SIKU: 5. SOMO: *HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO*MWL. C. MWAKASEGE | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Friday, March 10, 2017

SIKU: 5. SOMO: *HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO*MWL. C. MWAKASEGE

SOMO: *HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO*
ENEO: *DAR ES SALAAM*
SIKU: 5 March, 9 2017
MWL. C. MWAKASEGE



*LENGO YA SOMO:*
Kuhakikisha ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi yanafunguliwa
*Kumb 6:12, 2Nyk 7:14*
*SUMMARY YA SIKU 4*
Pitia somo la siku ya kwanza mpaka siku ya tatu ili kujua tulipotoka na yale mambo ya msingi 5 juu ya kufungua mafanikio yako yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba ya utumwa siku ya kwanza na vipengele 6 vya namna ya kujiondoa kwenye madhara ya lango ya ardhi ya nyumba unayoishi inapomilikiwa kiroho ya nguvu za shetani kwa siku ya pili, siku ya tatu tulijifunza mambo 7 juu ya kufunguliwa toka kwenye kiapo kilichoifunga nafsi yako na hali ya kiroho ya ardhi na kwa siku ya nne tulijifunza hatua 8 za kimaombi kwa ajili ya kujitoa kwenye kifungo cha kiapo kilichoungwa na ardhi
Leo tujifunze *JINSI UKIWA ULIOPO KATIKA ARDHI UNAVYOWEZA KUZUIA MAFANIKIO YA MTU ANAYEHUSIKA NA ARDHI HIYO*
Na tutazame katika mtiririko ufuatao
1⃣Ukiwa maana yake nini Kibiblia?
Ni hali ya kiroho inayojidhihirisha katika maisha ya mtu ili kuonyesha ya kuwa eneo hilo la ardhi limo katika adhabu
*Ez 15:8*
Kumbuka tulipotoka *2Nyk 7:14*
Nchi maana yake ni ardhi yenye mipaka halali, kwa hiyo anavyosema nitaifanya nchi kuwa ukiwa MUNGU anazungumza ardhi yenye mipaka halali kuwa ukiwa
*Mwz 1:1-2*
Hapo mwanzo MUNGU aliziumba mbingu na nchi, nayo nchi ilikuwa ukiwa, utupu na ina giza na kile kitabu cha isaya anasema MUNGU hakuimbua dunia iwe ukiwa bali ikaliwe na watu. Kwahiyo kama MUNGU hakuumba ukiwa na wakati wa uumbaji ukiwa ulikuwepo kumefichika vitu fulani acha nisiseme leo nilitaka tu ujue maana ya ukiwa
2⃣Utaitambuaje ardhi yenye ukiwa?
Kwa kuangalia unavyojisikia moyoni mwako unapokanyaga ardhi ya eneo hilo
*Yer 4:27-28*
..Kwa ajili ya ukiwa nchi itaomboleza..
*Yosh 5:14-15*
unatuonyesha jinsi Yoshua alivyoukabiri Yeriko akatokea jemedali wa BWANA akapopoma kiusouso na kuuliza BWANA aniambia nini mimi mtumishi wake? Malaika alimwambia vua viatu vyako maana hapo unaposimama ni nchi takatifu..maana kuna mahusiano kati ya miguu yako mahali inapokanyaga na uwezo wa kusikia ndo maana Biblia inasema tuvae utayari miguu mwetu
MUNGU anaposema nchi takatifu maana yake ameisafisha, ameitenga haina sauti za kukuchanganya tena amekutengenezea mazingira ya kukusikilizisha jambo! Wajengao makanisa wanaweka wakfu ile ardhi maana yake wanaitenga ili iweze kutumika kwa makusudi ya MUNGU na wale wanaokuja pale waweze kumsikia MUNGU akisema bila kusumbuliwa na sauti zingine zilizoko ndani ya ardhi
Lile eneo lilikuwa limesafishwa lakini shida ilikuwa Yoshua alichovaa, aliambiwa vua viatu vyako maana yake nini ..Joshua kuna kitu nataka kukusemesha cha kukusaidia juu ya Yeriko lakini huna utayari kuna kitu ulichovaa, kuna mipango uliyonayo, kuna makusudi uliyonayo ambayo hauko tayari kuyaachia lakini unataka nikusaidie..
Tatizo si kusikia tu peke yake bali ni ule utayari wa kutekeleza unachosikia. Ndiyo maana wengi husema MUNGU hajanisemesha siyo kweli bali ni wewe umekataa kusikia kuna vitu umeshajiamulia jinsi gani MUNGU aseme kwako
Kama ukienda eneo ambalo lina ukiwa utasikia moyoni mwako kuomboleza gafla na huoni kitu kwa jinsia ya nje kinachokusuma kuomboleza
*Yer 4:23*
Ukikanyaga mahali peke ukiwa gafla utasikia upweke moyoni hata kama umezungukwa na watu au utasikia upweke sababu hakuna watu wakati unajua unaweza kukaa bila upweke hata kama hakuna watu
*Yer 4:31*
*Yer 51:29*
Ukikanyaga eneo lenye ukiwa si tu utasikia kuomboleza ama upweke bali saa nyingine utasikia kuomba maombi ya kuomboleza maombi ya kuzaa kitu, maana utasikia mzigo wa kuomba
*Ez 26:20*
Anazungumzia juu yakusikia moyoni mwako mauti, mahali palipo na ukiwa utasikia mauti ndani yako au kusikia kama umefiwa hata kama hujafika ndiyo maana mtu akifa kinachokuja ni ukiwa na ukiwa ni adhabu kwa hiyo adhabu inapokuja namna hiyo inatuonyesha kwamba haukuwa mpango wa MUNGU mtu afe bali tunakufa kwa sababu ya dhambi zilizokuwa zimeingia kwenye Bustani ya Eden
*2Sam 13:20-22*
Ukiwa wakati mwingine unaunganisha huzuni yenye uchungu ambayo ndani yake inakuwa na hasira na chuki
Si kila ukiwa unakaa juu ya ardhi bali kuna ukiwa unaokaa juu ya
Mtu
Tukio
Kikao
Mkutano
Ardhi
Unaweza ukaenda kwenye ardhi ambayo haina ukiwa lakini ameenda mtu mwenye ukiwa kama tamari ukiingia pale anaingia na ukiwa wake na ule ukiwa unafunika ardhi yote ile na kuwaambukiza wote waliokule ndani na wote wanasikia ukiwa
Saa zingine unakuta mtu akiwa ofisini anacheka na kutabasamu na kila mtu sasa subiri akifika nyumbani, ni hasira, aongei wala hana utulivu hata yeye hajui shida ni nini maana akitoka gafla eneo la nyumbani unaona anaongea na kila mtu hata wale wa nyumbani wakiwa eneo jingine. Wengine wakiwa kwenye biashara ni ugomvi lakini wakirudi nyumbani ni salama
3⃣Nini matokeo ya ukiwa katika ardhi juu ya maisha ya watu wanaohusika na ardhi hiyo
Matokeo kwa ujumla
Jambo kubwa sana utakaloona na kuligundua kwenye mistari ihusuyo ukiwa ni kwamba ukiwa unaweka zuio eneo hilo lisiendelezwe bila kumaliza au kuondoa tatizo lililo fanya ukiwa ukawepo..ukiwa hauji peke yake bali uweka na zuio.
Mfano una kiwanja lakini umeshindwa kukijenga au kukiendeleza, kuna sababu nyingi tu za kimsingi lakini sehemu kubwa sana iliyowakwamisha watu ni zuio linalotokana na ukiwa ulioko pale.
*Ez 48:8-14*
Wana wa Israel walikuwa wakipewa maelekezo na nabii Ezekiel kwamba mahali popote pale wanapokuwa kwenye maeneo ya kuishi lazima watoke maeneo mengine kama sadaka kwa MUNGU na hilo eneo linawekwa na kutengwa kwa ni mahali pa ibada na hilo eneo wanapewa makuhani na walawi kujenga
Inawezekana umenunua shamba au kiwanja ambacho kina zuio kisiuzwe, katika ulimwengu wa roho kina zuio kisiuzwe, sasa mtu anataka kukiuza wewe mnunuzi ukienda pale ukikanyaga tu unajisikia ukiwa, unajisikia kuomba. Hii ndiyo imewapata watu wengi sana walionunua ardhi za kurithi ambazo familia ziliweka zuio zisiuzwe..Mnunuzi anashangaa sasa kawekeza pesa gafla anaona eneo halisogei na kuendelea tena
*Ez 35:9*
Inawezekana umenunua kiwanja ambacho ukiwa umepewa zuio haruhusiwi mtu kukaa hapo, sasa na wewe unanunua kujenge nyumba gafla wazo la kuendeleza linapukutika hata kama fedha unazo za kufanya hivyo
*Zak 7:14*
*Sef 3:6*
Kuna zuio si tu kwamba usikae bali kuna zuio eneo hilo usitembelee, unapanga kwenda kwenye shamba ama eneo ulilonunua unajikuta umeshindwa kwenda…Wangapi wamenunua viwanja na mashamba na hawajayatembelea mwaka mzima?
*Yer 9:11*
Magofu…si kwamba watu hawana hela bali kuna zuio la kuendelea kujenga. Katika ulimwengu wa roho kuna kibao kwenye ardhi kikisema uruhusiwi kujenga hapa njoo kwa MUNGU uambiwe ni kwanini
*Yer 51:26*
Umekwama kwenye msingi..jiwe la pembeni anazungumzia majengo ya ibada unachukua kiwanja kwa ajili ya kujenga jengo la ibada inagomea kwenye msingi si kwamba watu hawana pesa bali kuna zuio kwenye kiwanja maana MUNGU hawezi kuagiza kazi akashindwa kulipia, si maskini akageuka ombaomba. Ukiona unafanya kazi ya MUNGU na pesa inakupa shida rudi kwa MUNGU kwa TOBA usijaribu kujihesabia haki, usijaribu kumkemea shetani yawezekana akasema ninakibali cha MUNGU wako kukaa hapa lazima MUNGU akupe kibali na uhalali wa kumtoa
Kesho ntazungumza nawe na kukupa mistari yake kwanini ukijenga nyumba inabomoka au kwanini ukijenga nyumba unashindwa kukaa ndani yake au kwa wale wanaofanya biashara bila kujua eneo hilo lina zuio la uzalishaji.
Leo tuangalie kwa wale ambao wanaishi ndani ya nyumba iliyowekewa zuio watu kuishi lakini umeng’ang’ana kukaa na huna raha
*Isy 13:20-22*
Saa nyingine MUNGU anaweka zuio na anajua kuna watu wengine watalazimisha kukaa kwa hiyo anaweka vitu vingine ndani kukuzuia..Ukitaka kuona tafuta nyumba yoyote mtaani ambayo haijakaliwa na watu mda mrefu kuwa na uhakika utakuta majini, bundi, mbuni na mbwea..Sasa si kwambii uogope kununua maana si wajua YESU ni mkuu kuliko majini.
Sasa wengi ununua tu ama na kukarabati unafanya maombi tu kirahisi rahisi bila kujua namna ya kufanya na MUNGU anajaribu kukusemesha na kukuwekea ishara mahali pale kwamba kuna kitu hajika kaa sawa wewe unalala, uwe na uhakika yale majini yaliyopo mahali pale yamepata nafasi ya kusherekea
Yakobo wakati anamkimbia Esau akafika eneo moja linaitwa luzu baadae alipaita betheli akalala gafla aliota, alipoamka alisema kumbe hapa MUNGU yupo, kumbe hili ni lango la mbinguni, alilala mahali ambapo kuna madhabahu chini. Sasa fikiri unauziwa nyumba ambayo ndani yake mtu aliweka madhabahu ya mungu wake halafu unalala ukiota unafikiri utaota nini miungu ya pale na kukupa utaratibu wa kukaa hapo
Kuna wakristo wengi sana ambao wanashindwa kukaa kwenye nyumba zao hawalali na hawapati msaada wanaomba na kuomba na kujikuta wanaenda kwa waganga wakipewa pua ya nguruwe wakifiri shetani anaogopa nguruwe wakati mapepo yalimwomba YESU yawaingie wale nguruwe sasa unadanganywa tu. Na wakati mwingine unajikuta unaota ndoto mbaya sababu ni eneo ulilolala
*MAOMBI*
Masomo kama haya ndiyo maana nang’ang’ana kupeleka mstari kwa mstari ili ujue yako kwenye Biblia MUNGU anahitaji kukupa macho ya kuona na kuweza kuweka haya mambo sawasawa. Haya mambo ni halisi kuliko unavyofikiri na yanatesa watu wengi sana

#Tazama_kupitia https://youtu.be/91O3UI_0E30
*TANGAZO MUHIMU*
👌🏽Jumamosi asubuhi kama una huduma ya ualimu hata kama ujui njoo kuna mafundisho na shule ya ualimu kujua na kutambua
👌🏽Na tarehe 14 May Diamond Jubilee siku ya vijana
👌🏽Kila siku maombi yatakuwa yanafanyika mahali hapa kufuatata na somo la siku hiyo

#MUNGU_akubariki_Mtumishi_wa_MUNGU_Mwl_C_Mwakasege
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.