INATANGAZA NAFASI ZA KAZI ZIFUATAZO
1.
MENEJA (Nafasi
Mbili)
a.
Sifa
·
Awe
tayari kufanya kazi hiyo katika kituo cha Njombe, Iringa au mahali pengine
atakapopangiwa na mwajiri
·
Awe
na shahada katika fani ya Uongozi, Utawala au Rasilimali Watu pamoja na elimu
ya Biashara na Fedha
·
Awe
na umri wa kati ya miaka 25 na 45, mwenye uzoefu wa kazi wa zaidi ya miaka
miwili katika taasisi inayotambulika
·
Awe
ni mbunifu, mpana katika uelewa wa masuala ya utawala na biashara, mchapa kazi
na anayeweza kujisimamia
·
Awe
na ufahamu wa kutosha kuhusu taratibu za uendeshaji wa makampuni
·
Awe
na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na mifumo ya fedha katika kompyuta
(Accounting packages)
·
Awe
na uwezo wa usuluhishi (reconciliation attitude)
b. Majukumu
·
Kumsaidia
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni kutekeleza majukumu ya kila siku ya kampuni
·
Kumshauri
Mkurugenzi Mkuu kuhusu masuala yote yanayohusu wafanyakazi kwa upande wa
utendaji kazi, maslahi na mahusiano kazini
·
Kusimamia
na kuongoza shughuli zote za kampuni na kuhakikisha zinakwenda na kuendeshwa ipasavyo
·
Kuendeleza
na kutekeleza mipango yote ya kampuni kwa kushirikiana na idara zake zote
·
Kutoa
msaada wa kiutawala kwa kazi zote za kampuni na kuchukua hatua sahihi za
kuboresha utendaji wa jumla wa kampuni
·
Kulinda
mikataba na kusimamia mahusiano baina ya kampuni na wateja; na kusimamia
utekelezaji wa majukumu ya watumishi wengine wote
·
Kuwasiliana
na washauri na wakandarasi walioteuliwa na kampuni
·
Kuwasiliana
na serikali na mamlaka zingine za kisheria
·
Kuandaa
mipango kazi, ratiba za miradi, makadirio ya matumizi ya rasilimali na ripoti
za utekelezaji wa miradi
·
Kufanya
mikutano ya mradi, uchambuzi na ufuatiliaji
·
Kuwasiliana
na vyombo na taasisi za fedha kuhusu usalama na usahihi wa rekodi za fedha za
kampuni
·
Atakuwa
msemaji wa kampuni akimsaidia Mkurugenzi Mkuu
·
Atawajibika
kwa Mkurugenzi Mkuu na kufanya kazi yoyote ya kampuni kwa maelekezo ya kiongozi
huyo
2.
MHASIBU MKUU
(Nafasi mbili)
a.
Sifa
·
Awe
tayari kufanya kazi katika mkoa wa Iringa , Njombe au katika kituo chochote
atakachopangiwa na mwajiri.
·
Awe
na shahada katika masomo ya uhasibu kutoka katika chuo chochote
kinachotambuliwa na amesajiliwa na mamlaka za kisheria
·
Awe
na ufahamu wa kutosha kuhusu taratibu, kanuni na sheria za makampuni
·
Awe
na uzoefu ama uelewa wa kinadharia wa kukokotoa mizania ya mirejesho ya kodi za
makampuni kwa mujibu wa kanuni na taratibu za TRA
·
Awe
na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na mifumo ya fedha katika kompyuta
(Accounting packages)
·
Awe
mbunifu, mwaminifu, anayejituma na anayeweza kujisimamia mwenyewe
·
Awe
na uzoefu wa kazi hii wa kipindi kisichopungua miaka miwili
·
Awe
na umri wa kati ya miaka 25 na 45
b. Majukumu
·
Ndiye
atakayehidhinisha hati za malipo kwa maelekezo na kwa kuzingatia taratibu za
kampuni
·
Ataandaa
taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi
·
Atasimamia
wahasibu wasaidizi katika kazi zao za kila siku
·
Atasimamia
shughuli za uhasibu kwenye kitengo cha Idara
·
Ataandika
taarifa ya maduhuli
·
Kutayarisha
ripoti maalumu ya fedha kwa kukusanya, kuchambua na kufupisha maelezo ya
akaunti
·
Awe
na uwezo wa kukokotoa mizania ya mirejesho ya kodi za makampuni kwa mujibu wa
kanuni na taratibu za TRA
·
Atahakikisha
malipo kwa wafanyakazi na vyama vingine yanafanywa kwa kuzingatia sheria,
kanuni na taratibu kwa kufuata miongozo na sera ya kampuni
·
Atachambua
mwenendo wa mapato na matumizi ya kampuni na kupendekeza viwango vya bajeti
vinavyokwenda sambamba na udhibiti wa matumizi
·
Kufanya
kazi nyingine zozote kwa maelekezo ya manejimenti
3.
MHASIBU MSAIDIZI
(Nafasi mbili)
a.
Sifa
·
Awe
tayari kufanya kazi ama katika mkoa wa Iringa, Njombe au katika kituo chochote
atakachopangiwa na mwajiri
·
Awe
na stashahada (diploma) katika masomo ya uhasibu
·
Awe
na ufahamu wa kutosha kuhusu utaratibu, kanuni na sheria za makampuni
·
Awe
mbunifu, mwaminifu, anayejituma na anayeweza kujisimamia mwenyewe
·
Awe
na umri wa kati ya miaka 25 na 45 na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili
·
Awe
na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na mifumo ya fedha katika kompyuta
(Accounting packages)
b. Majukumu
·
Awe
na uwezo wa kupokea na kulipa fedha
·
Ajue
namna ya kutunza daftari la fedha
·
Ajue
kufanya usuluhishi wa hesabu za benki
·
Ajue
kukagua hati za malipo
·
Ajue
kupitisha malipo kulingana na kanuni za fedha
·
Ajue
namna ya kusimamia kazi za wasaidizi wa hesabu
·
Atakuwa
msaidizi wa mhasibu mkuu
4.
AFISA UGAVI
a.
Sifa
·
Awe
na shahada au stashahada ya juu katika fani ya manunuzi na ugavi (materials
management) kutoka katika chuo kinachotambuliwa na serikali
·
Awe
na cheti cha CPSP na awe amesajiliwa na PSPTB na uzoefu wa kazi usiopungua
miaka miwili
·
Awe
na umri wa kati ya miaka 25 na 45
·
Awe
na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na mifumo ya fedha katika kompyuta
(Accounting packages)
·
Awe
na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili
b. Majukumu
·
Atatakiwa
kutambua mahitaji ya bidhaa na huduma mbalimbali za kampuni na kufanya manunuzi
kwa wakati muafaka na kwa gharama nafuu kwa kuzingatia sheria ya manunuzi na
kanuni zake
·
Kuwashauri
viongozi wa kampuni kuhusu kanuni na taratibu sahihi za kufuata wakati wa
kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma kwa ajili ya kampuni
·
Kwa
kusaidiana na viongozi wa kampuni kuweka kumbukumbu ya vifaa vilivyo chakaa,
ambavyo havijachakaa na thamani yake
·
Kuandaa
makabrasha ya tenda, na kupokea na kuwasilisha tenda
·
Kuhakikisha
nyaraka zote za ununuzi na uuzaji zinapatikana na kujazwa vizuri kwa kuzingatia
sheria na kanuni za ununuzi
·
Kuhakikisha
kwamba nyaraka zote za ununuzi na uuzaji zinatunzwa vizuri kwa ajili ya
kumbukumbu pale zinapohitajika
·
Atafanya
kazi nyingine zozote kwa maelekezo ya manejimenti
5.
AFISA KUMBUKUMBU
(nafasi mbili Njombe na Iringa)
a.
Sifa
·
Awe
na shahada ya kwanza katika fani ya utunzaji na uhifadhi wa kumbukumbu (records
managements & archives) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali
·
Awe
na umri wa kati ya miaka 25 na 45
·
Awe
na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili
·
Awe
na ujuzi wa kutumia kompyuta na mifumo yake ya uhifadhi wa kumbukumbu
b. Majukumu ya kazi
·
Kudhibiti
mifumo ya kumbukumbu, kutunza na kusimamia matumizi ya kumbukumbu za kampuni
·
Kutambua
na kutafuta kumbukumbu katika masijala za kampuni
·
Kudhibiti
mfumo wa kumbukumbu zinazozalishwa na kompyuta, na kutunza na kusimamia
matumizi yake.
·
Kufanya
kazi nyingine atakayopangiwa.
Mwisho wa kupokea
maombi ya kazi hizi ni Desemba 31, 2016
Maombi yote
yatumwe kwa njia ya Posta kwa
Mkurugenzi Mkuu,
Boimanda Modern Construction
Company Ltd,
S.L.P 1491,
Iringa.