Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
Na Nukuu Maneno ya Mathias Canal
"Oh Oh NIMEALIKWA KUHUDHURIA KONGAMANO LA NYUMBANI NA DIASPORA ZANZIBAR
Na Canal Mathias
Ndugu zangu..!
Waandaaji wa Tamasha la Nyumbani na Diaspora wamenialika kuwa kijana mshiriki katika Kongamano litakalo wakutanisha zaidi ya watanzania 450 waishio Nje ya nchi yetu Maridhawa.
Hii ni heshima kubwa kwangu na kwa Vijana wengine wa kitanzania kupata mualiko wa kipekee kama Mchambuzi, Mjasiriamali na Mwandishi asiyeteteleka katika taaluma yake.
Kwa dhati kabisa nimepokea mwaliko huu na nipo katika maandalizi ya kushiriki Tamasha hili Muhimu litakalofanyika Zanzibar Beach Resort kuanzia tarehe 24 hadi 25 Agosti ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ally Mohamed Shein anatarajiwa kuchezesha ufunguo ishara ya ufunguzi wa mkutano huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli atachezesha ufunguo wakati wa kufunga Tamasha hili.
Mkutano unatarajiwa kuvutia kwa kuwakutanisha washiriki 450 waishio Nje ya nchi na waliorejea, wadau kutoka sekta ya umma na binafsi pia kama wanachama wa Jamii ambao wamekuwa na mchango Mkubwa katika uhamasishaji wa wanachama wa Diaspora katika kujenga Taifa.
Kauli mbiu ya Mkutano huu ni kukuza Utalii na uwekezaji nchini Tanzania lakini pia kujihusisha na kuhimiza ugenini ili kuwa na Tanzania ya kushiriki katika Biashara ya Utalii kama Njia ya kukuza uwekezaji nchini.
Hii ni fursa Muhimu sana kwangu lakini inanifanya kuwa na uelewa mpana zaidi katika ushiriki na namna mijadala Mkubwa inavyoendeshwa.
Kipekee sasa niwashukuru kila mmoja kwa nafasi yake kwa namna mnavyoniimarisha kuwa bora Leo kuliko Jana.
Safari moja inaanzisha nyingine Asante kwa Mwenyekiti wangu Maggid Mjengwa kwa uratibu mzuri wa Tamasha hili ambalo limezidi hadi idadi tarajiwa tena pasina kutangazwa kwenye vyombo vya habari zaidi mitandaoni ya kijamii pekee."
Naaam, chura hapigwi teke ukijidanganya kumsukuma kwa hasira ujue umeirahisisha safari yake.
Ni Neno La Wakati Mwema
Mathias Canal (Sauti ya Wanyonge)
0756413465
Mwanza Mjini
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.