Day 3. FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA- Mwl Mwakasege | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Tuesday, April 4, 2017

Day 3. FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA- Mwl Mwakasege

3⃣ *SEMINA YA NENO LA MUNGU  DODOMA UWANJA WA  BARAFU*

*FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA*

*NA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE*

*4 APRIL 2017*

*LENGO: KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU ILI UFANIKIWE KIMAISHA*.

Jana tulipitia mambo mawili

*JAMBO 1*
Shetani anaweza kutumia NDOTO kupandikiza mambo ambayo usipoyang'oa mapema yataharibu maisha yako

*JAMBO 2*
Kutazama ishara  zitakazo kuonyesha kuwa NDOTO zinahitaji kufuatiliwa

*Jambo 3*
⏩Tumia viashiria vilivyokuja na ndoto ili kujua ikiwa umeiombea hiy Ndoto na kuifuatilia ipasavyo

VIASHIRIA- Imetoka katika Neno ishara

_Marko 16:17 *Na ishara hizi* zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;_

⏩Ishara haziji peke yake huwa zina ambatanishwa na kitu Fulani
Kutoka 4:1-8
_Mstr 8... Basi itakuwa, wasipokusadiki, *wala kuisikiliza sauti ya ishara ya* kwanza, wataisikiliza sauti ya *ishara ya pili*._

⏩Ishara zina sauti
Musa aliambiwa kwa ishara ya kijiti kilichokuwa kinaungua bila kuteketea

⏩Ishara ilikuwa kama kibao ili kuelekeza kuwa hayo yaliyosemwa ni kweli

⏩Ndoto lazima zije na viashiria ili uzifuatilie,ishara ndani yake imebeba  msukumo wa kitu fulani

_Daniel 4:4-7 Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi. Nikaota *ndoto iliyonitia hofu;* mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha. *Basi nikatoa amri kwamba wenye hekima wote wa Babeli, waletwe mbele yangu, ili kunijulisha tafsiri ya ndoto ile.* Ndipo wakaingia waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu; nikawahadithia ile ndoto; wao wasiweze kunijulisha tafsiri yake._

Katika Ndoto ya Nebukadreza ilibeba mambo 4
1. Hofu
2.Mfadhaiko
3. Msukumo wa kupata tafsiri
4. Msukumo wa kuisumulia

⏩Nia ya Nebukadreza ilikuwa ni kutafuta Tafsiri ya hiyo ndoto. Hizo Ishara 4 zilikuja kwa msisitizo ili kumfanya atafute maana yake ndio maana alitafuta watu mbalimbali kumtafsiria

⏩Ukiona umeota ina ishara zaidi ya 1 ujue ina mzigo na inabidi uifuatilie
Daniel 4:6-7( hapa aliota ndoto) 👆👆

thenDaniel  20-26( alipewa Tafsiri ya ndoto) _Ule mti uliouona, uliokua, ukawa na nguvu, urefu wake ukafika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka dunia yote; ambao majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha wote; ambao chini yake wanyama wa kondeni walikaa, na ndege wa angani walikuwa na makao yao katika matawi yake; ni wewe, Ee mfalme, uliyekua, na kupata nguvu; maana ukuu wako umekua na kufika mpaka mbinguni, na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia_.

_Tena, kwa kuwa mfalme alimwona mlinzi, naye ni mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni, akisema, Ukateni mti huu, mkauangamize; ila kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikatiwe maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama wa kondeni, hata nyakati saba zipite juu yake; tafsiri yake ni hii, Ee mfalme, nayo ni amri yake Aliye juu, iliyomjia bwana wangu, mfalme; ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng’ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote. Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala._

27- ( alipewa ushauri wa yapi ya kuyafanya)

_*Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha.*_

*NOTE*

⏩Watu wengi wanakuwa na hamu ya kutafsiriwa ndoto bila kutaka kusikiliza ushauri uliopo ktk hiyo  ndoto

⏩Tafsiri ya ndoto ina vitu 2
*1. Ujumbe*
*2. Ushauri*

Ni vema uvipate vyote sio kimoja. Nebukadreza alichukua *Tafsiri akaacha ushauri*

*Jambo la 3* katika ndoto ya Nebukadreza. Daniel alipata kiashiria kama cha Nebukadreza ( mfadhaiko). Daniel  alipopewa taarifa ya Ndoto ndani yake ilimtibua

⏩Daniel alitaka ajue
1. Yaliyokusudiwa ndani ya Ndoto yatatokea. Mfano kuna watu wanaoota mambo na baada ya muda yanatokea ,usifurahie  hizi ndoto huwa ni taarifa ili kama ni mbaya uipangue mapema au kama nzuri uiombee. Una uwezo  wa kuibadili Yale yaliyoonekana ktk mst 27

Mst 28".... _*Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza*._

Kama Nebukadreza angefuata ushauri aliopewa na Daniel yasingemkuta hayo  kwani alipewa allowance ya miezi 12 ya kutengeneza ila hakuyafuata na baada ya hiyo  miezi 12 yakampata ya kukaa kondeni na wanyama miaka 7,
soma Daniel 4:31-33 _Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; *Ufalme huu umeondoka kwako. Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote. Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.*_

⏩Kuna gharama za kupuuzia ushauri unaopewa ,ona yaliyomkuta Nebukadreza aliishia kutolewa ufahamu wake na kuishi porini na wanyama

👉Ndoto aliyoota kwa muda mfupi aliipuuzia kwa miezi 12 na ilimtesa maisha yake kwa miaka 7

⏩Mungu alikiacha kiti cha Nebukadreza kwa miaka 7 bila kiongozi ili ajue kunae Mungu wa mbingu na nchi. Soma mstr 4: 34-37

_Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi; na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe? Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi. Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili._

4. Unapo ikumbuka kuifuatilia ndoto mara kwa mara au unapoimbea na ukaona viashiria haviondoki ujue kuna jambo ndani ya ndoto inahitaji kuifuatilia

⏩Mfaidhaiko wa Nebukadreza sio wake ni ndoto aliyoota

⏩Unapopata mzigo wa kumuombea mtu kuombea *ombea saa hiyohiyo* usisubiri kumhadithia mtu hadi upate kibali,unaweza muhadithia ndio ukamvuruga zaidi.

⏩Unaweza kuta umeingizwa kwenye maagano ya ukoo ukawa unaomba bila mafanikio,inabidi ufanye maombi ya kujitoa kwenye hayo maagano kwa kulifuta jina lako kwa Damu ya Yesu ,usiwe kama wale wanaosema *"Ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya"* ni lazima ujitoe kwenye hayo maagano maana huwezi jua wanamtumia mungu gani unajikuta mambo yako hayafanikiwi kumbe umeunganishwa na maagano

Kuna mtu aliota kang'atwa na nyoka ktk ndoto na alivyoamka akajikuta damu inatoka sehemu hiyo. Hivyo alikuwa kaachiwa roho ya mauti na ile  sumu iliharibu maisha yake kabisa kwani familia yao ilikuwa imeingia ktk maagano hivyo ingawa alikuwa kaokoka hakufanikiwa kwa sababu yalikuwa na uhalali nae

*MAOMBI*

🛐Fanya Toba

🛐Ita Damu ya Yesu itakase popote ambapo uling'atwa na ng'e,mbwa,nyoka, mende n.k  katika ndoto ili kukuondolea uhalali wa shetani kukutesa

🛐Tubu kwa kuachia mlango uliochilia  mashambulizi ambayo yanamiliki mwili wako

🛐Futa sumu yoyote iliyoachwa kupitia ndoto na ondoa jina lako kwenye maagano kwa kujua au kutojua kwa jina la Yesu

Amen na ubarikiwe sana.

_Glory_
_Dodoma_
_Tuonane tena somo lijalo._
👋👋👋👋👋👋👋

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.