|
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mh. Richard
Kasesela akizungumza kwenye kongamano la Fursa 2016 kwa vijana
liliyofanyika jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Mtana, Millenium
Towers. | | |
Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Alvaro
Rodriguez amewahamasisha vijana mbalimbali kujitokeza kwa wingi
kuchangamkia fursa zilizopo katika malengo endelevu ya Dunia
ilikuwezeshwa kimafunzo na mitaji zaidi.
|
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Alvaro Rodriguez akitoa elimu
kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana walioshiriki
kongamano la Fursa 2016 jijini Dar. |
Akizungumza katika semina maalum ya FURSA 2016 kwa mkoa wa Dar es
Salaam iliyoandaliwa na Clouds Media kwa kushirikiana na Umoja wa
Mataifa (UN) na wadau wengine mbalimbali huku wananchi kutoka maeneo
tofauti wamepata kuhudhuria, Bw. Alvaro amesema vijana na wananchi
wanayo fursa ya kuchangamkia malengo hayo ya endelevu.
“Tumeweza kuzunguka maeneo mbalimbali ya Tanzania kuwafundisha vijana
kuwa mabalozi wa malengo endelevu ya Dunia. Na zaidi ya vijana 10,000
kwa kufikiwa na elimu ya maendeleo endelevu. Ikiwemo Iringa, Kigoma
Mbeya na mikoa mingine” amesema Bw. Alvaro.
Aidha kwa upande wa washiriki wengine wakiwemo watoa mada wameweza
kutoa shuhuda mbalimbali za mafanikio na namna ya kupata elimu ya
kibiashara.
"Asanteni sana kwa kuja hapa kwa niaba ya mashirika ya umoja wa mataifa huu ni mkoa wa mwisho, tumefurahi kuona
#Fursa2016
inavyowafikia Vijana tuna amini vijana wanaweza kumaliza matatizo ya
vita, kujenga uchumi kuleta usawa wa kijinsia pamoja na kutunza
mazingira. @ALVARO_UNTZl
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela akitupa madini na fursa zinazopatikana Mkoa wa Iringa.
"Mimi ni moja ya Ma-DC tajiri na mkiwaona Ma-DC unaona namna gani
lakini tupo vuri, mimi nilitumia nafasi vizuri wakati wetu na niliwahi
kubeba spika za
#Clouds
ili nipate kuingia bure kwenye muziki, enzi hizo @Josephkusaga ni DJ
ndipo Ruge Mutahaba alipokuja na wazo la Radio, ila mimi no Kati ya watu
nilikuwa sikuona kama fursa.
Vijana Watanzania fursa sio hela ni mtaji na aj
ira
kila unachokiona mbele yako ni fursa kwa sababu bahati ipo kila mahali,
unapoamka unapomwangalia mke wako hiyo ni opportunity, unapoana
changanoto kwa wenzako hizo ni opportunity unatakiwa kuzitumia ili
ujiongezee kipato na maendeleo." Richard Kasesela
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mh. Richard Kasesela (mbele) wakiingia kwenye mkutano huo wa Fursa 2016
Msanii Mrisho Mpoto akiingia ndani wakati wa tukio hilo la FURSA 2016
Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Alvaro
Rodriguez akiingia ndani ya ukumbi wakati wa tukio hilo la FURSA 2016
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia tukio hilo
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya MaxMalipo, Injinia Juma Rajab akitoa elimu kwa washiriki.
Mwanamuziki Nick wa Pili akizungumza na vijana wenzake kwenye Fursa 2016 jijini Dar es Salaam.
"*Maarifa ya kwanza ya kijana kuwa Muasi lazima ujikane kwa sababu utatumika kwa kile unachofanya.
*Kutengeneza Utamaduni unapoanza kama Mama Ntilie vile unavyoovaa ndio
unajijingea utamaduni wako, mtu anaingia kwenye biashara wanakuwa hawana
kanuni za utamaduni kwa sababu ukienda #Clouds wana utamaduni wao, ukiona Max Malipo wanafanikiwa kutokana na utamaduni.
Kama kijana lazima utengeneze utamaduni wa kesho utafanya nini, utaenda wapi...?
*Kutengeneza Mtaji- Vijana wengi watazungumzia mtaji badala ya kutengeneza bidhaa, ukitengeneza bidhaa itajiuza." @nikkwapili
Mkuu wa
Wilaya ya Iringa, Mh. Richard Kasesela akizungumza kwenye kongamano la
Fursa 2016 kwa vijana liliyofanyika leo jijini Dar es Salaam kwenye
ukumbi wa Mtana, Millenium Towers.
Mkurugenzi
wa Sera na Mipango wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Francis
Assenga akitoa elimu na maelezo kwa vijana na wakulima kujitokeza
kuwezeshwa na benki hiyo.
Injinia Juma Rajab ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya MaxMalipo akitoa elimu katika kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Francis Assenga akisisitiza jambo kwenye kongamano hilo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw.
Alvaro Rodriguez akitoa elimu kuhusu malengo ya maendeleo endelevu
(SDGs) kwa vijana walioshiriki kongamano la Fursa 2016 jijini Dar.
Mtalaam wa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce Temu akiwapiga msasa juu
ya malengo ya dunia vijana walioshiriki kongamano la Fursa 2016 jijini
Dar.
|
Damas Anthony Mwandishi wa Apostle Blogspot. Ni
muhimu sana kwa vijana kuelewa Malengo ya Dunia. Huu ni wakati wao. Kwa
kuyaelewa malengo haya inarahisisha utekelezaji wake. Nimefurahi kuona
muamko wa vijana waliojitekeza hapa leo na natumaini watawafikishia
wengine ujumbe huu.” ( picha; David Mtegile) |
|
picha ya Maktaba |
credit to
Zainul Mzige
Operations Manager @ Mo Blog