MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

Goo

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Friday, December 9, 2016

MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA

RAIS MAGUFULI KUENDELEZA JITIHADA ZA MARAIS WALIOPITA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI.

mako4
Rais John Magufuli akiwapungia wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam wakati alipoingia kwenye uwanja huo kuongoza sherehe  za miaka 55 ya Uhuru Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mako5
Rais John Magufuli akikagua gwaride katika sherehe za miaka 55 ya uhuru kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mako2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika sherehe za miaka 55 ya uhuru kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mako3 mako4
Makamu wa Rais, Samia Suluhu akisalimiana na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuhudhuria sherehe za miaka 55 ya Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
mako6
Rais Joh Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuongoza sherehe za miaka 55 ya Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mako7 mako8
Makomando wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakionyesha  uwezo wao wa kukabiliana na adui bila kutumia silaha za moto katika  maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mako1

……………………………………………………………………..
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO-Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza jitihada zilizoachwa na Serikali za awamu zilizopita   ili kuzidi kuwaletea maendeleo Watanzania.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara yaliyofanyika katika uwanja wa uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeanza jitihada za kuboresha huduma za maendeleo ya jamii, ambapo katika bajeti ya mwaka 2016/17 imeamua kutenga asilimia 40 ya bajeti  katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo umeme, miundombinu, afya, elimu.
“Mbali na kujiwekea vipaumbele mbalimbali kwa maendeleo ya nchi, kumekuwa na changamoto kadha wa kadha zinazozikabili nchi ikiwemo ufisadi, rushwa ndani ya baadhi ya watendaji” alisema Rais Magfuli
Aidha Rais Magufuli alisema juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ni kuboresha maslahi kwa watanzania kwa kuchukua hatua mbalimbali za kuwawajibisha wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi.
Akifafanua zaidi Rais Magufuli aliwataka watanzania kudumisha amani na kulinda muungano uliyopo kwani amani ni msingi wa maendeleo ya nchi bila amani hakuna maendeleo.
Rais Magufuli pia alitoa wito kwa wantanzania kuendelea kufanya kazi kiwa bidii kwani kila mwananchi ana haki ya kufanya kazi, na kusema kuwa waasisi wa nchi walileta uhuru kwa maendeleo ya nchi kwani Uhuru ni kazi.
“Serikali ya Tanzania imejipanga kufanya kazi, tutafanya kazi kwelikweli, watendaji niliowachagua wanafanya kazi hivyo watanzania kwa ujumla mnatakiwa kuonesha ushirikiano kwao kwa maendeleo ya nchi yetu” alisema Rais Magufuli.
Mbali na hayo Rais Magufuli alisema kuwa ndani ya miaka 55 ya Uhuru Tanzania imepata mafanikio makubwa ambapo Tanzania imelinda Uhuru wa nchi, sambamba na kulinda mipaka iliyopo.