Ø Lengo ni kuwa endapo
ibilisi atakuwa amepanda kitu cha kwake
au mataifa wamekunasa na vitu ambavyo si kusudi la Mungu kwako na wewe kufikiri
ndio Mungu anataka, vitu ivyo vibatilishwe na nguvu ya Mungu. Zab 33:10 anasema “BWANA huyabatilisha mashauri ya mataifa huyatangua makusedi ya watu”
mstari wa 11 anasema “Shauri la BWANA
lasimama milele, makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi” hivyo maombi
yatabatilisha makusudi ya watu.
Ø Unapoomba endapo
ulikuwa umenaswa katika hali ya udanyanyifu na moyo wako kudhania kuwa hivyo
ndivyo ulivyopaswa kwenda nguvu ya maombi hutangua mipango ya udanyanyifu na
kutembea kwenye kusudi hasa uliloitiwa, Ayubu
5:12 anasema “Yeye huyatangua
mashauri ya wadangenyifu, mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao”
Ø Unapojikabidhi kwa
Mungu na mipango yako anakusaidia kutembea kwenye kusudi lake Mith 16:3 anasema “Mkabidhi Bwana kazi zako na mawazo yako yatadhibitika” ukisoma
Biblia ya kingereza tafsiri ya Good News anasema “Ask the LORD to bless your plans and you will be successful in carring
them out” akiwa na maana muombe Mungu abariki mikono yako ili ifanikiwe,
hivyo basi ni vema ukaelewa kuwa bila Mungu kukuwezesha huwa haiwezekani
kufanikiwa kutembea kwenye kusudi lake ndio sababu ukisoma Mith 16:9 utakuta anasema “Moyo
wa mtu huifikiri njia yake; bali Bwana huziongoza hatua zake” Ikiwa na
maana unaweza ukafikiri ukawana maono na usiongozwe na Bwana lakini pia unaweza
ukafikiri ukaomba ukawana maono na ukaongozwa na Bwana.
Ø Maombi hufungua macho
husaidia kupata ufahamu na unapokaa kwenye maono ni rahisi kujua ni nini hasa
wito wako, kusudi la Mungu kukuitwa hapo na hata amani tumaini kutawaka moyoni
mwako, ukisoma Efeso 1:18 anasema “Mcho ya mioyo yenu yatiwe nuru mjue tumaini
la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika
watakatifu jinsi ulivyo………”
Ø Maombi humpa nafasi
roho mtakatifu kukusaidia wewe kuwa na uhakika wa mahali ulipo na kitu
unachokifanya, ndio sababu kama uka njia panda huelewi cha kufanya huna amani
usihangaike na hiyo hali isipokuwa ingia kwenye maombi Filipi 4:6 anasema “Msijisumbue
kwa neno lolote; bali katika kila neon kwa kusali na kuomba, pamoja na
kushukuru, haja zenu zijulikane na Mungu” Matokeo ya maombi itakuwa ni
Amani na Mungu kukusaidia kukaa mahali sahihi na kwenye lengo sahihi,
ukiendelea anasema
“Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote,itawaifadhi mioyo yenu na
nia zenu katika Kristo Yesu”
Ø Maombi hutusaidia kushinda vikwazo
na majaribu mbali mbali maana inawezekana kabisa mahali ulipo ni sahihi
isipokuwa unahitaji kuomba ili kuwa na uhakika pia kushinda vikwazo mbali mbali
Math 26:41 anasema “ Kesheni, muombe, msije mkaingia
majaribuni……” katika kiingereza tafsiri ya Good News ni nzuri zaidi anasema
“Keep watch and pray that you will not
fall into temptation” hii ukitafsiri katika Kiswahili ana maana kuweni
waangalifu msije mkaangukia majaribuni ikiwasisitiza kuomba wasije wakashindwa
majaribu yatakayokuja kwa hiyo maombi yanakusaidia kuwa na nguvu ya kutosha
kukabiliana na vikwazo hasa unapokuwa unalitimiza kusudi.
Ø Maombi yatakusaidia kujua fikra na
mipango ya adui katika kukuzuia usilifikie lile ambalo Mungu amelikusudia,
maana unaweza ukawa mahali sahihi lakini usiweze kulifikia lile
lililokusudiwa ukisoma 2Korintho 2:11 anasema “Shetani asije akapata kukushinda; kwa
maana hatukosi kuzijua fikra zake” Hivyo maombi ni taa na macho ya
kukusaidia kuiona na kuitambua mipango ya adui ili asije akatushinda.
Ø Maombi hutisaidia kushinda mitego
mbali mbali ya mwovu, mara nyingi utakapotembea kwenye kusudi, ibilisi
atakupiga maana anajua unaujenga ufalme wa Mungu na hivyo kutakuwa na mitego
mbali mbali ya adui kukutoa katika kulitimiza kusudi la Mungu ukisoma Zab 91:3 anasema “Maana yeye atakuokoa na mitego ya mwindaji………” hivyo basi kuna
umuhimu wa kujipanga kwenye maombi has unapojua lipo kusudi unalitimiza.
Ø Maombi yatakusaidia kufanya maamuzi
sahihi ili uweze kulitimiza kusudi la Mungu, unapohitaji kujua nini ufanye,
wapi ni sahihi kwako, yupi atakuwa ni mume sahihi kwako, mke sahihi haya na
mengine mengi ni mambo yanayohitaji kufanya maamuzi sahihi nje ya hapo
hutafanikiwa katika kulitimiza kusudi la Mungu alilokuitia hebu tujifunze kwa
Bwana Yesu, unaposoma Luka 6:12
anasema “Ikawa siku zile aliondoka
akaenda mlimani ili kuomba, (Huyu ni Bwana Yesu) akasesha usiku kucha katika
kumwomba Mungu hata ilipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na
wawili miongoni mwao, ambao aliwaita mitume” kumbe ili kufanya maamuzi
sahihi unahitaji muda wa kutosha kumwomba Mungu Bwana Yesu alikesha usiku kucha
akimwomba Mungu ili asikosee katika kuchagua, wewe je! utahitaji muda gani?
Ø Maombi yatakusaidia kuendelea kukua
na kuishi katika hali ya hekima na maarifa na ufahamu wa kimungu ili
kuendelea kuujenga ufalme wa Mungu ukisoma Kolosai
1:9 anasema “Kwa sababu hiyo sisi
nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili
yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa
rohoni” kumbe ni maombi yanayoweza kumjaza mtu maarifa, hekima na ufahamu
wa rohoni.
Maombi yatakusaidia kuendelea
kuishi kwa Imani pasipo kusitasita, Ebrania
10:38 anasema “Lakini mwenye haki
wangu ataishi kwa Imani nae akisitasita roho yangu haina furaha nae”
Ø maombi huuwa matendo ya mwili
(tamaa mbaya, uadui, fitina na mengineyo mengi) ukisoma Rumi 8:10 anasema “Na Kristo
akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu I hai
kwa sababu ya haki” na ukisoma katika Galatia
5:24 anasema “Na hao walio wa Kristo
Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake”
Unausulubishaje ni kwa maombi na kuutafuta uso wa Mungu.
Ø Maombi yatakusaidia kupata ufunuo
Ukisoma Ufunuo 2:9 anasema “ Lakini kama ilivyoandikwa mambo ambayo
jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,
mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa
roho” Sisi ambao tumelibeba kusudi lake.
Ø Maombi yatakusaidia katika udhaifu
alio nao, mapungufu yako, ukisoma Rumi
8:26 anasema “ Kadhalika roho nae
hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi ipasavyo; lakini roho
mwenyewe hutuombea kwa kuugua tusikoweza kutamkwa” Neno udhaifu kwenye
tafsiri ya kingereza limeandikwa
Weakness yaani Mapungufu, hivyo
usipokuwa muombaji hakuna namna unaweza kupona na mapungufu ulionayo, unapoomba
kwa muda wa kutosha unatoa nafasi ya roho
mtakatifu kukusaidia, maana ibilisi anaweza kutumia mapungufu ulionayo
kukuvuruga.
Ø Maombi yatakusaidia kuitunza nafasi
yako 1Timoth 5:6 “Basi yeye asiyeizuia nafsi yake amekufa
ingawa yu hai” ukisoma Tito 1:8
anasema “Bali awe mkaribishaji, (huyu
mtumishi aliyebeba kusudi la Mungu) mpenda wema mwenye kiasi, mwenye haki,
mtakatifu, mwenye kuidhibiti nafsi yake” kumbuka utatakiwa kudhibiti nafsi
yako maana kuna wakati nafsi itakutaka uishi kwa kufuata tama za mwili na zile
za duniani, sasa ni maombi peke yake yatakayoweza kukusaidia kuidhibiti na si
vinginevyo.
Ø Usiache kuombea kutimilika kwa
kusudi la mungu kwenye maisha yako yaani kuufikia mwisho mwema, Mtume Paulo
alifanikiwa kulijua kusudi la Mungu
kwenye maisha yake na hatimaye kuufikia mwisho mwema. 2 Timoth 4:7 anasema “Nimevipiga
vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda…” ni maombi yangu
kuwa uje useme maneno kama haya utakapokuwa ukimaliza wito wako.
Daudi pia alilitimiza kusudi la
Mungu vizuri maishani mwake na kuufikia mwisho mwema unaposoma Matendo 13:36 anasema “Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia
shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala (Ahaa! kumbe ukulitimiza kusudi la
Mungu haufi isipokuwa unalala maana kuna siku utaamshwa) akawekwa pamoja na
Baba zake….”
MAMBO
YA KUFAHAMU KUHUSIANA NA KUSUDI LA MUNGU
Ø Ukiishi nje ya mpango wa Mungu kuna
Baraka hutaweza kuziona maishani mwako.
Ø Ukiishi nje ya mpango wa Mungu kuna
hatari ya kuishia kwenda jehanamu.
Ø Ukiishi kwenye mpango wa Mungu ni
mtaji wako wa kuurithi uzima wa milele.
Ø Mungu alituumba ili tumzalie
matunda na si vinginevyo.
Ø Hakuna aliyeumbwa bila kitu/kipawa
unatakiwa tu kuomba ili ujue namna ya kufanya.
Ø Unapomtumikia Mungu anakuheshimu.
Ø Wanaoishi sawa na mpango wa Mungu
wanapata upendeleo kwa Bwana.
Ø Kuishi sawa sawa na mpango wa Mungu
unakuwa ni mtenda kazi pamoja na Kristo.
Ø Kuishi nje ya kusudi unaweza
kusababisha ghadhabu ya Mungu kwenye maisha yako maana alikuleta kwa kazi
maalum.
MASWALI
AMBAYO UNATAKIWA KUJIULIZA
i.
Niliubwa
kwa ajili ya nini? Na je nalitimiza lengo la Mungu kuniumba?
ii.
Ni
nini lengo kuu la Mungu kuniweka hai leo?
iii.
Je
ninaishi kwa faida ya Mungu? Au ya Ibilisi?
iv.
Mungu
anataka nini kwenye maisha yangu?
v.
Je
maisha yangu yana mchango wowote katika jamii katika kuujenga Ufalme wa Mungu?
vi.
Je
ninafanyika Baraka mbele za Mungu na watu wanaonizunguka?
vii.
Ni kitu gani kinaniongoza kwenye maisha yangu?
viii.
Je! maisha yangu yanawaidia wengine kupata tumaini katika wito
walioitiwa?
ix.
Je!
ni kitu gani kinachonizuia kuishi sawa na mpango wa Mungu?
x.
Je!
ninamruhusu Mungu kunitumia au namzuia kwa jinsi nilivyo?
xi.
Je! nina muda wa kutosha kutafakari mwisho wangu?
xii.
Je! nina sifa za kutumiwa na Kristo! kama chombo chenye heshima?
xiii.
Je! ni vitu gani vinaweza kuchochea zaidi wito ulioko ndani
yangu?
xiv.
Na Je! ni vitu gani vinaweza kuharibu wito nilionao?
xv.
Je!
nimejitoa kwa Mungu kwa jinsi anavyotaka?
xvi.
Naweza
kuwa nasonga mbele! nimesimama au narudi nyuma katika kuutimiza wito
nilioitiwa?
xvii.
Na
je! hivi nilivyo ndivyo Mungu anavyotaka niwe?
Unapopata nafasi ya kujihoji namna
hii itakusaidia kujipanga na Mungu kwa mfamo ambao utakusaidia kusonga mbele
ili kulitumikia kusudi lake alilotuitia.
Mwl. Tuntufye A. Mwakyembe
Tuntufyemwakyembe@yahoo.com