Vita ya Israel na Iran inaonesha Waisrael 500 watakufa,Vita itachukua siku 30 tu.
Na Apostle Darmacy
Mainjinia wa kivita wa Israeli wamekamilisha mipango yote ya kulivamia
taifa hilo la kiislamu ili kulipokonya uwezo wa kumiliki silaha za
nyuklia, huku mpango vita ukionesha kuwa idadi ya wayahudi watakaopoteza
maisha vitani na wale watakaofikiwa na makombora ya masafa marefu
yakiwepo Scud watafikia 500, huku mapigano yakikadiriwa kuchukua siku
30.
Waziri wa Ulinzi wa Israel, alibainisha hayo wiki iliyopita alipokuwa
akiongea na Gazeti la Maariv la nchini humo, ambapo alieleza kwamba
wanatarajia kufanya uvamizi dhidi ya taifa la Iran mapema mwezi huu wa
Oktoba, na wataanzisha vita vitakavyodumu kwa siku 30, na hilo
litapelekea waisrael wasiopungua 500 kupoteza maisha.
Dokomenti iliyovuja na kunukuliwa na mitandao kadhaa ya Marekani imezua
mijadala mikubwa. Nyaraka hiyo ilikuwa na kichwa kisemacho; 'Israel
prepared' (Israeli imejiandaa) watafiti wa mambo ya usalama wanadai
kuwa, huenda Israel yenyewe imevujisha nyaraka zake hizo ikiwa ni
sehemu ya taarifa ya mangwiji nane walioteuliwa na baraza la Mawaziri
la taifa hilo kuandaa mpango vita na madhara yake.
Inaelezwa kuwa waraka huo unaweza kuwa umeachiwa uvuje kama onyo la
mwisho kwa mataifa ya magharibi yanayosua sua kuidhibiti Iran na
kuipokonya uwezo wa kumiliki silaha hizo za maangamizi makubwa.
Mmoja wa wataalamu hao walioteuliwa kuandaa mpango vita (jina
linahifadhiwa) alisema kuwa mapigano Jeshi la Israeli lina utayari wa
vita kuliko wakati mwingine wowote wa uhai wake na halina cha kusita
linasubiri amri ya utekelezaji kutoka kwa Waziri Mkuu tu.
Kulingana na mpango huo, shambulia la kwanza litahusisha makombora ya
kurushwa kutoka baharini kwenye manuari zinazotumia vipimo vya
setilaiti, yakipiga maeneo 100 kwa wakati mmoja yakiwepo yale ya vituo
vya kurushia makombora kambi za jeshi na miundombinu muhimu ya kivita
na mashambulizi hayo yatakuwa mfululizo nchi nzima kwa saa 48, kisha
ndege vita zisizo na marubani 500, zitaruka kwa pamoja kwenye anga ya
irani na kuleta maangamizi makubwa.
 |
| Waziri Mkuu wa Israel Benjamin wa Netanyahu |
Mpango unaonesha kuwa hawatakuwa na muda wa kusubiri majibizano ya
silaha bali utakuwa ni uvamizi wa moja kwa moja wenye malengo, na
wanategemea msaada mkubwa kutoka katika manuari na meli kubwa za kivita
za Marekani zilizopo ghuba.
Hata hivyo maafisa wa Irani kwa utafiti wao walioufanya walibaini kuwa,
Jeshi la Israeli limejipanga vilivyo kupambana na Iran na wamejipanga
ili kukabiliana nao ikiwezekana kuwazuia ingawa wanakiri kuwa taifa hilo
linateknolojia ya hali ya juu sana hasa katika uwezo wake wa angani.
Nyaraka za siri za Israeli zimeeleza kuwa, oparesheni ya kijeshi itaanza
kuharibu miundo mbinu ya Iran ikifuatiwa na kuteketeza silaha za kivita
kwa kutumia silaha na kumalizikia kwenye vinu vya kinyuklia
zilizotengenezwa na wao.
Marekani na marafiki zake wamekuwa katika juhudi kubwa za kuhakikisha
kuwa zinazuia shambulio la kivita kutoka Israeli kwa kumaliza mgogoro
huo kwa amani, ingawa kikwazo ni mataifa ya Urusi na China ambayo
yamegoma kupitisha azimio kali linaloweza kuilainisha Iran.
 |
| Rais wa Irani Ahmadinejad |
Mwanadiplomasia makini, Jonathan Marcus akielezea uvamizi huo
unaotarajiwa kufanywa na Israel alisema; mbali na ndege zisizokuwa na
rubani, lakini pia kutakuwa na zana zingine ambazo hakutaka kuziweka
wazi kwa kuwa mwisho wa zoezi litaleta hasara kubwa nchini Iran.
Serikali ya Iran na jeshi lake ilisema wazi kuwa, kama litashambuliwa na
Israel au Marekani, italipiza kisasi kwa njia isiyotarajiwa katika
malengo ya mataifa ya maghari kote dunia na kwa hakika dunia itakuwa
mahali pachungu pa kuishi kwa kila mtu.
Akiongea katika mahojiano na Gazeti la Maariv, Jenerali mmoja aliyestafu
mwezi wa nane, mwaka huu na kupelekwa kuwa balozi wa nchi hiyo huko
China, aliyejitambulisha kwa jina moja la Vilnai alisema, Israel
imejiandaa kwa viwango vya juu tofauti na maandalizi yaliyopita.
Jumanne iliyopita, Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu alisema,
matatizo ya kinyuklia yalipelekea Irani kushindwa kufikia makubaliano na
nchi nyingine zenye nguvu duniani zilizokuwa zikipinga mpango huo wa
kinyuklia.
 |
| Waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barak |
Waziri wa ulinzi, Ehud Barak na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu
walipinga vikali maoni ya viongozi wa Wizara ya Ulinzi kwamba waanzishe
mashambulizi dhidi ya Iran kwa siri.
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, na Ehud Barak walieleza kwamba katika
vita itakayotokea kati ya Israeli na Iran, hoja kubwa ni kutafuta
uhalali ili kuwavuta Marekani katika vita.
“Mpango ni mwepesi, Netanyahu na Barak wa Israel wana nguvu za kijeshi
kuishinda Iran kutokana na zana zake za kinyuklia. Na lazima wapigane
ili kukwamisha mpango wa Iran wa kutengeneza silaha za kinyuklia,”
alisema mmoja wa wachambuzi makini.
Rais wa Marekani atakuwa hana uchaguzi ila kuliagiza jeshi lake kujiunga
kupigana vita. Netanyahu alisema kwamba, kama Obama hataki kufanya
hivyo, atashindwa katika uchaguzi na Romney atashika nafasi yake.
Toa Maoni Hapa Chini