Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
Mida ya saa 2 Asubuhi katika maeneo ya Stand kuu ya mabasi Iringa aliibiwa mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 5.
Mtoto huyo aliibiwa na binti ambaye alikuwa amekuja kutafuta kazi. Akieleza tukio hilo Mama yake Bi Asha Shaban Lauza alisema " nikiwa naosha vyombo binti huyu ambaye toka jana alikuwa anatafuta kazi alianza kumpa maziwa mtoto yaliyo kwenye chupa mpaka mtoto akamaliza , baadae mtoto akajisaidia basi bila wasiwasi nikampa shilingi elfu kumi ili akanunue pampasi duka la pili tu akanyanyuka na mtoto kwenda dukani toka asubuhi mpaka sasa usiku hautuja muona" .
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alifika eneo la tukio baada ya kumhoji mzazi akagundua walichelewa kutoa taarifa polisi. Baada ya msako muda was saa 3 usiku mtoto alipatikana eneo la Mkungugu km 33 kutoka Iringa Mjini. Binti wa miaka 14 (Jina linahifadhiwa) alikuwa akitoroka na mtoto huyo gari la polisi la doria likishirikiana na wananchi wa kijiji cha Mkungugu lilifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mwizi huyo wa mtoto.
Mkuu wa Wilaya alifika akiongozana na mama Mzazi wa mtoto pamoja na Diwani wa kata ya Kisinga Mh Ritha Mlagala. Binti mwizi yupo kituo cha polisi akiendelea kuhojiwa na mama mzazi baada ya kuandika maelezo alipewa fomu ya matibabu na kumpeleka mtoto hospitali. Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amekemea vikali kitendo cha uzembe wa mama huyu na wazazi kwa ujumla "pamoja na mama huyu kuwa na uchungu wa mtoto bado ana mashtaka ya kujibu ya uzembe, watu tusio wajua tusiwape watoto wetu hata kidogo huu ni uzembe wa hali ya juu" alisisitiza Mkuu wa wilaya.
Pichani anaonekana mtoto Latifa akiwa ambebwa na Mkuu wa wilaya walipofika kituo cha polisi.
Picha zingine ni za eneo la kijiji cha Mkungugu barabani alipokamatwa binti mwizi akiwa na mtoto usiku