Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
KWA WASIOJUA:
MAJUKUMU MAKUU YA RSA TANZANIA NI:
1. *KUELIMISHA JAMII;*
2. *KUKEMEA NA KURIPOTI MATUKIO YANAYOATHIRI USALAMA BARABARANI;*
3. *KUSHAWISHI MABADILIKO YA TABIA, SHERIA NA SERA.*
Katika kuelimisha jamii RSA TANZANIA inatoa mada mbalimbali za kuelimisha jamii, inaendesha mijadala, inajibu maswali ya mabalozi na wadau wengine, na inaendesha kampeni mbalimbali ndani na nje ya mtandao. Pia inawaelimisha mabalozi wake yenyewe ili wawe mabalozi wazuri kwa wengine bila ubabaoshaji.
Katika kukemea na kuripoti, Mabalozi wa usalama barabarani mara waonapo tukio au kitendo chochote kibaya humkemea mhusika aache mara moja kufanya jambo hilo na asiposikia humripoti mahala husika au kupitia namba 0682887722. Wakati mwingine mabalozi wasipokuna na nafasi ya kuongea na mhusika basi humripoti moja kwa moja na hatimaye hatua kuchukuliwa na mrejesho kutolewa.
Matukio yanayoripotiwa ni pamoja na hali ya barabara, mwenendo wa.magari pamoja na mwenendo wa watumiaji wengine wa barabara na wasimamizi wa sheria. Ndio maana katika kuripoti na kukemea sisi huwaripoti na kuwakemea si tu madereva bali pia hata wasimamizi wa sheria kama vile askari, wamiliki, na Sumatra ili watende kazi zao kwa ufanisi, weledi na kutojisahau. Sawa kabisa na tunavyofanya kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara tukiwemo sisi wenyewe mabalozi. Mabalozi kwa mabalozi hukemeana na kuripotiana pia.
Katika kushawishi mabadiliko ya tabia sheria na sera.
RSA Tanzania hushawishi watu wabadilike kimtazamo na kitabia hasa wawapo barabarani na waanze kujali maisha yao na ya wengine. Mtu anayeshawishiwa kunadili tabia hushawishiwa pia kuwa balozi.
Mabalozi hupitia sheria na sera mbalimbali na kuona kama zinakidhi mahitaji ya sasa. Na pale kwenye mapungufu basi mabalozi hushawishi kubadilishwq kwa sheria hizo. Tunatoa mawazo mbalimbali kwa vyombo vya usimamizi wa sheria juu ya namna ya kuboresha usimamizi wa sheria, tunatoa mapendekezo ya namna sheria inavyopaswa kuwa pamoja na kushiriko katika michakato mbalimbali ya kimaamuzi, kisera na kisheria.
HII NDIO RSA TANZANIA ambapo tunaamini *USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE*
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.