Watazame Mayatima na Wajane Katika Dhiki Yao | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Sunday, February 7, 2016

Watazame Mayatima na Wajane Katika Dhiki Yao

Kutunza Mayatima na Wajane Leo

HAKIKA MOYO WANGU PIA KATIKA MAISHAYANGU YA HAPA DUNIANI MIMI PAMOJA NA FAMILIA YANGU TUTA MTUMIKIA BWANA KWA KUWASAIDIA WAHITAJI WA MAMBO MBALIMBALI

 KWA KULIONA ILO MIMI DAMAS ANTHONY AMBAYE NI MDAU WA MAENDELEO YA JAMII NAPENDA KUWALIKA WADAU WENGINE KUJITOA KWA AJILI YA KUWASIDIA WENGINE WENYE UHITAJI.

 

Ni wazi kabisa kwamba tunaishi katika ulimwengu usio na upendo. Mtume Paulo aliandika hivi kuhusu watu ambao wangeishi katika “siku za mwisho”: “Nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo zitakuwa hapa. Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, . . . wasio na shauku ya kiasili.” (2 Timotheo 3:1-3) Maneno hayo ni ya kweli kabisa.

 



HALI ya maadili ya siku hizi ni mojawapo ya sababu zinazofanya watu wengi wakose huruma. Watu wengi hawajali wengine, na baadhi yao hawajali hata watu wa jamaa yao wenyewe.








 

 

Jambo hilo linaathiri wengi ambao wamekuwa maskini kwa sababu mbalimbali. Idadi ya wajane na mayatima inaongezeka daima kwa sababu ya vita, misiba ya asili, na wakimbizi wanaotafuta makao. (Mhubiri 3:19) Ripoti moja ya Hazina ya Watoto ya Umoja wa Mataifa yasema hivi: “Zaidi ya [watoto] milioni 1 wamepoteza wazazi au kutenganishwa na jamaa zao kwa sababu ya vita.” Pia, kuna mama wengi wasio na wenzi na mama ambao waume zao wamewataliki au wamewaacha. Mama hao wana kazi ngumu ya kujiruzuku na kulea watoto wao. Hali ni ngumu zaidi katika nchi zenye matatizo ya uchumi. Katika nchi hizo watu wengi ni maskini sana.

 

Je, kuna tumaini lolote kwa wale ambao wanateseka? Wajane na mayatima wanaweza kusaidiwaje? Je, tatizo hilo litakuja kutatuliwa?

Utunzaji Wenye Upendo Katika Siku za Biblia

Katika siku za Biblia wale ambao walimwabudu Mungu, walitunza wajane na mayatima na kutosheleza uhitaji wao wa kimwili na wa kiroho. Waisraeli walipovuna nafaka au matunda yao, hawakuruhusiwa kukusanya mavuno yaliyobaki shambani. Waliamriwa wasichume mara ya pili. ‘Mgeni, yatima, na mjane’ waliachiwa yaliyobaki. (Kumbukumbu la Torati 24:19-21) Sheria ya Musa ilisema: “Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.” (Kutoka 22:22, 23) Katika Biblia wajane na mayatima huwakilisha kwa kufaa watu maskini kwa kuwa mume na baba, au wazazi wote wawili wanapokufa, huenda waliofiwa wakawa maskini. Ayubu alisema hivi: “Nalimwokoa maskini aliyenililia; yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.”—Ayubu 29:12.

 

Kutunza waliokuwa wanateseka na waliokuwa wenye uhitaji kwa sababu walikuwa wamefiwa na wazazi au wamefiwa na mume, kulikuwa sehemu muhimu ya ibada ya kweli katika siku za mapema za kutaniko la Kikristo. Maneno yafuatayo yaliyoandikwa na mwanafunzi Yakobo yanaonyesha kwamba aliwajali sana wajane na mayatima: “Namna ya ibada iliyo safi na isiyo na unajisi kwa maoni ya Mungu wetu na Baba ni hii: kutazama mayatima na wajane katika dhiki yao, na kufuliza kujitunza mwenyewe bila doa kutokana na ulimwengu.”—Yakobo 1:27.

 

Mbali na kutaja wajane na mayatima, Yakobo pia alihangaikia sana wengine waliokuwa maskini na wenye uhitaji. (Yakobo 2:5, 6, 15, 16) Mtume Paulo aliwahangaikia vivyo hivyo. Paulo na Barnaba waliagizwa ‘wakumbuke walio maskini,’ walipotumwa wahubirie mataifa. “Jambo hilihili mimi pia nimejitahidi sana kwa bidii kulifanya,” Paulo aliweza kusema kwa dhamiri safi. (Wagalatia 2:9, 10) Simulizi kuhusu utendaji wa kutaniko la Kikristo muda mfupi baada ya kuanzishwa, lasema hivi: “Hapakuwa hata mmoja mwenye uhitaji miongoni mwao . . . Nao ugawanyaji ulikuwa ukifanywa kwa kila mmoja, kama vile alivyokuwa na uhitaji.” (Matendo 4:34, 35) Naam, mpango wa kutunza mayatima, wajane, na maskini uliokuwapo katika Israeli la kale hutumika pia katika kutaniko la Kikristo.

Bila shaka, msaada uliotolewa ulikuwa wa kadiri na kulingana na uwezo wa makutaniko. Fedha hazikutumiwa ovyoovyo, na wale waliosaidiwa walikuwa na uhitaji wa kweli. Wakristo hawakupaswa kujinufaisha isivyofaa na mpango huo, wala kutaniko halikupasa kutwikwa mzigo huo isivyo lazima. Paulo alitoa maagizo yaliyo wazi kuhusu habari hii katika andiko la 1 Timotheo 5:3-16. Andiko hilo laonyesha kwamba ikiwa watu wa ukoo wa yule mwenye uhitaji walikuwa na uwezo wa kumsaidia, basi, ilikuwa daraka lao kufanya hivyo. Wajane maskini walihitaji kutimiza matakwa fulani ili kustahili kupokea msaada. Hayo yote ni mpango wa busara wa Yehova kutunza wale wenye uhitaji. Hata hivyo, yanaonyesha pia kwamba lazima kuwe na usawaziko ili mtu yeyote asijinufaishe isivyofaa kwa mpango huo.—2 Wathesalonike 3:10-12.

 

Kutunza Mayatima na Wajane Leo

Kanuni zinazohusu kuwajali na kuwasaidia wanaoteseka, ambazo zilifuatwa na watumishi wa Mungu zamani, zinafuatwa hata leo katika makutaniko ya Mashahidi wa Yehova. Upendo wa kidugu ni sifa inayowatambulisha kama Yesu alivyosema: “Kwa hilo wote watajua kwamba nyinyi ni wanafunzi wangu, mkiwa na upendo miongoni mwenu wenyewe.” (Yohana 13:35) Ikiwa baadhi ya Wakristo ni wenye uhitaji au wamepatwa na misiba au wameathiriwa na vita au mapambano ya kiraia, ndugu wao ulimwenguni pote wanajitahidi kutoa msaada wa kiroho na wa kimwili. Acheni tuchunguze visa vya siku zetu ambavyo vinaonyesha kile kinachofanywa leo kuhusiana na kusaidia wajane na mayatima.

 

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.