GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na
kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa
muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya
gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.
Kwa mara ya kwanza tuzo za Gospo Awards zitatolewa tarehe 30.04.2017
ndani ya ukumbi wa City Christian Center jijini Dar es salaam kuanzia
saa nane mchana.
SABABU ZA KUANZISHWA KWA TUZO ZA GOSPO (GOSPO AWARDS)
- Kutambua na kuthamini kazi njema na jitihada za waimbaji na wanamuziki wa nyimbo za Injili.
- Kutoa hamasa na ari kwa wanamuziki na waimbaji wa nyimbo za Injili.
- Kuleta mageuzi mapya katika tasnia ya muziki wa Injili Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
- Kuongeza chachu ya maendeleo ya ubora wa kazi za wanamuziki na waimbaji wa nyimbo za Injili.
- Kupanua wigo wa soko la Muziki wa Injili kutoka ngazi ya kitaifa kwenda kimataifa.
- Kutambua na kukuza vipaji vya waimbaji na wanamuziki wapya wa nyimbo za Injili ili kuboresha tasnia ya muziki wa Injili.
- Kuhamasisha na kukuza ushirikiano na mshikamano baina ya waimbaji,
wanamuziki, na wadau mbalimbali katika tasnia ya muziki wa Injili.
Tuzo za
GOSPO Awards zitakuwa zinafanyika mara moja
kila mwaka ikishirikisha waimbaji, wanamuziki na wadau mbalimbali kutoka
kwenye taasisi, mashirika ya kiserikali, mashirika binafsi, makampuni
na watu binafsi.
Vipengele vya Tuzo za Gospo (GOSPO Awards) mwaka 2016/2017 vimegawanyika kama ifuatavyo:
- Muimbaji bora wa kiume (Best Male Gospel Music Singer)
- Muimbaji bora wa Kike (Best Female Gospel Music Singer)
- Wimbo bora wa mwaka (Best Music Song of the Year)
- Video bora ya mwaka (Best video of the Year)
- Wimbo Bora wa kuabudu (Best Worship Song)
- Wimbo Bora wa Gospel HipHop (Best Gospel HipHop Song)
- Kundi/Bendi bora ya mwaka (Best Group/Music Band of the Year)
- Mtaarishaji bora wa Audio (Gospel Music Audio Producer)
- Mtaarishaji bora wa Video (Gospel Music Video Director)
- Album bora ya mwaka (Best Gospel Music Album)
- Muimbaji bora anayechipukia (Best Gospel Music Upcoming Artiste)
- Wimbo Bora wa kushirikiana (Best collabo)
- Wimbo bora wa mwaka kutoka Afrika mashariki (Best East African Song)
- Mtangazaji Bora wa Mwaka (Best Gospel Music presenter)
- Kipindi bora cha Radio (Best Gospel Music radio Program)
- Kipindi bora cha Tv (Best Gospel Music Tv Program)
- Management/Label bora ya mwaka
- Achievement Awards
- Tuzo ya heshima
- Tuzo Maalum (Special Award)
HATUA ZA KUPATA WASHIRIKI (NOMINEES) NA WASHINDI WA GOSPO AWARDS 2016/2017
HATUA YA KWANZA: Mapitio ya chati za kumi bora.
HATUA YA PILI: Kutangazwa kwa washiriki(Nominees)
HATUA YA TATU: Kupiga Kura
HATUA YA NNE: Kutangaza washindi wa Gospo Awards 2016/2017
VIGEZO NA MASHARTI YA KUSHIRIKI GOSPO AWARDS 2016/2017
- Wimbo au video ya muimbaji husika ni lazima iwe imefuata misingi ya muziki wa Injili.
- Kazi ya Muimbaji ni lazima iwe imekidhi viwango vya ubora kiufundi.
- Wimbo au Video ya muimbaji ni iwe walau imetangazwa kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, blogs na vyombo vingine vya habari kama vile radio na tv ndani ya mwaka husika.
- Wimbo au video ya muimbaji inayotakiwa kushiriki iwe walau
imefanikiwa kufanya vizuri kwenye chati mbalimbali za kumi bora kupitia
tovuti ya gospomedia.com, blog zingine za muziki wa Injili, radio na tv.
- Washiriki wa tuzo za Gospo Awards ni lazima wawe ni waimbaji na
wanamuziki kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla (Tanzania,
Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Congo).
Baada ya sherehe za utoaji wa Tuzo za gospo/Gospo Awards, uongozi na
timu nzima ya gospomedia ikishirikiana na wadhamini na wadau mbalimbali
itajumuika pamoja kurudisha shukrani kwa jamii hasa kwa makundi maalumu
kama vile watoto waishio kwenye mazingira magumu, wagonjwa walio
hospitalini, wazee waliokosa msaada na walemavu lengo la programu hii ni
kufanya ibada ya pamoja katika kujali makundi maalumu ya watu
mbalimbali yaliyo na uhitaji wa misaada na faraja na kuwakumbusha uwepo
wa Mungu juu ya Maisha yao na kuwatia Moyo na baada ya shughuli hii
kutafanyika tamasha maalumu la kuwatambulisha washindi wa gospo awards
2016/2017, zoezi hili litafanyika ndani ya mikoa ya Tanzania.
Toa Maoni Hapa Chini