TAARIFA KUHUSU KAMPENI YA ABIRIA PAZA SAUTI NA WAJIBU WA KILA BALOZI KUSHIRIKI KATIKA KAMPENI HIYO.*
*UTANGULIZI*
Kampeni ya ABIRIA PAZA SAUTI inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na mhe.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni
Naibu
Waziri wa Mambo ya ndani mhe. Hamadi Masauni,
siku ya Jumamosi tarehe
*5/11/2016*
katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo(UBT).
Kabla ya uzinduzi
kutakuwa na Press Conference itakayofanyika katika Ukumbi wa habari
maelezo katika
tarehe mtakayotangaziwa.
*WADAU WA KAMPENI.*
Kampeni hii itawahusisha wadau wote muhimu yaani SUMATRA, SUMATRA CCC,
MAKINI APP, CHAKUA, UWAMATA, FIRE, TRAFIKI POLISI,TABOA NA RSA. Na
wengine watakaoongezeka baadae.
*SIKU ZA KAMPENI*
Kampeni hii itakuwa inafanyika siku zote kwa kasi mpya kunzia mwezi novemba hadi January-kwa awamu ya kwanza.
Kwakuwa mabalozi wengi wanakuwa kazini basi siku rasmi za kampeni ya
pamoja zitakuwa kila wiki Jumamosi na Jumapili. Hiyo ndiyo ibada yetu.
Siku za katikati ya wiki balozi mmoja mmoja au wawili watatu wanaweza
kushiriki. Lakini pia wenzetu wa jeshi la Polisi na SUMATRA watacover
siku hizo kwakuwa majukumu yao yapo barabarani kila siku.
*USHIRIKI WA MABALOZI*
Tunataka mabalozi wote washiriki kwa vitendo katika kampeni ya
pamoja(group campaigns) kwa siku za wikiendi. Na kwa yule atakayeshindwa
kushiriki kwa vitendo physically basi walau atoe mchango wa vipeperushi
au wa fedha au usafiri angalau kuwawezesha mabalozi watakaokuwa field
walau kupata maji ya kunywa.
*KITAKACHOFANYIKA WAKATI WA KAMPENI*
Wakati ya kampeni mabalozi watafika katika vituo vya mabasi na kwa
kushirikiana na jeshi la polisi na SUMATRA watapanda mabasi yanayoelekea
mikoani. Ndani ya mabasi mabalozi watatoa elimu kwa abiria kuhusu haki
zao mbalimbali, wajibu wao, bima, umuhimu wa kufunga mikanda, kutunza
usafi ndani ya basi, na kuwapa namba za kutolea taarifa kunapojitokeza
lolote. Watawaelekeza abiria namna ya kufunga mikanda na hatimaye
kuwagawia vipeperushi.
Baada ya kuteremka watakutana wote pamoja
wataelemisha makundi ya bodaboda madereva wa malori nk. Na hatimaye
watageuza kurudi walikotoka.
Sambamba na upandaji wa mabus kutakuwa na kampeni kupitia redio,tv, mabango pamoja na mtandaoni.
Madereva 100 waliochaguliwa pale ubungo watashiriki moja kwa moja
kuelimisha na kuendesha kwa usalama magari kila siku watakapokuwa
wanaanza safari na wakati wa safari. Aidha baada ya kampeni kufungwa
kutakuwa na siku ya tuzo kwa madereva bora watakaopatikana, ambapo
zawadi mbalimbali zitatolewa.
*LENGO LA KAMPENI* ni kuhakikisha
wananchi wanashiriki kikamilifu katika juhudi za kudhibiti ajali za
barabarani na kuwafa ya watambue haki na wajibu wao wawapo kwenye vyombo
vya usafiri.
HIVYO tunaomba sana ushiriki wenu wa dhati katika
kampeni hii. Na kila balozi ashiriki kusambaza ujumbe wa kampeni ya
abiria paza sauti kila tunapoutoa ili elimu iwafikie watu wengi zaidi.
Asanteni sana
RSAadmin1
ABIRIA PAZA SAUTI IMEKWISHAANZA. NI KAMPENI YA MIEZI MITATU MFULULIZO YA
KUWAKUMBUSHA ABIRIA WA VYOMBO VYA MOTO KUTIMIZA WAJIBU WAO WA KUCHUKUA
TAHADHARI KUEPUKA AJALI BILA KUTEGEMEA ASKARI.
KILA BALOZI WAKATI
HUU POPOTE PALE ALIPO KUANZIA NYUMBANI KWAKE, KAZINI KWAKE, MTAANI
KWAKE, KWENYE VYOMBIO VYA USAFIRI, NK ANATAKIWA KUENEZA UJUMBE WA ABIRIA
PAZA SAUTI.
"HATUTAKI AJALI, TUNATAKA KUISHI"