BWANA YESU ASIFIWE!
Ndugu yangu katika Kristo karibu tujifunze somo hili MISINGI YA WOKOVU NI IMANI, Pia tutaangalia baadhi ya faida za imani.
IMANI NI NINI? Waebrania 11:1 “Basi imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”.
FAIDA YA IMANI
a) Kuleta ushindi
Marko 9:23 “Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yanawezekana kwake aaminiye.
b) Kuleta uponyaji
Luka 5:17-26 “20: Naye alipoiona imani yao, alimwambia, Ee rafiki,
umesamehewa dhambi zako. 24b: Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako,
ukaende zako nyumbani mwako”.
c) Kututia nguvu
Yuda 1:20 “Bali niyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu”.
d) Inatusaidia kuwaleta wenye dhambi kwa Yesu
Matendo 11:24 “Maana alikuwa mtu mwema amejaa Roho Mtakatifu na imani; watu wengi wakaongezeka upande wa Bwana”.
e) Hutuwezesha kustahimili mateso
Matendo 14:22 “wakifanya imara roho zao za wanafunzi na kuwaonya wakae
katika ile Imani, nay a kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu
kwa ajili ya dhiki nyingi”.
Ili uweze kustahimili na imani lazima neno likae ndani yako.
f) Husafisha mioyo yetu iwe safi
Matendo 15:9 “wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani”.
g) Hutuwezesha kupokea msamaha
Warumi 3:25 “ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya
imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya
kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia
kufanywa”.
h) Hutufanya wenye haki mbele za Mungu
Warumi 5:1 “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo”
i) Hutuletea amani
Warumi 5:1 “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo”
j) Hutupa uvumilivu (saburi)
Yakobo 1:3-4 “Ndugu zangu hesabuni ya kwamba ni furaha tupu, mkiangukia
katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu
huleta saburi”.
k) Hutuepusha na dhambi
Warumi 14:23 “Lakini
aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula
kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi”.
l) Hutupa ujasiri
Waefeso 3:12 “Katika yote tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini”.
m) Huleta umoja
Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na
kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika
kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo”.
n) Hutulinda na mashambulizi ya shetani
Waefeso 6:13-18 “zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya Yule mwovu".
Kazi ya ibilisi ni kuharibu mahusiano yako na Mungu ili kukuondoa
kwenye imani. Imani ndiyo inayotusaidia kusimama kinyume na hapo
utachanganyikiwa. Hakuna kitu kisicho na changamoto bali Mungu
anatusaidia kuweza kusimama.
Mbarikiwe sana
By Nyandula Mwaijande.
Source
Toa Maoni Hapa Chini