Bwana ni mwema kwa watu wake
Na Apostle Darmacy
Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe…
Soma Luka 19 :29-38
Hapa tumesoma habari ya wanafunzi wawili wa Bwana Yesu waliotumwa kwenda kumfungua mwana-punda aliyekuwa amefungwa.
Bibilia inatuambia wazi kabisa juu ya sifa za mwana-punda huyu;
*Kwanza alikuwa ni mwana-punda aliyekuwa amefungwa.
Yaani yupo kifungoni,
-Mwana-punda ambaye hana uwezo wa kufanya lile alitakalo kulifanya,sababu tu, yupo kifungoni.
-Ni mwana-punda anayetenda kwa shuruti,
yaani si kwa hiyari yake mwenyewe bali ni kwa lazima,
kwa kadri ya matakwa ya bwana zake,kwa sababu tu, yupo kifungoni.
-Mwana-punda huyu ni yule asiye na UHURU wa jambo lolote lile ,kwa sababu tu, yupo kifungoni.
-Mwana-punda huyu ni yule anayeitumikia sheria zilizowekwa juu yake na
mabwana zake kwa sababu tu, yupo kifungoni,Yaani yupo chini ya sheria
kwa sababu yupo kifungoni.
-Mwana-punda huyu aliyefungwa ni yule ambaye hana sauti,yaani hana kibali kwa jambo lolote alifanyalo,
kwa sababu tu,yupo kifungoni.
Lakini leo Bwana asema ana haja na mwana-punda wa namna hii.
“Bwana ana haja nawe.” Nasema ;
“Bwana ana haja nawe.”
Sifa ya pili ya mwana-punda huyu,Biblia inatuambia kwamba mwana-punda
huyu alikuwa ni mwana-punda ambaye hajapandwa na mtu yeyote bado,
hii ikiamaanisha kuwa ni mwana-punda aliyetengwa kwa kusudi ya kazi ya Bwana.
Haleluya…
Jina la Bwana libarikiwe…
Leo hii mahali hapa yupo mwana-punda mmoja aliyefungwa,
Nami nazungumza kwa ajili yake.
Nikukuambia Bwana ana haja nawe,
wewe uliyefungwa ,
Wewe ambaye upo chini ya sheria.
Wewe uliokosa kibali ,
Wewe usiyekuwa na kazi,
Kazi ninayoizungumzia hapa sio kazi ya kupata mkate wa kila siku bali ninazungumzia KAZI ILIYO NJEMA MACHONI PA BWANA,
nayo kazi hiyo iko moja tu ulimwenguni ambayo imedhibitishwa na Mungu mwenyewe ya kuwa ni kazi iliyo njema machoni pake ,
nayo kazi hiyo si nyingine bali ni kazi ya INJILI . Kwa sababu Injili ni
uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza,
na kwa Myunani pia.( Warumi 1 :16)
Kwa habari ya kazi iliyo njema Biblia inatuambia;
Katika matendo 10 :38;
“ habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho
Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, AKITENDA KAZI NJEMA na
kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja
naye.”
Sasa tazama;
Biblia inatuambia katika Luka 19 :30;
“akisema, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia
ndani mtaona mwana-punda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote
bado, MFUNGUENI MKAMLETE HAPA.”
-Jambo moja tunalojifunza hapa kwamba yeyote anayefunguliwa ni lazima apelekwe kwa Bwana Yesu.
Na wala si yeyote Yule bali ni kwa Yesu pekee tazama hapo asemapo MFUNGUENI MKAMLETE HAPA.”
Yaani mahali alipo Yesu ndipo aliyefungwa anapaswa kuwapo
Toa Maoni Hapa Chini