KWA TAARIFA YAKO HII NDIO SIRI YA JOSHUA MLELWA NA MKEWE KUJITOA UPENDO GROUP
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''
KWA TAARIFA YAKO''
ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la
kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia
yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au
kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka
comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu.
KWA TAARIFA YAKO hii leo tunaye mwimbaji aliyejijengea jina kubwa
ndani na nje ya nchi katika tasnia ya muziki wa injili nchini huyu si
mwingine bali ni Joshua Mlelwa ambaye GK inathubutu kusema ndiye alikuwa
akilibeba kundi maarufu nchini la Kijitonyama Upendo Group kabla yeye
na mkewe ambaye pia ni mwimbaji Lilian Mlelwa kujiondoa na mumewe katika
kundi hilo na kuwa waimbaji binafsi.
KWA TAARIFA YAKO kama ulikuwa hujui ni kwamba Joshua ndiye
alikuwa mtunzi mkuu wa nyimbo na mwalimu wa kundi hilo kwa taarifa
ambazo GK ilizipata lakini pia kanda ya kwanza iliyotambulisha vyema
kundi hilo iitwayo "Mungu Anakupenda" asilimia 90 nyimbo zote ni utunzi
wa Joshua na kwamba wakati wanaitoa kanda hiyo walikuwa ndani ya kwaya
ya Uinjilisti Kijitonyama kama GK ilivyowahi kuandika kupitia kipengele
hiki kwa mara ya kwanza kabisa.
KWA TAARIFA YAKO ni kwamba ni
takribani miaka minne sasa tangu Joshua na mkewe wajiondoe ndani ya
kundi hilo ambalo GK inaweza kuthubutu kusema kwamba ndilo lilikuwa
waasisi wakutumia playback na kufanya makundi yote na waimbaji binafsi
kutaka kucheza saana kama waimbaji wa kundi hilo.
 |
| Joshua enzi zake akiwa na Upendo Group wa kwanza kushoto ni mkewe Lilian. |
Sasa watu wengi walikuwa wakijiuliza ni kitu gani kimetokea mpaka wawili
hao kujitoa ndani ya kundi hilo, tofauti na wengi walivyotarajia ama
Watanzania walivyotarajia majibu mareeeefu ama maelezo maaarefu lakini
Joshua alikuwa na majibu mafupi sana akijibu maswali ya wasomaji wa GK
kupitia kipengele cha "Muulize via GK".
KWA TAARIFA YAKO mwimbaji
huyu amesema sababu ya yeye na mkewe kutoka ndani ya kundi hilo
"ilikuwa ni agizo kutoka kwa mwenye kazi (Mungu), mwenye kazi akisema
wingu limeshahama na wewe lazima ufuate agizo la Roho Mtakatifu kwahiyo
nilitii, kifupi ni kwamba nilihama Upendo Group baada ya kutii agizo la
Mungu," alisema Joshua
KWA TAARIFA YAKO mwimbaji huyu na mkewe wanafanana kwa mengi
wawapo jukwaani katika utumishi kwani mkewe alikuwa mshambuliaji mzuri
wa jukwaa toka akiwa ndani ya kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ambako
alikuwa mmoja kati ya masolo wakutegemewa hata walipokuwa ndani ya
Upendo Group kati ya waimbaji waliokuwa wakilipa uhai kundi hilo ni
Joshua na mkewe huyo ambao uchangamfu wao ulikuwa wakipekee.
KWA TAARIFA YAKO
Joshua hivi sasa na mkewe wanaendeleza huduma ya kumsifu Mungu kwa
pamoja na wamekuwa baraka sana kwa watu wengi kupitia nyimbo zao ambapo
wamekuwa wakialikwa katika mikutano ya injili ndani na nje ya nchi.
Toa Maoni Hapa Chini