SEMINA YA NENO LA MUNGU- MWL MWAKASEGE | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Wednesday, January 25, 2017

SEMINA YA NENO LA MUNGU- MWL MWAKASEGE

🌂8⃣ *SEMINA YA NENO LA MUNGU ARUSHA UWANJA WA RELI*

*TUMIA AKILI KIROHO ILI UFANIKIWE KIMAISHA*

*NA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE*

*22 - JANUARY - 2017*

Bwana Yesu afiwe leo ni siku yetu ya nane na ndio tunamaliza semina. Tumekwenda vizuri kabisa kwa siku saba na sasa tunaeleka mwishoni. Jitahidi pata kanda za semina hii na zitakusaidia sana. Kwa maelezo wapi pa kupata kanda tembelea www.mwakasege.org. Semina inayofuata ni Dar es Salaam tar 29 January 2017 (Semina ya siku moja) diamond jubilee kuanzia saa nane hadi saa 12.30 jion. Pia tutakuwa live kwa (redio tutawaambia na pia kwa njia ya internet (Youtube, ustream na kicheko redio) 

Na angalia yale malengo mawili kama yamefikiwa tuliyoyaweka wakati tunaanza semina. Tathimini na jitathimini na wewe pia kwa ajili ya kuona kama umepata lile lengo la semina.
*1. Kuweza kuona umuhimu wa akili na sehemu yake katika maisha ya kiroho*
*2. Ili uweze kutumia akili kiroho ili ufanikiwe kimaisha* 

*HAKIKISHA SOMO HILId UNALIWEKA KWENYE MATENDO ILI UFANIKIWE MAANA IMANI BILA MATENDO HAIZAI KWA HIYO SOMA AU SIKILIZA NA KUSIKILIZA HADI SOMO HILI LIKUSAIDIE, KUNA SHIDA HUJAELEWA OMBA MUNGU AFUNUE AKILI ZAKO ILI UELEWE, OMBA KWA KUNENA KWA LUGHA HADI UONE UNAVUKA. MAANA UTENDEJI KAZI WA AKILI ZAKO NI WA MUHIMU SANA KUKUFANIKISHA*

>>Pia tulikwenda kwa kutazama ile mistari mikuu ya _Mithali 3:19 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi; *Kwa akili zake akazifanya mbingu imara*_kwa hiyo Mungu anakili.  Sasa unganisha na _1 Yohana 5:20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, *naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli*, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele._

>>Hivyo basi tumia akili zako ili ufanikiwe, kwa maana hiyo Katika _Waebrania 5:14 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, *ambao akili zao*, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya._ Lakini matumizi ya akili isiwe sababu ya kuweka tegemeo ndio maana biblia inasema _Mithali 3:5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, *Wala usizitegemee akili zako mwenyewe*_.  Lakini pia kuwa na angalizo hilo haina maana usizitumie akili zako. Ni jambo la muhimu sana kuweza kutumia akili zako ipasavyo kama Mungu anavyotaka. Kwa sababu hiyo kuwa na imani haina maana akili zisihusike, hakikisha akili zinafanya kazi kawaida sana.

>>Akili zinaweza kuharibika na kwa sababu utendaji wa akili unakwenda sambamba na fikra, nazo zikiharibika. Mwisho wake ni kuwa Mungu kutotumia akili zilizoharibika na ndio maana katika _Warumi 1:28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, *Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa*, wayafanye yasiyowapasa._ Mungu  akimuacha mtu ajiendee anavyotaka inakuwa ni hatari sana kwake na sababu ni sawa na gari linalotembea usiku bila taa maana neno la Mungu nitaa, uwe na uhakika tu litapata ajali.

>>Mpaka jana tulikuwa tumeangalia point tano za namna ya kufanya ili akili zako zirekebishwe na zifanye kazi ipasavyo na leo nataka tusogee mbele ili tuangalie point zingine.

>>Jana nilianza kwa kukuonesha mfano wa mwana mpotevu. Na sasa nataka tuangalie mambo muhimu ya kujifunza kutokana na habari ile.

*Point ya Kwanza* *SI SUALA LA KUBADILISHA ENEO UNALOISHI ILI UFANIKIWE BALI BADILISHA AKILI ZAKO YAANI MTAZAMO (FIKRA)*
Maana tuliona mwana mpotevu alipoondoka kwa baba yake na kwenda nchi ya mbali na alitegemea afanikiwe na haikuwa hivyo. Ndio maana mtu akiwa hafaniki hapa Arusha anajua anaweza hamia Dar Es Salaam. Na anashangaa hafanikiwi basi shida kubwa ni  akili zake sio eneo maana kuna watu katika eneo hilo hilo wanafanikiwa isipokuwa yeye.

* Point ya Pili*  *SI SUALA LA KUBADILISHA CHANZO CHA MAPATO YAKO, AU KAZI BILA KUBADILISHA AKILI ZAKO*
Maana kuna wengine wanabadilisha kazi kama shati na wanashangaa maisha yao yako plae pale. Wanahama kutoka kazi moja kwenda kazi nyingine kwenda  akili zile zile.Tuliona mwana mpotevu alibadilisha chanzo cha mapato yake kutoka hela za urithi kwenda kulisha nguruwe na hakufanikiwa kwa sababu akili yake ile ile ndiyo ilikuwa inafanya kazi hadi pale alipo*zingatia moyoni mwake yaani alipofikiri yaani alipotumia akili zake.

* Point ya tatu* *SI SUALA LA UWINGI AU UCHACHE WA HELA ULIZONAZO ILI KUBORESHA MAISHI YAKO BALI NI AKILI YAKO*
Mwana mpotevu alipokuwa na hela nyingi bado maisha yake yaliendelea kuwa mabaya na hata alipokuwa na hela kidogo (alipokuwa analisha nguruwe napo bado maisha yake yaliendelea kuwa duni Zaidi, hadi pale alipobadilisha namna ya kufanya na kufikir vizuri.  Maana kuna watu wanapesa kidogo na wanamaisha mazuri na kuna watu wanapesa nyingi sana na wanamaisha mabaya sana.

*HATUA YA 6* *WEKA KWENYE MATENDO/FANYIA KAZI NENO AU WAZO LA MUNGU ULILONALO MOYO MWAKO*
>>Wazo/neno likiingia ndani yako hakikisha unalitafakari sawa sawa  hadi likusukume kwenye matendo maana yake hadi uone njia yaani mikakati ya kiutekelezezaji . Angalia _Isaya 55:8-11 Maana mawazo yangu *si mawazo yenu*, *wala njia zenu si njia zangu*; asema Bwana. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma._

>>Kwa hiyo litafakari hilo wazo hadi liwe njia maana yake liwe mkakati wa kiutekelezaji, na ndio maana Mungu atakuletea mawazo mbali mbali. Na ndio maana anazungumza kwa habari za *mvua* yaani ni *Roho Mtakatifu* na *ardhi*  ni *Moyo wako* na *Mbegu* ni *Neno la Mungu* Hakikisha Mungu anashiriki katika utekelezi wake.

_Mathayo 7:24-27 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, *atafananishwa na mtu mwenye akili*, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa._

>>Yesu asilema yule anayesikia neno na kulifanyia kazi biblia inamwita ni mtu wa akili haijasema wa kiroho na anaposema *asikiaye hayo maneno yangu* maana yake neno ili litende kazi linabadilika na kuwa wazo na ndio maana neno linasema baba yako alitii maneno yangu maana yake alifuata mawazo yangu niliyompa. Na ili ufanikiwe unahitaji neno la Mungu maana neno ndio linakupa guarantee ya kufanikiwa ili uweze kusonga mbele.

*HATUA ZA KUFANYA ILI ULIFANYIE KAZI WAZO AMBALO MUNGU KAKUPA*
>>Hakikisha mawazo ambayo Mungu anakupa unayafanyia kazi, maana kuna wengine wanakufa na mawazo ndani yao na hata wakienda mbinguni, mbinguni wanakuonesha namna ulivyokuwa na mawazo mengi na mazuri ya kuweza kuwasaidia na wengine ili wavuke na unatamani urudi tena kama Yule Tajiri. Maana hapa duniani, Mungu alimpa akili ili aweze zitumia kwa ajili ya kuweza kutekeleza mawazo ambayo Mungu kakupa.

*1 Andika wazo, mawazo ambayo Mungu anakupa, hakikisha unakuwa na notebook  ili uweze kuandika*
>>Jenga nidhamu ya kuandika maana katika biblia Habakuki 2:1-4 Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habarif ya kulalamika kwangu. *Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji*. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia. Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.

>>Maana ukiandika inakuwa ni rahisi sana kukumbuka maana kuna wengine wanasema ntatunza kichwani lakini kanuni inasema *Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao* maana yake inote.

*2 Tafakari kwa kuombea mawazo hayo uliyo andika*
_Yoshua 1:8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, *bali yatafakari maneno yake mchana na usiku*, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana._

>>Bali maneno hayo yasiondoke kwenye kinywa chako maana ndiyo yanaumba yale uliyoyatafakari (si unajua dunia iliumbwa kwa neno na maandiko yanasema *Isaya 57:19 A) Mimi nayaumba matunda ya midomo*; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema Bwana; nami nitamponya.  (ndio maana biblia inasema yasiondoke kinywani mwako yaani uwe unayanena (affirm) sasa ukiyanena ndiyo yanakuwa yanaumba. Tunakwenda sawa sawa.

Kwa hiyo hakikisha Roho Mtakatifu anakusaidia na utasema Mwakasege hili neno nimelipata wapi Lipo kwenye  _Wagalatia 4:19 Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka *Kristo aumbike ndani yenu*_ haya yawe maombi yako kwa kadri utakavyokuwa unaomba kuna kitu ndani yako kinakuwa kinaumbika. Na kumbuka kuwa *Mungu hu-umba matunda ya midomo*

>>Hata mimi mwenyewe unakuta Mungu kanipa mawazo ya kuandika vitabu kama vitatu hivi. Baada ya hapo naendelea kutafakari na kuomba na kuomba na unakuta kati ya vile vitabu kimoja kinatokeza Zaidi kwa hiyo hicho ndicho naanza kukifanyia kazi.

*3 Hilo wazo lilopata nafasi moyoni mwako liandike kiutekelezaji au kimalengo ya utekelezaji* (Andika hatua za kutekeleza yaani njia
>>Maana biblia inasema katika Waebrania 11:1 kuwa  imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo na ni bayana ya mambo yasiyo onekana na Warumi 10:17 inatuambia basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo.  Na ukishalipa nafasi basi hakikisha hiyo imani yako unaiweka kwenye matendo.

Mandiko yanatuambia katika _Yakobo 2:17-26 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu. Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka._

_Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu? Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale. Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu_

_Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake. Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine? Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa_ 

>>Jambo lolote ili lionekane linahitaji kuwekwa kwenye matendo yaani akili yako ichanganye neno na mazingira  na Uwepo wa Bwana ili liweze kufanya kazi ndio maana ya imani katika matendo.  Katika Waebrania 4:1-3 Biblia inasema Wanaisrael walikwama kwenda Kanani kwa sababu ya kutoamini maana yake kushindwa kulitendea kazi neno lilowaambia waende katika ile nchi waliyoaahidiwa na Bwana.

*4 Tathmini Visima vya vya Ibrahimu vilivyokatika familia yako uweze kustawi kimaisha*
>> _Mwanzo 26:18 Isaka akarudi akavichimbua *vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye*; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye_

>>Tunaona namna visima vilivyokuwa vimefukiwa, huwa najiuliza sana ninaposoma habari hii kwa sababu wakati wafilisti wanavifukia walikuwa hawaoni umihimu wa visima hadi Isaka alipovifukua na ndipo wakaanza kugombania, na waligundua kuwa ili asije fukua na vingine waliona wasinyang’anye tena.

>>Nataka kukuuliza wewe mtu wa Mungu, je visima ulivyopewa na baba yako uliviacha kwa wafilisti wavifukie, je ile nyumba aliyokuachia baba yako au lile shamba au gari liko wapi , je umewaachia wafilisti wakati una visima. Mungu ni wa agano ina maana kuna mawazo aliyowapa kwa baba yako na anategemea wewe utekeleze na wewe umeyaacha na kuwaachia wafilisti. Nenda kafukue,  Ukisoma habari za Daudi _1 Nyakati  22:11-16 Sasa mwanangu, Bwana na awe pamoja nawe; ukafanikiwe, na kuijenga nyumba ya Bwana, Mungu wako, kama alivyonena kwa habari zako. Bwana na akupe busara na akili, akakuagizie juu ya Israeli; ili uishike torati ya Bwana, Mungu wako. Ndipo utakapofanikiwa, ukiangalia kuzitenda amri, na hukumu, Bwana alizomwagizia Musa juu ya Israeli; uwe hodari, na wa moyo mkuu; usiogope wala usifadhaike_
_Basi sasa, tazama, katika shida yangu, *nimeiwekea akiba nyumba ya Bwana, talanta elfu mia za dhahabu, na talanta elfu elfu za fedha;* na shaba na chuma isiyo na uzani; kwa vile zilivyo tele; miti tena na mawe nimeweka akiba, nawe utaweza kuongeza. Tena kwako kuna mafundi wengi, wenye kuchonga na kufanyiza kazi ya mawe na miti, na kila aliye mstadi kwa kazi yo yote; ya dhahabu, ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, hapana hesabu; basi inuka ushike kazi, naye Bwana na awe pamoja nawe_

>>Wenzetu nchi zingine unaona baba anaanzisha duka watoto wanakuja kuendeleza, bali hawali  au kuua sasa cheki baba yako au mama yako alipokuachia shamba je umelipelekea wapi? Kwa nini mzazi wako alikuwekea, usifikiri yeye alikuwa hana shida ya hela hapana bali alikuwa anaangalia ya mbele.  Usiwe na akili kama ya *mwana mpotevu ya kutumia mali na unamaliza zote akili yako inazinduka hela imeisha na kazi hauna na wazazi wameshakufa na inabaki historia tu.

*5 Weka muda wa kukamilisha jambo yaani deadline ya wazo ambalo Mungu kakupa kufanya*
>>Siku moja nilikuwa nafanya kazi ya serikali na kuna report nilikuwa naindaa kwa ajili ya kikao asubuh, sasa nilandika hadi usiku kufika saa tano nilichoka nikaomba Mungu anitia nguvu na nilimaliza. Baada ya kumaliza nilimshukuru sana Mungu kunisaidia kumaliza ile kazi. Sasa Mungu aliniletea neno ambalo nasema ilikuwa ni ngumi ya usoni. Alisema *Na kazi zangu zinakuwa na deadline na wakati ule nilikuwa naandika Kitabu cha kwanini *Bwana Yesu alituombea umoja* na nilikuwa sijaweka deadline.  Akili ilichanganya nilijua maana yake nini kuwa na deadline na nilibadilika kuanzia pale hadi leo kila kazi inakuwa na deadline.  _Wagalatia 6:9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho_ 

Pia MUNGU aliniambia kuwa kipindi nimekuambia soma kitabu cha Joshua ulisoma, nikasema ndiyo akasema angalia _Yoshua 1:1-2 Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa Bwana, Bwana akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema Musa mtumishi wangu amekufa; haya basi, *ondoka, vuka mto huu wa Yordani*; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli. _

>>Mungu anaweza shusha wazo ndani yako na inakutaka wewe uchukue hatua ili Mungu aanze kutembea na wewe katika kile alichokuagiza kufanya.

*6 Jiandae kupambana na upinzani dhidi ya wazo lako na utekelezaji wake*
_Mwanzo 26:18-22 Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye. Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika. Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye. Wakachimba kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna. Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi_

>>Hapa tunaona kila unapotaka kutekeleza kitu cha Mungu upinzani unainuka, na Isaka alipambana na wafilisti, ndio maana _Zaburi 23:5 *Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu*. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika_  kwa hiyo unapoanza kutekeleza cha Mungu jiandae kupamba na upinzani. Ndio maana biblia inasema Yesu alipingana na Petro _Mathayo 16:23 Akageuka, akamwambia Petro, *Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu*; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu_
>> *Ila jua kuwa mpinzani wa kwanza ni moyo wako acha kusingizia bali ondoa visigizio*

*7 Ingia agano na Mungu, kwa njia ya sadaka ilishiriki kiutekelezaji*
_Zaburi 50:5 Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu_

>>Kuna baadhi ya mambo hayaendi kwa sababu inatakiwa utoe sadaka Katika  _Mwanzo 15:8-18 Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitairithi? Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa. Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua._
_Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza. Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia. Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne. Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi. Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema. Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado. Ikawa, jua lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuru ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama. Siku ile Bwana akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati_

>>Unaona kuna baadhi ya mambo Mungu hawezi kukujibu si kwa sababu hustahili bali ndio utaratibu, jifunze kuachili sadaka kwa kila hatua, sio kwamba unanunua bali unaachilia imani yako kwa Mungu. Toka sadaka inayogusa yaani haijalishi ni kiasi gani ila imani unayoachilia. Usitoe kilichokizidi. Jifunze kutoa sadaka kwa kila msimu ambao Mungu anakupa, hata sisi kabla ya kufanya jambo lolote huwa kwanza lazima tutoe sadaka, kwa kila semina lazima tutoe sadaka kwanza ili tushirikiane na Mungu. Na wewe jifunze kufaynya hivyo hata kwa kila kitabu kabla hatujaanza kukiandika huwa tunatoa kwanza sadaka kwa Mungu.

>> sijajua kwako unataka ushirikiane na Mungu kwa namna gani.  Watu walimtolea Mungu sadaka hiyo na Mwl aliomba sana kwa Baraka za Mungu kwa watu na malengo yao kwa mwaka 2017. *Ili kuungana nao bonyeza linki hizi na chukua namba  hapo za kutoa sadaka yako*

>>Naongea na wewe ambaye hujaokoka yaani Yesu hajawa Bwana na mokozi wa maisha yako, inawezekana una matendo mazuri lakini unamhitaji huyu Yesu maana hatuendi mbinguni kwa kuwa na matendo mazuri bali imani. 

*VIPINDI VYA MAFUNDISHO KATIKA REDIO.*

REDIO SAUTI YA INJILI MOSHI.
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO UPENDO YA DAR ES SALAAM.
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO WAPO YA DAR ES SALAAM.
Kila siku ya Jumatano kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO FARAJA YA IRINGA.
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO FARAJA YA SHINYANGA.
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO UZIMA DODOMA
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO VOICE OF TABORA (V.O.T)
Kila siku ya Jumatano kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

🌂Youtube
https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw

🌂Ustream
http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry
website

*Ili kupata kanda za semina tembelea*

http://www.mwakasege.org/nunua.htm

*Pia ili kusoma summary za semina zilizopita tembelea*

🌂 http://www.gospelkitaa.co.tz
🌂http://www.kanisaforum.com/forums/Mafundisho-ya-Biblia/
     www.facebook.com/felixmbwanji

*UBARIKIWE SANA NA BWANA YESU*

🙋‍♂🙋‍♂🙋‍♂🙋‍♂🙋‍♂🙏🙏🙏🙏

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.