HURU FESTIVAL.....
IRINGA
Ni Usiku wa Kuwekwa Huru Kwa Vijana Wengii
NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII KUKUKARIBISHA KWENYE MSIMU MPYA WA HURU FESTIVAL IRINGA.
TAMASHA LA IBADA NA SIFA
TAR: 4/11/2016
Mahali: Chuo kikuu RUCU
ONGEA UKWELI NA NAFSI YAKO
Ili ufike hatua ya kutambua kwa namna hii ni lazima uwe ni mtu unaeweza
kusema ukweli na nasfi yako mwenyewe,Kwasababu kuna nyakati ambazo
tumejikuta tunapoteza fulsa za mabadiliko ndani yetu kwasababu ya kitu
kidogo sana ambacho ni kukubali kuiambia ukweli nafsi yako.Ni fikra
ngumu kidogo hii unaweza ukawa unajiuliza kuongea ukweli na nafsi
yangu...!Hii inawezekanaje? Tulia kidogo, vuta pumzi kisha tujifunze
pamoja.
(Yohana 8:32) Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Ukisoma kwa umakini hapo utagundua kabla ya uhuru au kuwekwa huru kuna
hatua ya kwanza ambayo mimi hua naiita wajibu ni kuijua kweli
unawajibika kuitafuta kweli na kuikubali hata kama haikufurahishi sana,
tofauti na ufahamu wa watu wengi sana ulivyojijenga hapa nataka
nikupeleke hatua ya juu zaidi ya kutambua kwamba kabla ya kweli ya nje
kuthibitika ni lazima kwanza kweli hiyo ianze ndani ya nafsi yako ndipo
ije kujithibitisha nje. Japo kuna wakati mwingine pia tumejikuta
tukisema kitu nje lakini ndani yetu hakiua hivo kama jinsi vile
tulivyosema.Sasa hali hiyo ndo inaitwa kutosema kweli na kukubaliana na
nafsi kwasababu kuna wakati dhamira yetu ndani imetushuhudia hasi ila
kwasababu na matakwa binafsi tukajifariji kwamba tuko chanya lakini
chanzo cha taarifa cha ndani ambacho ndicho chanzo kikuu cha kweli yetu
kilitujuza vingine na sisi tunatenda vingine.Kweli hujs kupitia vynzo
mbali mbali na sehemu ya kwanza kuithibitisha kweli hua ni kwenye nafsi
ya mtu binafsi na huna budi kuikubali kweli ya ndani ili isababishe
badiliko.
Muhimu: unaweza ukatakiwa kufanya jukumu flani na mkuu wako au
rafiki au ukasikia jambo Fulani la ushawishi kutoka kwa mtu wako wa
karibu na ukatakiwa kulitolea mawazo yako, kutokana na ukaribu ulionao
na yule mtu ukalazimika kusema ndiyo!Lakini ndani yako umesema hapana au
haukuona haja ya wewe kukubaliana na lile lakini kwa sababu binafsi
umeamua kusema ndio pengine ili kumridhisha mtu,Sasa tendo hili ni tendo
la kuidanganya nafsi yako mwenyewe.Jifunze kusema kweli kama ni ndio
basi ndio yako iwe ni ya ndani na nje na kama ni hapana vivyo hivyo
hapana yako iwe hivyo.
Kwa maneno machache naweza kusema ili uwe huru ni wajibu wako kwanza
kuijua kweli na kupitia hiyo kweli utakua na haki ya kua huru.Kweli ya
ndani(kweli ya nafsi) ni ile hali ambayo mtu unalijua tatizo lako
binafsi na hakuna mtu mwingine wa nje anaeweza kuliona wala kugundua juu
yako , Na unaamua kulifanyia mabadiliko japo kua hakuna mtu
aliekugundua wala kuhisi kitu.Hii ni hatua kubwa sana ambayo itakusaidia
kufanya maamuzi ya kuchagua ni nini chanzo sahihi kitakacho kupelekea
wewe kuijua hii kweli ambayo kwayo utakua huru.Ni mara nyingi sana
tumezidanganya nafsi zetu kua tupo salama kwasababu watu wanaotuzunguka
wametuamini na hakuna matokeo yeyote ya nje yaliyokuthibitisha kwa watu
kua wewe ni mkosaji au hauko salama,lakini moyoni au nafsini mwetu
tukijua kwa hakika hatuko salama. Hali hii kamwe si ya kuinyamazia au
kuendekea kuifumbia macho kwani hii imekua ni sababu kubwa sana kua
kupotoka kwetu kwasababu matokeo yeyote ya nje unayoyaona chanzo chake
kilikua ndani. Na hii sasa ndio maana halisi ya lile andiko tulilosoma
kwamba ‘Ajionavyo mtu nafsini mwake hivyo ndivyo alivyo.Hivyo kusema
ukweli na nafsi yako kutasababisha mabadiliko sana katika maisha yako ,
kwamba ni kweli mimi nina tatizo hili hata kama watu hawajanigundua sasa
je nifanye nini kuondokana na tatizo hili?Hiyo ndio njia na namna ya
kusema ukweli na nafsi yako.
3. UMESIKIA NINI.... TOKA KWA NANI?
Chanzo cha taarifa mara nyingi ndio hua chanzo cha kuakisi na
kukuaminisha kitu fulani ambacho baada ya kukisikia, kuona au kusoma na
kukiamini na kuiweka imani katika matendo baada ya muda fulani wa
mchakato matokeo huja vile vile kama jinsi uliona au kuamini.Inawezekana
wewe ulianza kuuona ukuu ndani yako.... katika biashara, huduma,
masomo, siasa au uongozi, Sasa baada ya kuhisi kitu hicho ndani yako ni
taarifa gani ulioipata juu yako au juu ya ndoto yako? Je chanzo cha hiyo
taarifa yako kilikua sahihi? Ukijizoesha kusikia habari za kushindwa
basi unajijengea matokeo ya kushindwa kwasababu ubongo wako umekaa
tayari kupokea taarifa, kufikiri na kuifanya fikra kua imani na imani
kua katika matendo na kuleta matokeo halisi na kama kushindwa ndio
imekua taarifa yako basi jiandae kushindwa.
Kama jinsi ulivyoona huo mtirirko katika kifani chetu hapo juu hivyo
ndivyo taarifa husafiri na mwisho wake hua ni matokeo ambayo yanaweza
kua mazuri au mabaya, lakini inategemea sana pale mwanzoni ulianza kwa
kupokea taarifa gani! Kama taarifa ilikua ni sahihi basi tegemea matokeo
sahihi ya yenye manufaa, Lakini kama haikua sahihi basi tegemea matokeo
yasio sahihi pia.
Sio kila chanzo cha taarifa ni sahihi kwako, tukutane wiki ijayo ambapo
tutaanza kutazama vyanzo sahihi vya taarifa kwako. Unaweza kuwasiliana
na mwandishi kupitia namba 0653-318117, ama kwa barua pepe
fredymsungu@gmail.com.