shilingi Bilioni 3.2 kuendesha mradi huo wa Fahari Yetu ambao utadumu kwa miaka mitatu.
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.