Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
WAHANGA WAKIWASILI SALAMA
|
BABU MMOJA MIONGONI MWA WA WAHANGA WA MAFURIKO
|
MKUU WA WILAYA YA IRINGA MHE. RICHARD KASESELA KATIKA
MAAFA YA PAWAGA
|
MAKADA WA VYUO WAKIWAPA POLE WAHANGA WA MAFURIKO |
|
Makada wa Shirikisho la vyuo vikuu mkoani iringa wakisaidia kutoa baadhi ya misaada kwa ajili ya wahanga |
BAADHI YA MISADAA IKITOLEWA NA KUPOKELEWA NA DIWANI WA KATA YA ITUNUNDU Mhe,ALDO MFINDE |
|
DIWANI WA KATA YA ITUNUNDU Mhe,ALDO MFINDE AKIPOKEA MSAADA WA VITU PICHANI MAKADA WA SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU MKOANI IRINGA
Misaada
hiyo imetolewa na wadau mbalimbali kutokana na mafuriko ambayo
yalibomoa nyumba 82 katika kitongoji cha Kilala, kijiji cha Kisanga na
kuwaacha wananchi wake bila makazi.
Waziri Mkuu aliwashukuru wadau wote waliojitolea kuwachangia
watu waliopata maafa kutokana na mafuriko hayo.
Wadau waliotoa misaada hiyo ni Benki ya NMB mabati 500, mifuko ya saruji 500, kilo 820 za maharage, kilo 750 za unga wa mahindi na lita 250 za mafuta ya kupikia vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 20/-. Wengine ni Mfuko wa Pensheni wa PPF uliotoa mabati 200 na mifuko ya saruji 200 vyenye thamani ya sh. milioni 6.6/-. Wengine ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) waliotoa mabati 200 na mifuko ya saruji 160 vyenye thamani ya sh. milioni 4.5/-; Kiwanda cha kusindika nyanya cha RedGold kimetoa mifuko ya saruji 100 na mabati 50 vyenye thamani ya sh. Milioni 3/-; mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya CHADEMA, Bi. Susan Chogisasa na wenzake wametoa mabati 150, mifuko 23 ya saruji, kilo 100 za maharage, kilo 50 za chumvi na nguo mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 1.3/-. Madiwani wa Iringa Vijijini walitoa sh. 380,000/-, Wabunge wa Viti Maalum kupitia CCM walitoa vifaa vya sh. Milioni 1.7/-; ofisi ya CCM Mkoa wametoa vifaa vya sh. milioni 6.1/-, Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Bw. Salim Abri aliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Iringa sh. milioni 5/- ili wanunue vyakula vya waliopatwa na maafa. Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mbunge wa Isimani, Bw. William Lukuvi alitoa fedha taslim sh. milioni 20/- kati ya hizo sh. milioni 15 zikiwa ni zake na milioni 5/- ni za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bw. George Simbachawene. Pia alikabidhi seti 251 za mashuka zenye thamani ya sh. milioni 4/- zikiwa ni mchango kutoka Benki ya CRDB. Waziri Lukuvi ambaye alishatoa mabati 250, aliahidi kuongeza mabati mengine 250 (yote yana thamani ya sh. milioni 8), pia alikabidhi sh. milioni 1.5/- kwa diwani wa Mlenge ili ziwasaidie kukodi gari la kukarabati barabara yao ambayo imeharibika sana kutokana na mafuriko hayo.
Mapema,
akitoa taarifa ya maafa kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi.
Amina Masenza alisema jumla ya kaya 82 zilikosa makazi kutokana na mvua
zilizonyesha Februari 12 na kusababisha mafuriko. Kabla ya hapo, kaya
nyingine 75 zenye wakazi 377ziliathirika kutokana na mvua zilizoanza
Februari 3, mwaka huu.
Alisema
miundombinu ya barabara na ya maji safi iliharibiwa vibaya na
kusababisha hasara ya zaidi ya sh, milioni 250/-. Pia wakazi hao
walikubwa na uginjwa wa kipindupindu kutokana na mto Mapogoro kufurika
na kusomba baadhi ya vyoo vya wakazi hao.
|
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.