Tanzania will witness the solar eclipse which
according to astronomy experts Tanzania in particular Rujewa Area in
Mbeya region located in Southern Tanzania will be the best site for
viewing this fascinating event where the sun’s disk will change to a
ring.
Today, the moon will pass in front of the sun
The Eclipse is expected to begin at 10:01am to 01:45pm.
Kupatwa kwa jua au Annular Eclipse hutokea pale jua na mwezi zinapokuwa kwenye mstari mmoja ambapo umbo la mwezi linaonekana kuwa dogo zaidi kuliko umbo la jua.
Wanayansi wanasema kwamba September 1, 2016 Tanzania ndio itakuwa sehemu pekee ambayo kupatwa huko kwa jua kutaonekana vyema na kuwavutia watalii wengi.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya Uingereza imeripoti kwamba kupatwa huko kwa jua kutaanza kwenye bahari ya Altantic, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Tanzania, Msumbiji, kisiwa cha Madagascar kisha kwenye Bahari ya Hindi.
Wataalamu wanasema kwamba miongoni mwa maeneo yatakayoonekana vizuri kwa kupatwa kwa jua ni Mbeya na Tunduru, Ruvuma ambapo tukio hilo litachukua dakika 3 hadi dakika 7.
Today we are starting a new month
Today is the day of solar eclipse
Today is the day we are starting the last quarter of the year
TUKIO kubwa la angani litatokea tarehe 1 Septemba mwaka huu na kusababisha macho mengi duniani kote kuelekezwa Tanzania.
Tukio hilo linatazamiwa kuanzia saa 4:17 asubuhi hadi 7:56 adhuhuri.
Hili si lingine bali ni la kupatwa kwa jua ambapo linatazamiwa kufanyika
katika usawa wa anga ya Tanzania. Mashabiki na wanataaluma wa anga
kutoka duniani kote pamoja na wanasayansi, wanafunzi pamoja na jamii ya
Tanzania wataelekea Rujewa, kusini mwa Tanzania, karibu na Mbeya,
kushuhudia duara la Jua linavyobadilika kuwa mithili ya pete.
Nchini kote Tanzania, siku hiyo mamilioni ya watu watashangaa kuona
Jua kali la utosini likimegwa kwa zaidi ya asilimia 90 kwa kufunikwa na
mwezi katika tukio hilo la kupatwa kwa jua. Hali hiyo italiacha jua
lionekane kama pete au hilali nyembamba au mithili ya mwezi mwandamo.
Watu wanaoishi ndani ya ukanda wenye upana wa kilometa 100
unaokatisha kusini mwa Tanzania, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya-
Kongo kuelekea Katavi, Mbeya, Ruvuma hadi Masasi na kuingia Msumbiji,
siku hiyo wataona jua kama duara jembamba mithili ya pete, kwa vile
asilimia 98 ya jua katika maeneo yao litakuwa limejificha nyuma ya
mwezi. Kupatwa huko kwa jua kunaweza kuonekana kwa usalama na
watazamaji, lakini inabidi kutumia vichuja maalum vya mwanga wa jua.
Tukio la kupatwa kwa jua ni la kusisimua na la nadra sana kutokea
katika maisha ya mtu na baadhi ya dini kama Uislamu zinawataka watu
wakati wa kipindi hicho kuwa kwenye swala maalumu. Vijana wengi katika
kizazi hiki kipya watakuwa hawajaona tukio hili na hivyo ni tukio
litakalowasisimua na wanafunzi ambao wamekuwa wakijifunza mashuleni
watapata ushahidi wa moja kwa moia siku hiyo.
Wengine watazidi kujifunza sayansi ili kuelewa kwa nini kinatokea
kile wanachokiona. Kwa hiyo tukio hili linaweza kutumiwa na shule na
taasisi za elimu kuendeleza sayansi na kuvuta wanafunzi kujiendeleza
kisayansi na hasa kuelewa mizunguko mbalimbali iliyopo katika mfumo wetu
wa sayari pamoja na anga za juu kwa ujumla. Bila shaka wataongeza
uelewa wa sayansi na umuhimu katika kuelewa maumbile ya ulimwengu wetu.
Kupatwa huku kwa jua kutatokea siku ya Alhamisi ambapo wanafunzi
wengi watakuwa shuleni na litatokea wakati wa masomo. Kwa vile mchakato
wote utaendelea kwa masaa manne hivi, kati ya saa 4:00 asubuhi hadi saa
8:00 mchana wanafunzi wataweza kushirikiana kuangalia, kusimulia na
kujadili tukio ili kulielewa vizuri na kuandika ripoti madarasani mwao.
Tukio jingine kubwa la kupatwa kwa Jua kama hili halitatokea miaka 15
ijayo, kwa hiyo tunahitaji kutumia fursa hii kwa ukamilifu kujifunza.
Ili kuangalia kupatwa huko, kila mmoja atahitaji kutumia kikinga
macho kinachochuja mwanga wa Jua kiitwacho Kitazamia Jua. Nini hatari
kuangalia jua lililopatwa kwa macho moja kwa moja au hata kutumia
vichujio vingine vya kiza vilivyotengenezwa mitaani. Kitazamia Jua
maalumu ni kifaa rahisi kilichotengenezwa kutokana na kichuja nguvu ya
jua ambacho kinaondoa mionzi haribifu kwa asilimia 99.999.
Miwani hiyo maalumu ya Jua inaweza kutengenezwa Tanzania kwa gharama
isiyozidi Sh 500 kila moja, ikiwemo kuchapa fremu za kadbodi na kichuja
nguvu ya jua (polymer filter) kinachoagizwa kutoka Marekani.
Mwandishi wa makala haya, Dk Noorali Jiwaji wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Make *evaluation* All the plans and achievements and challenges up to this day.
Remember in *most cases* when you are fine and successful
you belong to the Society and other people. But when you are weak, Sick
or dead then you belong to the family.
*Try to speak to the family, pray, plan and try to do good for the family* in this month
Remember a good Church, a good Nation and good leader or bad as well as a good or bad society comes from the family.
Ombea familia na ujiombee wewe mwenywe. Panga kufanya kitu
kwaajili ya kurekebisha mambo yasiyoenda vizuri katika familia zetu na
pia tushughulikie mambo yasiyofaa katika Nidhamu binafsi, in our
personal habits.
Toa Maoni Hapa Chini