'KUELEKEA 2030
TOKOMEZA UMASIKINI KWA UZALISHAJI ENDELEVU NA MATUMIZI YENYE TIJA'
Salam kwenu ndugu zangu.
Kwa niaba ya Shirika la Maendeleo ya Vijana la Restless Development napenda kuwapa taarifa kuwa leo tarehe 12.08.2016 ni siku ya Kimataifa ya Vijana na kuwa ni wakati wa vijana kuadhimisha kwa kutengeneza mijadala inayozungumzia masuala mbalimbali yanayowagusa zikiwemo fursa pamoja na changamoto hasa katika ngazi ya kitaifa.
 |
DAMAS ANTHONY WA RESTLESS DEVELOPMENT VOUNTEER ICS |
Maadhimisho ya mwaka huu yamebebwa na dhana pana na endelevu ya kujadili
msingi wa vijana kama chachu ya mikakati ya kutokomeza umaskini kupitia
maendeleo endelevu ya dunia. Tunatambua nguvu kazi kubwa ya watanzania
ni vijana ambapo zaidi ya 65% ya nguvu kazi yote ya taifa inamilikiwa na
vijana. Ni wajibu wa kila mdau wakiwemo vijana kama wanufaika wakuu
kuweza kutambua mchango wao katika kukipa nafasi kizazi hiki ikiwa pia
ni kudadavua mchango na nafasi yao katika kuhakikisha Tanzania inakuwa
nchi ya uchumi wa kati na inayoongozwa kwa misingi ya ukuaji wa viwanda
kupitia mpango wa maendeleo serikali wa miaka mitano na dira ya 2025.
 |
Damas akiwa katika moja ya Shule ya Sekondari Miyomboni |
Kwa kutambua dhana hii vijana wanayataja mambo makuu wanayokumbana nayo
kama changamoto; Ukosefu wa ajira -zaidi ya asilimia 50 ya vijana hawana
ajira na kwamba hawapo shuleni pia; ushiriki katika ufanyaji maamuzi -
ni aslimia 18.3 tu ya vijana hushiriki katika vikao vya serikali za
mitaa; huduma za afya ya uzazi - vijana ndio wanabeba idadi kubwa ya
maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI, wanaathiriwa na matatizo makubwa
ya unyanyasaji wa kijinsia, upatikanaji wa huduma rafiki za afya ya
uzazi kwa vijana.
Kwa kuwa hayo yote ni mambo yanayomgusa kijana, upo wajibu wa msingi kwa
wadau wote tunaobeba bango la maendeleo ya vijana ikiwemo serikali kama
mdau mkuu kuhakikisha vijana wanatumia nguvu yao kwa tija katika
kuhakikisha tunajipatia maendeleo stahiki na yenye tija. Ni lazima
tuhakikishe taarifa sahihi zinawafikia vijana, ni ni wajibu wetu pia
kuhakikisha vijana wanashirki kikamilifu katika utekelezaji wa mpango wa
serikali wa maendeleo ili tufikie lengo la kuwa nchi ya uchumi wa kati
lakini kwa mapana kufikia malengo ya maendeleo ya dunia yaani Sustainable Development Goals.
 |
Allen Muhangwa mdau wa maeendeleo pia mkurugezi wa taasisi ya kilimo na msaada wa kisheria Tanzania Vijana Agrics & Paralega TAVAPA pamoja na wanfunzi wa shule ya sekondari Miyomboni |
Wito ni juu ya kuungana na kuhakikisha tunajielekeza 'kwa pamoja' katika
kuhakikisha tunatumia "Nguvu Kazi Ya Ujana" katika kushawishi ujana
kiwa sehemu muhimu na mstari wa mbele wa maendeleo na mabadiliko katika
taifa letu.
 |
katika moja ya Darasa shule ya sekondari Miyomboni |
 |
Picha pamoja ya International Citizen Service volunteer (ICS) |
 |
Mr Andrew na Franco katika kituo cha watoto yatima Tosamaganga |
 |
Upendo |
 |
Denis akiwa na moja wa mtoto katika kituo cha kulea watoto yatima |
 |
Anthony Damas akiwa mmoja wa watoto katika kituo cha Kulea watoto yatima mkoani Iringa |
 |
Mr. Denice Simeo afisa miradi ofisi za Restless Development Iringa akionyesha kauli mbiu katika t-shirt ya Damas |
Nawatakia maadhimisho mema tafadhali tushirikiane kuufikisha ujumbe huu kwa wote.
'KUELEKEA 2030
TOKOMEZA UMASIKINI KWA UZALISHAJI ENDELEVU NA MATUMIZI YENYE TIJA'
Toa Maoni Hapa Chini