JINA LA YESU KRISTO – MOJAWAPO YA FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI-Mwl Christopher Mwakasege | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Monday, February 6, 2017

JINA LA YESU KRISTO – MOJAWAPO YA FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI-Mwl Christopher Mwakasege

 JINA LA YESU KRISTO – MOJAWAPO YA FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI

sehemu ya 2
-Mwl Christopher Mwakasege

TAFAKARI JUU YA JINA LA YESU KRISTO
“Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali YATAFAKARI MANENO YAKE MCHANA NA USIKU, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapofanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.” (Yoshua 1:8)
Mtu mmoja aliwahi kuniuliza swali hili: “Je kutafakari maana yake nini?” Kila mara ninapofundisha somo hili nakutana na swali la jinsi hii .
Naamini kuwa swali hili linawatatanisha wengi kwa sababu bado hawajatofautisha kati ya kusoma neno na kutafakari neno.
Kusoma neno ni tofauti na kutafakari neno. Kulitafakari neno ni zaidi ya kulisoma neno. Watu wengi huwa wanasoma neno zaidi kuliko kulitafakari.
Kutafakari maana yake nini?
Maana ya karibu sana ya neno kutafakari ni kuwaza. Ni kusoma neno huku unalicheua na kulitafuna rohoni mwako.
Kutafakari ni njia mojawapo kubwa ya kuweza kuilisha roho yako. Yesu Kristo alisema “Imeandikwa, mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” (Mathayo 4:4)
Mkate ni chakula cha mwili wa nje ulio wa nyama na damu; neno la Mungu ni chakula cha mwili wa kiroho. Kinywa kinapokea chakula na meno yanatafuna.na kukivunjavunja huku kikilainishwa na mate, tayari kwa kumeza.
 Kusoma neno ni kama kinywa, kazi yake ni kulipokea neno. Kutafakari ni kuvunjavunja hilo neno huku Roho wa Mungu akililainisha liwe tayari kumezwa na roho yako.
Kutafakari neno kunamletea mtu siri ya ajabu ya uhakika na ushindi ndani ya Kristo.
Sisi ni watenda kazi pamoja na neno la Mungu hapa ulimwenguni. Tunaliwakilisha Neno la Kristo mahali tulipo na ulimwenguni pote.
 Na kwa sababu hiyo, Imeandikwa, “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote.” (Wakolosai 3:16)
Huwezi ukawa na Neno la Kristo moyoni mwako bila ya kuitumia siri ya kutafakari. Kukariri neno la Kristo hakutoshi peke yake kukuletea uhakika na ushindi kiroho na kimwili kama vile kutafakari kunavyofanya ndani ya mtu.
Kutafakari ni kuwaza. Kulitafakari jina la Yesu Kristo ni kuliwaza jina hili.
Tatizo kubwa sana ambalo linawapata watu ni tatizo la mawazo. Na huu ni ugonjwa mkubwa sana ambao umewakwamisha wengi katika maisha yao ya kiroho.
Kutafakari na kuwaza ni jambo la rohoni, - ni jambo la rohoni! Si jambo la akili kama wengi wanavyodhani.
Mtu anapowaza, au kutafakari jambo huwa ni jambo linalofanyika rohoni mwake, ingawa utadhani linafanyika katika ubongo.
 Je! Wewe unayesoma somo hili sasa hivi unawaza nini rohoni mwako, unatafakari nini? Mara nyingi utaona mtu anaposoma Neno mawazo yake mara nyingi yanakuwa mbali sana, kwa hiyo hakuna anachoelewa katika hayo anayosoma.
 Pia, hata wakati watu wanasikiliza neno la Mungu, mara nyingi mawazo yao yanakuwa mbali sana na neno linalofundishwa. Hii inajidhihirisha hasa ukimwuuliza mtu huyo muda mchache baadaye, juu ya neno lililofundishwa maana hatakumbuka.
 Unapoumwa huwa unawaza nini? Wengi wanautafakari ugonjwa, na wengine hata kukata tamaa anapoona hauponi haraka. Wengine wanapoumwa wanawaza na kutafakari kufa kuliko kuishi.
Unapokuwa una matatizo huwa unawaza nin? Unapokosa maelewano na mwenzako, nyumbani, kazini au mahali popote, huwa mawazo yako yanawaza nini?
Unapokuwa huna fedha au vitu fulani vya kimwili huwa unawaza au kutafakari nini?
 Tunaweza kusema mengi lakini swali kubwa ni hili; “Kila wakati huwa unawaza nini na kutafakari nini?”
 Je! unafahamu ya kuwa matendo yako na maneno yako , ni matokeo ya mawazo uliyonayo? Mtu husema anachokitafakari au kukiwaza, na pia hutenda anachokitafakari au kukiwaza moyoni mwake.
 Ukitaka kumfahamu mtu alivyo rohoni mwake, sikiliza maneno anayosema na angalia matendo anayoyatenda. 


Sijaona katika biblia ambapo mtu wa Mungu ameambiwa aitafakari shida yake, awaze juu ya ugonjwa wake au udhaifu wake.

Kumbuka kuwa maneno ni chakula cha roho, hali ya roho yako inategemea sana ni maneno gani unayasikia kila wakati na kuyatafakari.

Unapotafakari shida, magonjwa, hofu, unaifanya roho yako ijengeke katika hayo. Ukilitafakari jina la Yesu Kristo roho yako inajengeka katika jina hili.

Watu wengi sana wamejengeka katika kumwogopa shetani kuliko Mungu. Hii hali ipo hata kwa watu wa Mungu. Hayo ni matokeo ya kumtafakari shetani na majaribu anayowajaribu, kuliko kumtafakari Mungu na uweza wake.

Neno la Kristo linakosa nafasi katika roho za watu, kwa sababu roho za watu zimejaa mawazo ya dunia hii na shida zake. Roho za watu zimejaa mawazo yanayopinga na kwenda kinyume kabisa na neno la Kristo.

Roho za mtu ni uwanja wa vita. Ukishinda vita katika mawazo, utakuwa umeshinda vita katika mwili, katika roho na katika maneno.

Wakati mmoja nilianza kujiuliza kwa nini Nabii Ezekieli aliambiwa ale gombo la chuo, na mtume Yohana aliambiwa ale kitabu kilichofunguliwa.

Sikuelewa kwa nini hawakusoma tu maneno ambayo yalikuwa yameandikwa bila kula gombo la chuo na kitabu kilichofunguliwa. Mungu alikuwa ana uwezo wa kuwaambia wayasome maneno aliyokuwa anawaonyesha – lakini badala yake aliwaambia wale – kwa nini?

Nilikuwa siioni tofauti ya kusoma na kula. Kuna tofauti kubwa kati ya kusoma ujumbe wa Mungu na kula ujumbe wa Mungu. Soma Ezekieli 2:7 10; 3:1 – 3 na Ufunuo wa Yohana 10:1 – 2; 8 – 11.

Mtu anapokula chakula, huwa kinatafunwa na kulainishwa kabla ya kumezwa. Na kikimezwa na kuingia tumboni, kinanyonywa na kuingia katika mishipa ya damu inayozunguka mwili mzima na kukisambaza chakula hicho katika sehemu zinazohitajika.

Mtu anapotembea, ukweli ni kwamba ni chakula kile alichokula ndicho kinachotembea. INGAWA yeye ndiye anayeonekana anatembea.

Kwa hiyo Ezekieli na Yohana walipokula ujumbe wa Bwana uliokuwa umeandikwa katika gombo la chuo na katika kitabu kilichofunguliwa, ujumbe huo uliingia ndani yao kama vile ambavyo wangekula nyama.

Ujumbe huo uliingia kwenye damu yao na ukajenga misuli. Kila sehemu ilikuwa imejaa ujumbe wa Mungu. Ujumbe huo ndio uliowafanya wapate nguvu ya kutembea, na kuishi na kusema.

Kwa mtazamo mwingine tunaweza kusema, Ezekieli na Yohana walikuwa ni ujumbe wa Mungu uliokuwa unatembea.

Na sisi tukilitafakari neno la Kristo; na likijaa ndani yetu kwa wingi, tunakuwa ni neno la Kristo linalotembea; tunakuwa ni neno la Kristo linalosema; tunakuwa ni neno la Kristo linaloponya.

Tunafika mahali ambapo kuishi kwetu kunakuwa ni neno (Kristo) – kama vile Paulo alivyosema “Kuishi ni Kristo” (Wafilipi 1:21). Tukilitafakari jina la Yesu Kristo, tunakuwa ni jina la Yesu Kristo linalotembea,,, Je! unauona umuhimu juu ya jambo ninalokuambia la kutafakari?

Mtu anashindwa kuwa mtendaji wa Neno kwa kuwa moyoni mwake hakuna neno. Anabaki kuwa mtendaji wa maneno mengine aliyonayo mawazoni mwake tu.

“Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome); tukiangusha MAWAZO na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara KILA FIKRA ipate kumtii Kristo” (2 Wakorintho 10: 3 – 5).

Hii ina maana kuwa fikra zako ziwaze sambamba na Neno (Kristo).

Katika kuishi kwetu na kuenenda kwetu tuwe tunatafakari nini mioyoni mwetu, ili roho zetu zipate chakula safi cha kiroho?

“Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya staha, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema, ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote YATAFAKARINI HAYO” (Wafilipi 4:8).


  Neno la Mungu ndilo kweli inayodumu milele. Neno la Mungu ndilo linalompa mtu uhakika wa jambo ambao hauwezi kuyumbishwa na kitu cho chote.

Neno la Mungu linahifadhiwa ndani ya moyo wa mtu kwa kulitafakari na siyo kwa kukariri peke yake. Mtu anayekariri mistari ya biblia ni sawa sawa na mtu anayekula mahindi au chakula cho chote bila kutafuna.

“Neno la Kristo na likae moyoni mwako kwa wingi katika hekima yote” (Wakolosai 3:16)

Kumbuka, Neno la Mungu moyoni mwako ndilo linalokupa uhakika wa mambo yako yote; (Wokovu, uponyaji, ushindi katika majaribu; mamlaka yako juu ya shetani na kazi zake, uzima wa milele, na kadhalika).

Na huo ndio msingi mkubwa wa Imani, kwa kuwa “Imani ni kuwa na hakika ya mambo ………”
(Waebrania 11:1).

Kabla imani yako katika Kristo haijaonekana katika matendo yako na maneno yako ni lazima ijengeke kwanza katika moyo wako kwa njia ya kulitafakari au kuliwaza neno la Mungu katika mambo yako yote.

Matokeo yake ni kwamba utakuwa na uhakika wa jambo lo lote moyoni mwako na kwa ajili hiyo utakuwa na ujasiri wa kulisema na kulitenda.

Usipokuwa na uhakika wa jambo moyoni mwako, huwezi ukawa na ujasiri wa kulisema na kulitenda.

Neno la Mungu ndilo nuru na taa miguuni petu sisi tulio ndani yake (Zaburi 119:105); na kwa sababu hiyo tunaishi katika imani iliyo na uhakika udumuo, na wala si wa kubahatisha.

Kwa sababu ya umuhimu wa kutafakari neno la Kristo, hapa ninaorodhesha baadhi ya mistari inayozungumza juu ya jina la Yesu Kristo. Soma maneno yaliyomo na kuyatafakari mara kwa mara na baada ya muda utaona ushindi wa ajabu utakapokuwa unalitumia jina hili la Yesu Kristo.

Hakuna wokovu katika mwingine:

“Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo ya Mitume 4:12).

“Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:21).

“Bali wote waliompokea (Yesu Kristo) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake, waliozaliwa si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu” (Yohana 1:12 – 13)

“Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani, maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, kila atakayeliitia jina la Bwana (Yesu Kristo) ataokoka” (Warumi 10:12 – 13).

Ni amri kuliamini jina la Yesu Kristo – sio ombi:

“Na hii ndiyo amri yake, kwamba TULIAMINI JINA LA MWANA WAKE YESU KRISTO, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri” (1Yohana 3:23)

“Amwaminiye yeye (Yesu Kristo) hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini JINA LA MWANA PEKEE WA MUNGU” (Yohana 3:18)

Kuna uponyaji katika jina la Yesu Kristo:

“ Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; …….. wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya” (Marko 16:17 – 18)

“Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliitia jina la Bwana ataponywa …” (Yoeli 2:32).

Lolote ulifanyalo – lifanye katika jina la Yesu Kristo:

“Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye” (Wakolosai 3:17).

Kuomba na kupewa katika jina la Yesu Kristo

“Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya ….. Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” (Yohana 14:13 – 14; 26).

“Si ninyi mlionichangua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi, nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni” (Yohana 16:23 – 24).

Jina lipitalo kila jina

“Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia jina lile lipitalo kila jina, ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba” (Wafilipi 2:9 – 10)

Hii ni baadhi tu ya mistari mingi iliyomo katika Biblia inayozungumza juu ya jina la Yesu Kristo. Waza juu ya jina la Yesu mara kwa mara na hakika utafanikiwa.
 
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.