Day1. Semina ya Mwl. Mwakasege Dodoma " FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZO OTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA" | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Sunday, April 2, 2017

Day1. Semina ya Mwl. Mwakasege Dodoma " FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZO OTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA"

1⃣ *FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA.*

*NA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE*

*DODOMA UWANJA WA BARAFU*

*2 APRIL 2017*

*LENGO: KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU ILI UFANIKIWE KIMAISHA*.

*MUHIMU.SEMINA HII ITAKUWA IKIRUDIWA KWENYE DODOMA CABLE KWA SIKU MARA TATU. SAA NNE ASUBUH, SAA SABA MCHANA NA SAA TATU USIKU KILA SIKU HADI SEMINA ITAKAPOISHA*

PIA SEMINA IKO LIVE MAENEO MENGI NCHINI KWA NJIA YA REDIO. ANGALIA PALE CHINI

👉Somo hili litatoa majibu ya Maswali ya watu wengi kadri Mungu atakavyotusaidia.

👉Hili somo halipatikani kirahisi rahisi na miaka ile tulivyooanza tulipata shida  sana. Na hata vitabu havipo vingi sana vinavyoeleza mambo ya ndoto . Kwa hiyo twende pamoja.

*Jambo la 1.* *_Shetani anaweza kutumia ndoto kupandikiza vitu kwako ambavyo usipoving'oa vinaweza kwamisha maisha yako_*

_Ndipo huyo Elifazi, Mtemani, akajibu na kusema,  Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong’ono yake.   Katika mawazo yaliyotoka *katika maono ya usiku*, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.  Hofu iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote.   Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama.  Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,_ *AYUBU. 4:1‭, ‬12‭-‬16*

👉 Maana ya maono  ni ndoto  na ndio maana maandiko yanasema

_Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.   *Katika ndoto, katika maono ya usiku,* Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;_ *AYU. 33:14‭-‬15*

👉Hapa kuna vitu vinne yaani kuna

1 wazo liliingia ndani yake kwa ndoto

2 katika masikio iliingia sauti iliyoharibu usikivu wake

3 Hofu ilimwingia

4 Mifupa yake ikaanza kutetemeka

Na kuonesha kitu kilichokuja kwake na aliona pepo lililoingiza vitu ndani yake. Tangu siku hiyo hivyo vitu vilimsumbua sana kama hakupata msaada wa kuving'oa basi vilivuruga maisha yake.

Angalizo. Usiipuuzie ndoto unayo ota maana inaweza tumika

👉Kukuletea ujumbe wa Mungu
👉Kukuletea Maonyo
👉Au shetani anaweza pandikiza vitu.

*MFANO WA PILI*
_Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye._ *KUMBU KUMBU. 13:1‭-‬4*

Ndoto inaweza tumika na shetani
1.kupandikiza unabii wa uongo kwa kutumia ishara.

2.Wanapewa uwezo wa kushawishi watu wasimfuate Mungu katika Kristo Yesu. 

Mara nyingi hatakuja na ndoto atakuja na ishara na utampokea kwa sababu ya ishara au muujiza. Na yeye ataleta na ujumbe na itakuwa ngumu sana kwako  kukataa kwa sababu umeona ishara au muujiza . Na lengo kubwa ni kuwa uache kumfuata Mungu na kumpenda Mungu  kutapoa na utapoteza hofu ya Mungu

👉Unapoteza kuambatana na Mungu.

👉Unatopeteza kusikia Mungu anachosema na utaanza kupotea na utaanza kusikia neno la mtumishi zaidi bila kufuata neno la Mungu.  Na wengi wamekwama hapo.

Watumishi wameacha kumtumikia Mungu kwa sababu waliota ndoto na kuna vitu vilikuja na mbwembwe na wakidhani ni Mungu kumbe sio

*MFANO WA TATU.*
_Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, *Nimeota ndoto; nimeota ndoto.* Je! Mambo hayo yatakuwa katika mioyo ya manabii wanaotabiri uongo hata lini, manabii hao wenye udanganyifu katika mioyo yao wenyewe? Wanaodhania ya kuwa watawasahaulisha watu wangu jina langu kwa ndoto zao, wanazomhadithia kila mtu jirani yake, kama vile baba zao walivyolisahau jina langu, kwa ajili ya Baali._ YEREMIA. 23:25‭-‬27 SUV

*Hapa unaona ndoto ilipandikiza*
1.Unabii wa uongo

2.Udanganyifu moyoni mwake

3.Alipewa nguvu ya kushawishi watu wa Mungu walisahau jina la Mungu, jina linawakilisha heshima, uwepo au mamlaka aliyonayo mwenye jina kwako.

Mtu akikusahaulisha jina la Yesu.
👉Hujali tena neno la Mungu
👉Hutaona thamani wa uwepo wa Yesu.
👉Hutakuwa na heshima kwa Yesu

Na chanzo cha haya ni ndoto, na anahadhia watu ili kupandikiza kitu ndani ya mioyo ya watu ili wakae mbali na Mungu.

_Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA._
YEREMIA. 23:28

_Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto._
HESABU 12:6

Ndoto ni njia moja wapo Mungu anatumia kuwapa unabii watu. Na shetani nae anaiga na analeta manabii wa uongo, waalimu na mitume wa uongo.

Kuna manabii wa kweli Mungu anasema nao na kuna nabii wa uongo ambao shetani anaweka.

Pia hii itakusaidia kuchukua *tahadhari na kuweza kutofautisha*. Mambo haya yanahitaji ufutailiaji wa Karibu

Na nilipoanza kufundisha hili somo nimepata kuona ndoto nyingi sana na watu wengi sana wanauliza. Na bado naendelea kufuatilia

Mungu alianza kusema na mimi miaka ile ya 80 na ilinisukuma kufuatilia sana ndoto na wakati ule sijaokoka nilienda kwa waganga na walinipa tafsiri lakini sio kwa usahihi. Ndipo baada ya kuokoka Neema ya Mungu ilianza kunifundisha kwa hatua kwa hatua kwa muda mrefu kidogo ndipo sasa nilianza kufundisha..

*MFANO WA NNE.*
Kuna mtu  aliniandikia kuwa kaota ndoto kuna mtu anakata kwa kisu kidole cha gumba cha mguu wa kulia na baada ya kuamka nilianza kusikia maumivu. miezi 3 baadae kidole kikaaza kuweka weusi pale alipokatwa na palikuwa peusi na kuanza kuwasha na hadi aliponisikia nikifundisha ndipo alianza kuchukua hatua

*MFANO WA TANO*
Naomba niombee niliota nang'atwa na mbwa mkono  wa kushoto na sasa naanza kusikia maumivu hadi kwenye bega na nasikia ganzi.

*MFANO WA SITA*
Niliota nyoka kaingia mguu wangu wa kushoto  na mguu wukaanza kupata shida alipata ganzi na akiingia kwenye maombi tumbo linajaa na kufura

*MFANO WA SABA*
Kuna mtu alianidika kuwa anaota mara kwa mara akiteleza kuangukia kwenye shimo au maji na mguu huo ndio anateleza kwanza .

Baada ya miezi kadhaa ule mguu ambao ndio unatanguliza  ulipata shida na ndipo  aligundua kuwa unakidonda..

Mwingine aliota kameza buibui na baada ya muda alianza kukohoa na  kazunguka kila hospital  ili kutafuta dawa kwa sababu kifua kinamsumbua na haponi. Baada ya kusikia somo hili ndipo alianza kuhusianisha na ndoto aliyoota na akatuandikia

👉ushuhuda wa mama  aliyekuwa na binti yake alikuwa anachemea mguu na walikuja kunisalima nilipokuwa nje ya hospitali moja hapa nchini na nilisikia kumuuliza na alinieza na alisema kaota ndoto kuwa alikuwa anacheza mpira na alipopiga mpira kwenye ndoto aliumia na alipoamka akawa  anachechemea. Na hospitali walipopima hawakuona kitu.
Na nilimuombea na baada ya maombi alipona..

*Kuna hatua za kijumla za namna ya kufanya au kuomba*

1.Lazima kuomba toba kwa ajili ya mlango uliofunguka na kuruhusu ndoto kuleta mashambulizi. Kwa hiyo usijihesabie haki ili umeota ndoto na ikaleta madhara ina maana kuna mlango hapo uko wazi

Kazi ya toba ni .
i)Kuondoa uhalali kwa kiroho wa shetani kukutesa.

ii) Mungu kukusaidia/kupata  uhalali wa kukusaidia.

Shetani ili kukushambulia huwa anashambulia kihalali/ kwa hiyo na wewe ili kupambana nae inabidi umuondolee uhalali.

2.Nyunyiza damu ya Yesu kwenye eneo uliloshambuliwa..
Mawazo ombea fikra zako
Sikio
Mguu
Fikra
Tumbo.

👉Inategemea ni eneo gani. Kazi ya damu ya Yesu ni nyingi.
Damu inaongea
Damu inaondoa
Damu inasafisha.

👉Kuna mtu alinitumia picha kwenye whatsapp na alikuwa na alama ya kung'atwa na nyoka na meno .lazima unyunyize damu ya Yesu hapo. Na sumu hiyo iondolowe hata kama sio ulimwengu wa mwili basi ulimwengu wa roho .

Damu inakomboa
Damu inazuia
Damu inafungua

3.Kemea roho za kipepo zilizoingia na mifupa ilivyotetemeka.

👉Limejifunua kwa picha ipi. Mfano yule wa nyoka kemea pepo la nyoka.
Buibui kemea bui bui au wanyama kemea  kila picha ni roho.

Kama usipoona picha  angalia kazi iliyofanyika  kama unajiona umekufa kemea roho ya mauti.

4.Omba Mungu akuponye maeneo yote yaliyopata madhara kwa kupitia ndoto hiyo.

Mawazo Mungu aponye.
Hofu Mungu aondoe hofu na akupe amani.

Na Mungu atakupo6nya katika eneo ulilopata shida..

Mwingine aliona nyoka kaingia kwenye biashara na hakumtoa nyoka na baadaa yaa pale business  ikafa.

Na mama mmoja aliota ndoto nyoka kapita tumboni kwake na ndoa yake ilipata shida

Na kuna mtu aliotaa mtu kachukua pochi ndogo ndani ya begi na alipoamkaa ile pochi haijarudi. Na alipoenda ofisini alibadikishiwa kazi na alishwa cheo. Yamkini alisema ntaomba kesho na usiku tu kufika asubuhi Tayari mambo yamebadilika

Watu wanota wanakula vitu na watu waliokufa.. na zoezi lilifanyika kuombea hali hiyo.

Si kila kula kwenye ndoto ni ishara mbaya.

Unakila na nani wapi  saa ngapi na kwa ajili ya nini. Na kama wana israel walikula chakula baada ya kuabudu ndama. Kile kilikuwa ni sakramenti kwa miungu

Utakuta kama wenzio wanataka kukupeleka kwenye agano  wanakupeleka kula chakula ambacho hakijakaa vizuri kwenye ndoto ..

Pia unaweza andika ndoto yako na kuituma ili iombewe na utampa mhudumu au andika kwa msg kwa namba za huduma.

Chukua namba hizo na andika ujumbe wa msg kwenda namba hizo  kwenye link hii.  http://www.mwakasege.org/kuchangia.htm

Au andika barua pepe angalia katika link hii.  http://www.mwakasege.org/mawasiliano.htm

Pia nenda kwenye ukurasa wa Facebook na andika kwenye *inbox*   https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/

Hakikisha unampata huyu Yesu hakiisha unaokoka na unakuwa na mahusiano mazuri na Mungu. Wokovu sio dini mpya bali unajenga uhusiano wako na Yesu.

Bonyeza maandishi haya kuungana na sala iliyofanyika uwanjani.

http://www.mwakasege.org/mafundisho/okoka.htm

Baada ya hapo soma kitabu cha Hongera kwa kuokoka.

http://www.mwakasege.org/mafundisho/hongera/utangulizi.htm

*PIA SOMO HILI LA NDOTO LINAENDELEA FACEBOOK KWENYE UKURASA WA MWL MWAKASEGE PIA FUATILIA ILI UPATE MWANGA IKIFIKA KESHO UWE NA UELEWA ANGALAU KWA SEHEMU*

BONYEZA MAANDISHI HAYA.            https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/

RADIO ZINAZORUSHA

SEMINA LIVE DODOMA YA MWL MWAKASEGE

2– 9 APRIL, 2017

#KUANZIA SAA 10 HADI SAA 12 JION

#FREQUENCY & #COVERAGE
1. SAUTI YA INJILI – MOSHI
Arusha – 96.1
Moshi – 92.2
Same – 100.4
Rombo – 96.4
Tanga – 102.6
Mlalo Tanga – 96.7
Manyara – 102.9
Morogoro – 99.9
96.1 – Arusha, babati, karatu, mtowambu, musoma vijijini.
96.4 – Taveta, Rongai, Voi
102.6 – Unguja na Pemba, Mombasa
102.9 – Dodoma ( Kondoa, Chemba, Chamwino, Kibaigwa)
99.9 – Kiluvya, Rufiji, Pwani, Tegeta, Ubungo, Manzese, Mbezi, Ruaha, Lindi (Daraja la Mkapa).
www.sautiyainjili.org

2. HHC ALIVE FM – MWANZA.
91.7 FM
Mwanza, Simiyu, Mara, Shinyanga, Geita na Kagera.

3. BARAKA – MBEYA.
107.6 FM
Mbeya, Njombe (Siyo yote), Songwe (Kidogo), Rukwa – kidogo, Iringa baadhi ya maeneo (Mafinga).

4. INFO – MTWARA.
92.1 FM
Mtwara, Lindi ( Maeneo ya vijijini haisikiki vizuri)

5. REDIO CG FM
  89.5FM

- Tabora, Kigoma, Katavi, Singida

6 REDIO UZIMA YA DODOMA 94.0

-Dodoma,Babati,Iringa na Singida

7.RADIO MPANDA FM 97.0

Katavi, baadh ya maeneo ya Tabora

8.RADIO BUNDA 92.1
-Mara, Kagera,Simiyu

9.Rungwe Fm 105.7
TUKUYU,KYELA BAADHI YA MAENEO YA NJOMBE, MBOZI,

Youtube

https://youtu.be/dBYwy7T8pCs

USTREAM

http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry

Kicheko online Radio

http://169.255.114.200:8080/listern.pls?sid=1

http://udmcf.org/2017/04/02/listen-kicheko-radio/

www.mwakasege.org
www.kicheko.com

WAJULISHE NA WENGINE.
Credit to

FELIX MBWANJI

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.